Dk Mwakyembe kurejea India kwa matibabu

Sumasuma

JF-Expert Member
Jun 23, 2011
342
110
Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe anatarajia kuondoka nchini wakati wowote kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu.

Dk Mwakyembe amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi ambayo Oktoba 9 mwaka jana, alilazimika kupelekwa katika Hospitali ya Appolo nchini India kwa matibabu zaidi.

Jana, vyanzo vya karibu na Dk Mwakyembe vilidokeza gazeti hili kwamba naibu Waziri huyo na Mbunge wa Kyela anatarajiwa kurudi Appolo, kwa ajili ya kuangalia kama matibabu aliyopata yameweza kumsaidia kwa kiwango gani.

Vyanzo hivyo vilivyo karibu na Dk Mwakyembe, vilifafanua kwamba anachokwenda kufanya India ni "Uchunguzi tu wa kawaida kuona maendeleo ya matibabu."

"Atarudi katika uangalizi wa kawaida, kwasababu amekuwa akipata matibabu hivyo lazima achunguzwe kuona dawa alizokuwa akitumia zimemsaidia kwa kiwango gani," alisema.

Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Kyela, hivi karibuni alijitokeza na kutoa kauli nzito kuhusu chanzo cha maradhi yanayomsibu, huku Serikali ikiendelea kukaa kimya hata baada ya washirika wake wa karibu kusisitiza kwamba alipewa sumu.

Itakumbukwa kwamba, mwaka jana, Dk Mwakyembe akiwa na hali mbaya alipelekwa katika Hospitali ya Appolo, nchini India kwa matibabu baada ya kuugua maradhi yaliyosababisha ngozi yake kuharibika. Tangu arejee mwanzoni mwa mwezi uliopita alikuwa hajaonekana hadharani, mbali na kutoa tamko kwamba afya yake ilikuwa inaendelea vizuri.

Hata hivyo, muda wote huo aliokuwa nchini India na baada ya kurudi nchini, mazungumzo ya watu maofisini, nyumbani, mitaani na vijiweni yalitawaliwa na utata wa suala la afya ya Dk Mwakyembe, huku uvumi, tetesi na minong'ono kwamba maradhi yake yalisababishwa na hujuma za kisiasa vikitawala hisia za wananchi.

Hisia hizo zilikuzwa na kauli ya mmoja wa washirika wake kisiasa, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta ambaye alimtembelea hospitalini nchini India na baadaye kutoboa hadharani kwamba Dk Mwakyembe alikuwa amelishwa sumu kutokana na msimamo wake dhidi ya mafisadi.

 
Tunamwombea Mungu amsaidie apone. Bwana mwekee mkono wako, fanya maajabu yako kwa mtumishi wako huyu, hana hatia kabisa. Mponye arudi na afya tele. Tumwombee. AMEN.
 
king'ang'anizi tu huyo,si aachie uwaziri tu?he is underperforming and looting our tax money,.

halafu kumbe ukubwa wa baraza la mawaziri ni bure tu,serkali imefanya kazi na bajeti imepita bila perfomance ya mawaziri hawa.mwandosya,mwakwembe etc
 
Pole sana Dr Mwakyembe,tuko pamoja katika kipindi hiki kigumu kwenye maisha yako tunakuombea sana mungu akuponye urudi katika hali yako ya kawaida inauma sana kama ni kweli tumefikia hapa kisiasa!
 
Unanikumbusha novel yako moja Mwakyembe ambayo naipenda sana, 'Pepo ya mabwege'.
Hivi katika siasa hakuna pepo ya mabwege kweli?
Nalifikiria sana hili!
 
pole sana mzee mwakyembe ila kitu kimoja ninacho taka kufaham, nini unachohofia mpaka unaficha maovu yaliyoko kwenye chama na serikali yako, ni njaa ama unafiki? Unabaki kusema tu utakuja kusema, hiyo itakua lini? Acha upumbavu
 
Wish u a quick recovery! Baada ya hapo naamini utaujulisha umma kama yapo ambayo unaona yanafaa kujulisha umma kwa ujumla
 
king'ang'anizi tu huyo,si aachie uwaziri tu?he is underperforming and looting our tax money,.

Wewe ukiugua muajairi wako anatakiwa akuondoe kazini ama akusaidie upone uendelee na kazi hebu kuweni na utu ama wewe umehusika kumpa Sumu Mwakyembe?!! mijitu mingne inakera sana kabisa!!! mtu anaumwa wewe unasema kinganganizi!! kangangania nini sasa!!! nenda kasome vzr sheria za ajira uone zinasemaje!!!
 
Huu upenzi wa Mwakyembe kwa chama ni wa aina yake!...Kama mtu anaweza kulostishwa kiasi hicho, na bado anakuwa mzalendo wa chama....ishu ni uwaziri au?!
Anyweiz labda anangoja atibiwe apone, ndipo atangaze nia!
 
Ajafa tu huyo snitch?
'wataalam' wa polonium mbona mnamchelewesha huyo?
Mwaisheni akapumzike mapema na 'siri' zake za Richmond.
 
Back
Top Bottom