Dkt. Mwakyembe aandika waraka wa siri!

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898
AUSAMBAZA KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI ZAKE WA KARIBU

NAIBU Waziri wa Ujenzi anayeugua ugonjwa uliozusha utata mkubwa serikalini, Dk. Harrison Mwakyembe, ameandika waraka mahususi unaoeleza kile anachokiamini kuwa ni chanzo cha ugonjwa wake, Tanzania Daima Jumatano limebaini. Waraka huo ambao gazeti hili limeuona mbali ya kueleza kile ambacho Mwakyembe mwenyewe anaamini kuwa ni chanzo cha ugonjwa wake, unaeleza pia jinsi alivyoanza kuugua, watu anaowashuku kuwa nyuma ya mpango huo, siku na tarehe aliyodhani kuwa ndiyo aliyowekewa sumu hiyo.

Kama hiyo haitoshi, Mwakyembe katika waraka wake huo pasipo kueleza chanzo halisi cha undani wa taarifa zake, anaeleza mbinu iliyotumika kumdhuru na mahala mpango huo wa kumdhuru ulipopangwa. Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba Dk. Mwakyembe ambaye kwa sasa yuko nchini India ameusambaza waraka huo kwa ndugu, jamaa na marafiki zake wa karibu. Katika waraka huo, Dk. Mwakyembe anaeleza kwamba anaamini alipewa sumu hiyo akiwa ofisini kwake huku akitaja majina ya watu anaowatuhumu kuwa nyuma ya mpango huo ambao gazeti hili kwa sasa linahifadhi majina yao.

Kwa mujibu wa Dk. Mwakyembe, mara tu baada ya kuwekewa sumu hiyo alianza kuwashwa mwili kabla ya hali kuendelea kuzorota na kuwa mbaya. Akionekana kujibu hoja za Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, mwanasiasa huyo katika waraka wake anaeleza kwamba hakuwekewa sumu hiyo kwenye chakula, bali kwenye sabuni na kitaulo cha kujifutia, ambacho huwekwa kwenye chumba maalumu ofisini kwake kwa ajili ya kusafisha mikono na huduma nyingine awapo ofisini.

Vyanzo vyetu vya habari kutoka kwa ndugu na marafiki wa karibu wa Dk. Mwakyembe vilisema kuwa, naibu waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kyela, amefikia hatua ya kuandika waraka huo kwa lengo la kutaka kuijulisha familia yake na taifa kile anachoamini anakabiliana nacho endapo atapoteza maisha kabla ya ukweli kamili kubainishwa. Hata hivyo, kutokana na ukweli kwamba suala hilo la afya ya Dk. Mwakyembe liko katika hatua za uchunguzi, Tanzania Daima Jumatano haliwezi kuandika kwa undani kuhusu waraka huo kwa sasa.

Ukiacha hilo, Dk. Mwakyembe katika waraka huo ameelezea historia ya maisha yake kisiasa na mikasa iliyompata kiasi cha kujijengea maadui.Ameeleza jinsi alivyonusurika kuuawa mara kadhaa na kwamba taarifa zote za mikasa yake aliziripoti polisi, lakini hakuna hatua zilizochukuliwa na Jeshi hilo la Polisi.

Baadhi ya mikasa aliyoitaja kwenye waraka huo ni pamoja na tukio la kunusurika kuuawa kwenye ajali ya gari iliyotokea Mei 21, mwaka 2009. Ajali hiyo ilitokea eneo la Ihemi, kilomita 40 kutoka Iringa mjini akiwa safarini kutokea Mbeya kwenda Dar es Salaam. Kwa mujibu wa waraka huo, gari alilokuwa akisafiria aina ya Toyota Land Cruiser T 362 ACH, liliacha njia saa moja asubuhi baada ya kukanyaga shimo na tairi ya upande wa kulia kuchomoka na dereva wake, Joseph Msuya (30), kupoteza mwelekeo kabla ya gari hilo kutoka nje ya barabara upande wa kushoto na kuparamia mti kisha kupinduka.

Ajali hiyo ilitokea wakati dereva wa Dk. Mwakyembe akijaribu kulipita lori kabla ya kukanyaga shimo hilo. Anasema katika ajali hiyo aliokolewa na wasamaria wema pamoja na trafiki wawili waliokuwa kwenye basi dogo waliokuwa wakisafiri kutoka Iringa kwenda Njombe. Anasema katika waraka huo kuwa, baada ya ajali hiyo alilazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa kutokana na kuumia taya kisha alihamishiwa Dar es Salaam kwa matibabu zaidi. Kwa mujibu wa waraka huo, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, aliunda tume iliyoongozwa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani wakati huo, Kamanda James Kombe, kuchunguza chanzo cha ajali hiyo.

Matokeo yalionesha kwamba ilisababishwa na uzembe wa dereva wake, Msuya wakati Dk. Mwakyembe akiamini kwamba ajali hiyo ilipangwa.Februari 9, mwaka 2011, Dk. Mwakyembe aliandika barua kwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema, akimpa taarifa juu ya kuwapo kwa njama za kutaka kumuua yeye pamoja na viongozi wengine.

Wengine aliowataja katika barua hiyo ni pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela. Katika orodha hiyo ya Mwakyembe kwa IGP, hadi sasa kiongozi mwingine ambaye anaumwa ni Profesa Mark Mwandosya.
 
naskia alishawahi kuzidiwa tena hata kabla ya hii issue ya india, akaenda kutibiwa

hivi ile ilikua sumu?
 
huku akitaja majina ya watu anaowatuhumu kuwa nyuma ya mpango huo ambao gazeti hili kwa sasa linahifadhi majina yao

Vyanzo vyetu vya habari kutoka kwa ndugu na marafiki wa karibu wa Dk. Mwakyembe vilisema kuwa, naibu waziri huyo ambaye pia ni Mbunge wa Kyela, amefikia hatua ya kuandika waraka huo kwa lengo la kutaka kuijulisha familia yake na taifa kile anachoamini anakabiliana nacho endapo atapoteza maisha kabla ya ukweli kamili kubainishwa. Hata hivyo, kutokana na ukweli kwamba suala hilo la afya ya Dk. Mwakyembe liko katika hatua za uchunguzi, Tanzania Daima Jumatano haliwezi kuandika kwa undani kuhusu waraka huo kwa sasa.
Hapana ndugu mhariri, huo ni uharo na uongo mkubwa!

Umeshasema kwamba ndugu wa Mwakyembe wenyewe wamekwambia kwamba nia ya kuandikwa waraka huo ni kuliambia taifa kilichojiri, huwezi tena ukageuka ukasema habari haitakiwi kuwekwa wazi eti kwa sababu ya uchunguzi, wewe mhariri na waandishi wako you don't know what you are doing at your job, tena waongo wakubwa, huna hakika na unachoandika, mmeenda shule ya journalism ya chini ya miembe, vilaza wakubwa!

Umesema yeye mwenyewe Mwakyembe "amesambaza" waraka wenye majina ya watuhumiwa, itakuwaje tena wewe ndio uogope kutaja kile ambacho tayari kimeshatajwa? Tuna uhuru wa vyombo vya habari tatizo wahariri waoga, uozo! Halafu hakuna competition, ingekuwa Tanzania Daima wanajua kwamba wao wasipoanika huo waraka basi chombo kiingine kitaandika wangewahi kuuchapa, lakini ndio hivyo tena, hatuna waandishi wa kweli kwenye press Tanzania, nazi tupu!
 
Aache longolongo mbona ripoti ya madaktari haiweki hewani na sisi tuione . Huyu jamaa naona anatuyeyusha tuu ili apate huruma ya wananchi hajawekewa sumu huyu liongo tuu
 
Mhariri anasababu za kutotoa Majina kwa sasa,hata ungekua wewe ndiye mhariri usingedhubutu kutoa kuna sababu nyingi za kufanya hivyo.
 
Hapana ndugu mhariri, huo ni uharo na uongo mkubwa!

Umeshasema kwamba ndugu wa Mwakyembe wenyewe wamekwambia kwamba nia ya kuandikwa waraka huo ni kuliambia taifa kilichojiri, huwezi tena ukageuka ukasema habari haitakiwi kuwekwa wazi eti kwa sababu ya uchunguzi, wewe mhariri na waandishi wako you don't know what you are doing at your job, tena waongo wakubwa, huna hakika na unachoandika, mmeenda shule ya journalism ya chini ya miembe, vilaza wakubwa!

Umesema yeye mwenyewe Mwakyembe "amesambaza" waraka wenye majina ya watuhumiwa, itakuwaje tena wewe ndio uogope kutaja kile ambacho tayari kimeshatajwa? Tuna uhuru wa vyombo vya habari tatizo wahariri waoga, uozo! Halafu hakuna competition, ingekuwa Tanzania Daima wanajua kwamba wao wasipoanika huo waraka basi chombo kiingine kitaandika wangewahi kuuchapa, lakini ndio hivyo tena, hatuna waandishi wa kweli kwenye press Tanzania, nazi tupu!

UKWELI utajulikana lakini si vizuri tukaanza kutoa tuhuma kwa vitu tusivyo na uhakika, mwakyembe ni mgonjwa uenda hali hiyo ndo inamfanya atoe shutuma zisizo na UKWELI. Mungu ndo anajua sina iman sana na viongozi wa CCM, wanatafuta umaruhufu tu.
 
Watu wengine sijui vipi?! Mtu umeambiwa ripoti na majina haviwezi kuwekwa hadharani kwa sasa kwa sababu uchunguzi unaendelea watu wanakosoa tu utadhani hawaelewi.

Tanzania Daima kwa level hii wametoa clue tu ya hicho alichoandika Mwakyembe hawajaingia kiundani na ndio maana hakuna ndugu wala Mwakyembe mwenyewe aliyekuwa quoted kuhusu huo waraka
 
Aache longolongo mbona ripoti ya madaktari haiweki hewani na sisi tuione . Huyu jamaa naona anatuyeyusha tuu ili apate huruma ya wananchi hajawekewa sumu huyu liongo tuu
Yaani unataka ripoti ya ugonjwa wa Mwakyembe iwe hewani? Halafu ikishakuwa hewani wewe itakusaidia nini? Kikubwa unachotakiwa kujua ni kuwa AMEWEKEWA SUMU
 
Yani unataka ripoti ya ugonjwa wa Mwakyembe iwe hewani? Halafu ikishakuwa hewani wewe itakusaidia nini? Kikubwa unachotakiwa kujua ni kuwa AMEWEKEWA SUMU
Pole sana ujui usemalo, Tatizo la ugonjwa alionao mwakiembe linagusa public interest na limegubikwa na mazingira tata hivyo kwa nchi makini inayojali na kulinda watu waake na kuwathamini

haiwezi ikawa bubu kiasi hicho lazima ingetoa tamko na uchunguzi wa kina wa jopo la madaktari na vyoma vya usalama kushirkiana ili kulinda mstakabali wa raia wake, Ikiwa hayo alifanyiwa kiongozi katitaka serekali namna gani raia wa kawaida? huoni kua hali hii ikiachiwa athari zake ni kubwa kwa amani ya nchi na watu wake?

Huoni ikiwa kunawatu wamefikia hatua kunyweshana sumu hakuna tofauti na mtandao wa kigaidi ambao kwa nchi makini laziama upelelezi wakiaitelejensia ungefanyika?

Tukiacha ushabiki hili si jambo dogo hata kidogo hebu jiweke katika position ya Mwaikiembe then uone kama ni wewe ungefanya nini na serekali yako inayopaswa kulinda raia wake ndiyo hiyo tena haina msaada na wewe inakutumia kama kondom then hainampango na wewe eti kwa jibu rais tunahifadhi siri ya mgonjwa ****** mtupu.
 
Please mkuu The Invisible
Tayari Dr Mwakyembe amesha toa waraka wa siri,kwa kupitia JF na kwa kuwa tunaelezwa JF ni mahala pa kusema ukweli na uwazi pasi kumung'unya maneno. Tunakuomba utuletee waraka huo ili tuweze kuusoma. Kwani tayari baadhi ya ndugu na jamaa wa Dr. wanao waraka huo na hata baadhi ya magazeti wamejaribu kudodosa yaliyo andikwa ndani ya waraka huo
 
Hivi sasa ni kumwaga tu. Wengine wamemwaga Ugali na tena kuna wanaomwaga mboga na sasa yanamwagwa Maji ya kunywa. Haya ngoja tuone.
 
Back
Top Bottom