Dk. Mwaka afutiwa kibali cha utoaji tiba asili na tiba mbadala, wengine wasimamishwa miezi 6

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
image.jpeg


Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, limekifutia usajili wake wa kutoa huduma za kitabibu, Kituo cha Tiba Asilia cha ForePlan Kliniki iliyopo Ilala Bungoni jijini Dar es salaam, kinachomilikiwa na Dkt. Juma Mwaka maarufu kama Dkt. Mwaka, kwa madai kuwa kimekiuka taratibu za kitabibu na tiba mbadala

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dkt. Edmund Kayombo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ukumbi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

========

DK. MWAKA AFUTIWA KIBALI CHA UTOAJI WA HUDUMA ZA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA, WENGINE WASIMAMISHWA MIEZI SITA

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, limekifutia usajili wake wa kutoa huduma za kitabu, Kituo cha Tiba Asilia cha ForePlan Kliniki iliyopo Ilala Bungoni jijini Dar es salaam, kinachomilikiwa na Dkt. Juma Mwaka maarufu kama Dkt. Mwaka, kwa madai kuwa kimekiuka taratibu za kitabu za tiba asili huku akiwa ameonywa na kushindwa kubadilika.

Akizungumza jijini Dar es salaam leo katika Mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk. Edmund Kayombo amesema kuwa kufutiwa kibali cha Dk. Mwaka kunatokana na sababu nyingi ambazo amekuwa akikiuka licha ya kupewa maonyo na barua juu ya utoaji huduma zake.

Amesema sababu nyingine ni kuwa katika matangazo yake amesema anatoa tiba za kisasa wakati hiyo elimu hana ya kufanya huo.
1%25285%2529.JPG

Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala , Dk. Edmund Kayombo akizungumza na waandishi habari juu hatua walizozichukua kwa watoaji huuduma tiba asili na tiba mbadala leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Msajili Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Ruth Suza kushoto ni Kaimu Mkurugenz Msaidizi wa Huduma na Tiba Mbadala, Paulo Muhame.

Wengine waliofutiwa usajili ni Fadhaget Sanitarium kinachoendeshwa na Tabibu Fadhili Kabujanja pamoja na Mandai Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Abdallah Mandai

Hata hivyo limetoa adhabu mbalimbali kwa kituo cha Aman Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Esbon Baroshigwa, na Tabibu Castory Ndulu wa Kituo cha Ndulu Herbal Clinic wamepewa barua ya onyo.

Aidha wengine wamesimashwa kwa miezi sita ambao ni Tabibu John Lupimo wa Lupimo Suntarium Herbal Clinic pamoja na Tabibu Simon Rusigwa wa Sigwa Herbal Clinic.
2%25282%2529.JPG

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma na Tiba Mbadala, Paulo Muhame akizungumza na waandishi habari juu ya utekelezaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa wanaokiuka taratibu za utoaji huduma wa tiba asili na tiba mbadala katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala , Dk. Edmund Kayombo kulia ni Msajili Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Ruth Suza.

Dk. Kayombo amesema kuwa wale wote ambao wamepewa onyo pamoja na kusimamishwa wametakiwa wasiingie mikataba na vyombo vya habari kwa ajili ya Matangazo

Amesema kuwa waliofutiwa walifuata taratibu zote ikiwa kuwahoji na kujiridhisha kuwafutia kibali cha utoaji wa huduma za tiba asili na tiba mbadala.Imeandikwa na Chalila Kibuda.
 
View attachment 365540

Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, limekifutia usajili wake wa kutoa huduma za kitabibu, Kituo cha Tiba Asilia cha ForePlan Kliniki iliyopo Ilala Bungoni jijini Dar es salaam, kinachomilikiwa na Dkt. Juma Mwaka maarufu kama Dkt. Mwaka, kwa madai kuwa kimekiuka taratibu za kitabibu na tiba mbadala

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dkt. Edmund Kayombo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ukumbi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Naomba ufanye marekebisho isomeke Kitibabu, otherwise ngoja tuone ngoma itakavyokwenda kuisha, je sterling atauwawa??
 
Ngoja tuone je wizara ya afya watapiga makufuli au wataacha hivyo hivyo je Mwaka atasemaje maana ishu ya kigwa alipata watetezi je hii
 
Serikali imefungia kituo cha tiba asilia cha Foreplan kinachomilikiwa na Tabibu Juma Mwaka Juma kwa kukiuka masharti ya kibali alichopewa kwa kujitangaza kuwa anatoa tiba za kisasa badala ya matibabu ya asilia.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti Wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Dkt. Edmund Kayombo amesema kuwa kituo hiko kimefutiwa usajili na hakiruhusu kutoa huduma za tiba asilia na Tiba mbadala kwa jamii kwa kutokidhi masharti ya usajili na kufanya kazi kinyume cha usajili wake.

“Kuanzia hivi sasa tumekifutia usajili kituo cha tiba asili na tiba mbadala cha Foreplan kwa kukiuka masharti ya usajili na hivyo hakiruhusiwi kutoa huduma kwa jamii na watanzania kwa ujumla”.alisisitiza Dkt. Kayombo.

Aidha Dkt. Kayombo ameongeza kuwa vituo vingine vilivyofungiwa kutoa huduma ni pamoja na Tabibu Abdallah Mandai wa Mandai Herval Clinic na kituo cha Fadhaget Sanitarium Clinic kinachomilikiwa na tabibu Fadhil Kabujanja.

Dkt. Kayombo aliendelea kwa kusema kuwa, ukiacha waliofungiwa kutoa huduma pia vipo vituo vilivyofungiwa kwa miezi sita kila kimoja kama vile tabibu Simon Rusigwa wa kituo cha Sigwa Herbal Clinic na Tabibu John Lupimo wa kituo cha Lupimo Sanitarium Clinic.

Mbali na hayo Dkt. Kayombo amesema kuwa huduma za tiba asili na tiba mbadala zinagusa zaidi maisha na afya za wananchi moja kwa moja na hivyo sio vyema zikaachwa ziendeshwe kiholela bila utaratibu wa kitaalamu na kimaadili.

“Kutokana na huduma hizo kutolewa kiholela, waratibu wote mnatakiwa kufuatilia na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waganga wote ambao hawajajisajili na kutoa taarifa katika Ofisi ya Msajili wa Baraza la tiba asili na tiba mbadala kwa kila hatua iliyochukuliwa” aliongeza Dkt. Kayombo.

Aidha Dkt. Kayombo amesisitiza kwamba kila mtoa huduma lazima asajiliwe yeye mwenyewe, wasaidizi wake pamoja na kituo chake cha kutolea huduma kupitia ofisi za Mganga Mkuu wa Halmashauri husika.
 
Back
Top Bottom