Mwili wa Dkt. Mwele Malecela wawasili Tanzania ukitokea Uswisi

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,882
13,171
20220219_033738.jpg
20220219_011426.jpg
Mwili wa marehemu Dr. Mwele Ntuli Malecela umewasili Dar es salaam mnamo saa sita usiku na ndege ya KLM.

Mwili umepokelewa na baba yake mzee Samwel Malecela pamoja na waombolezaji wengi waliogubikwa na huzuni, na waliosubiri uwanjani toka jioni.

Msafara uliekekea moja kwa moja nyumbani kwa mzee Samwel Malecela ambapo sala fupi zilifanyika.

Mzee Abdulrahman Kinana aliyekuwa Katibu Mkuu CCM na Mama Kate Kamba Mwenyekiti wa CCM DSM, walishiriki misa hiyo fupi ya kuupokea mwili nyumbani kwa mzee Malecela.
 
Mange anavyompenda huyu mama, ona sasa hawezi kuja Tanzania hata kumzika mtu alompenda maisha yake yote.hiyo ni kwa sababu ya siasa alizozifanya huko nyuma bado zinamwandama.

Jpm ndo alisema alikuwa mbaya wake na sasa hivi JPM hayupo tena ila Mange alivyoulizwa kama atakuja mazishini, alisema haji anaogopa, najiuliza anaogopa nini? Na sifa anazozimimina awamu hii ya utawala bora? angekuja tu?

Nadhani jana mange niliumia sana kuliko siku zote.maana inaonekana kweli walipendana sana ila ndo hiyo aliishia kuona ndege ikipaa.

Ili uwe salama kaa mbali na siasa kufatilia fatilia hawa wanasiasa sio ishu.
Rip mwele.
 
Si JPM pekee,kachafua watu wengi sana..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
Hata mjomba wake lemutuz ile picha alopostig insta naiwaza bila majibu.

Lemutuz na Mwele damu moja sasa Mwele aliwezaje kuona hiyo picha ikiwa mtandaoni mange akimchafua ndugu yake wa damu? Kweli yapo mengi yanayomfanya Mange asije TZ.
 
Back
Top Bottom