Dk Kigwangalla aeleza sababu za mawaziri kung’oka Maliasili

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,446
7,817
Kwa ufupi

Kigwangalla anasema rushwa katika ugawaji vitalu; migogoro ya ardhi kati ya wananchi na hifadhi na utoaji vibali vya uvunaji magogo ndizo sababu kuu zilizowaondoa watangulizi wake.
By Daniel Mjema, Mwananchi dmjema@mwananchi.co.tz

Dk Hamisi Kigwangalla amekuwepo ndani ya Baraza la Mawaziri kwa takriban miaka miwili, na amemaliza mwezi mmoja tangu ateuliwe kuwa waziri wa Maliasili na Utalii, lakini anajua siri tatu ambazo zimekuwa zinawang’oa mawaziri waliomtangulia.

Wizara hiyo pamoja na iliyokuwa ya Nishati na Madini, ambazo ni sekta nyeti katika uchumi wa Tanzania zinaongoza kwa mawaziri wake kung’oka kutokana na kashfa za ufisadi, kutosimamia vizuri maliasili, mikataba mibovu na wizi.

Baadhi ya mawaziri waliondolewa baada ya kutumikia kwa muda mfupi.

Na hata suala la uwekezaji katika eneo la Loliondo ambalo limekuwa na mgogoro wa muda mrefu, waziri huyo anasema anajua sababu za mgogoro huo na anadai ana orodha ya watu waliowekwa mfukoni na mwekezaji wa eneo la Loliondo kutoka Falme za Kiarabu (UAE), ambaye ameahidi kuikabidhi Takukuru.

Waziri huyo alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake eneo la Area D mjini Dodoma.

Rushwa kwenye vitalu

Dk Kigwangalla alisema rushwa na upendeleo katika ugawaji wa vitalu zinachangiwa na mfumo uliojengwa katika kifungu namba 38 cha Sheria ya Wanyamapori ya mwaka 2005 kinachozungumzia ugawaji wa vitalu.

Alisema utaratibu uliowekwa Loliondo ni ukodishaji wa kiutawala, ambao unataka kuwapo na kamati ya ushauri wa ugawaji wa vitalu ambayo hufanya takwimu ya watu wanaovihitaji na baadaye kumshauri waziri.

Lakini anasema kumekuwapo na washauri ambao wanapewa rushwa na waombaji.

“Mawaziri wanakaa kwenye kiti moto kwa sababu mwisho wa siku watafanya uamuzi wa kugawa vitalu nao watahusishwa kwa sababu mwisho wa siku watagawa vitalu wenyewe kwa kalamu zao,” alisema Dk Kigwangalla.

“Anaweza kumpa mtu kitalu kwa uamuzi wake kwa sababu atagawa yeye, ama anaweza kugawa kwa sababu ameshawishiwa kwa namna yoyote ile. Si lazima kwa kutumia fedha.”

Kwa hiyo, Dk Kigwangalla alisema mfumo ndio tatizo kwa sababu unaruhusu mtu mmoja afanye uamuzi.

“Mfumo wa namna hiyo unajenga mazingira ya rushwa. Inawezekana hata rushwa isiwapo. Inawezekana hata upendeleo usiwapo, lakini ule mfumo tu ulivyokaa unajenga shaka,” alisema.

Alisema mawaziri wengi hawakubadilisha utaratibu kwa kuwa unawapa mamlaka, lakini kwa wale wanaopenda kupokea rushwa unawapa fursa.

Dk Kigwangalla alisema baada ya kuteuliwa aliipitia sheria na kutafuta sababu ya mawaziri wengi kuanguka na akagundua mojawapo ni mtego ulioko katika ugawaji wa vitalu.

“Nilipogundua hilo nikasema mimi sitagawa vitalu kwa njia hiyo,” alisema naibu waziri huyo wa zamani wa Wizara ya Afya.

“Nitabadilisha utaratibu. Niligundua utafiti umefanywa ambao ulipendekeza tutumie njia ya mnada wa wazi. Mfano kitalu cha daraja la kwanza kinaweza kuuzwa hadi Dola 2 milioni za Kimarekani ambazo ni karibu Sh4 bilioni za Tanzania. Lakini sisi tunakiuza kwa Dola 60,000 ambazo ni kama Sh120 milioni,” alisema.

“Si hizo tafiti tu, lakini maelekezo yaliyopo katika Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo (2016-2021) na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) wamependekeza twende kugawa vitalu kwa mnada.”

Alisema kundi jingine lenye masilahi katika utaratibu huu ni wamiliki wa vitalu kwa sababu utaratibu wa zamani unatoa fursa ya wanaohitaji kujadiliana na wagawaji.

“Ukishajuana na wale wanaohusika na ugawaji vitalu unajihakikishia kukipata. Kwa hiyo, nikaamua kufuta ugawaji wa vitalu uliofanyika kwa vile ulikuwa kinyume cha sheria. Vitalu vilitakiwa vigawanywe mwishoni mwa 2017, lakini viligawanywa mwanzo mwa 2017. Mchakato ulikuwa batili na mimi nikaufuta ili tuweke uwanja mpya wa kugawa vitalu kwa mnada,” alisema.

Waziri Kigwangalla alisema tayari ameanza mchakato wa kubadili sheria na kanuni na kama Bunge na Rais wataridhia na kupitisha sheria, atagawa vitalu kwa njia ya mnada.

Waziri huyo alitaja kundi jingine linalonufaika kuwa ni watu wenye mtandao ndani ya Serikali ambao huchukua kitalu kwa dola 60,000 za Kimarekani (sawa na Sh120 milioni) na kukikodisha kwa kati ya dola 200,000 hadi 500,000.

“Ni kama walikuwa wanafanya biashara ya kukodisha na wao wanapata kodi. Niliposema nafuta huo mchakato, kumetokea mtafaruku mkubwa katika sekta ya uwindaji wa kitalii,” alisema.

Alisema wadau hao wameamua kumshambulia, lakini wakienda kwenye mnada watakuwa wametatua jambo moja ambalo limekuwa likiwaangusha mawaziri wengi.

Utoaji vibali vya kuvuna magogo

Dk Kigwangalla alitaja sababu nyingine iliyowaangusha mawaziri waliomtangulia ni ugawaji wa vibali vya kukata magogo, ambayo yanatafutwa duniani.

“Mti ambao ni maarufu sana China na Mashariki ya Mbali ni mkulungu. Ukiwa na mkulungu hapa ukipiga simu Wachina wanapanda ndege saa hiyohiyo kuja kuununua,” alisema.

Alisema mti huo unavunwa kwenye mapori ya Tabora na Katavi kwa kiasi kikubwa.

“Mawaziri wengi wamekuwa wakifanya kazi ya kukata magogo au wakitumia watu wao wa karibu na wakishapata vibali wanaviuza. Wakati mwingine wanawapa marafiki zao vibali,” alisema.

“Hii nchi haina siri. Ni imara sana katika kukusanya taarifa za kiitelijensia. Vyombo vyetu hupata taarifa hizi za deal chafu. Hili ni eneo linawaangusha sana mawaziri.”

Migogoro ya wafugaji na hifadhi

Dk Kigwangalla alitaja eneo jingine kuwa ni migogoro kati ya wafugaji na mamlaka zinazosimamia maeneo yaliyohifadhiwa kisheria.

“Usiposhughulika nayo vizuri ni maeneo ambayo yatakuangusha. Ukumbuke idadi ya watu wetu imeongezeka, lakini eneo haliongezeki. Watu wetu hawafugi kisasa,” alisema.

Alisema kwa miaka ya karibuni kumekuwa na usimamizi mkali wa maeneo yaliyohifadhiwa kwa sababu hilo lisipofanyika nchi itaelekea kuwa jangwa.

“Ukiendesha tu operesheni halali, lazima moto uwake bungeni kwa sababu unagusa masilahi ya wananchi na ambayo ndiyo masilahi ya wabunge na iwe isiwe watakuchukia tu,” alisema.

Hongo kwa mawaziri

Dk Kigwangala alisema ana orodha ya watu waliowekwa mfukoni na mmoja wa wamiliki wa Loliondo.

Alisema amejiridhisha na kuna mtumishi mmoja wa wizara yake ambaye ni kiungo.

“Nimeona (mtu ambaye ni kiungo na mwarabu) atatuvuruga kadri tunavyoendelea,” alisema.

“Anavujisha siri za Serikali na anaweza hata kuhatarisha maisha yetu, maana tunashughulika na majangili na watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha. Ni jambo la hatari sana kwa maisha yetu.

“Ninalipeleka jambo hili Takukuru, wakithibitisha wachuke hatua na wakiona hahusiki basi wamwachie,” alisema Dk Kigwangalla bila kumtaja kwa jina ofisa huyo.

Apongeza watangulizi wake

Hata hivyo, Dk Kigwangalla amewapongeza mawaziri waliomtangulia kwa kazi waliyoifanya katika kupambana na ujangili na majangili.

“Katika maeneo ambayo watangulizi wangu wamefanya kazi kubwa ni suala la ujangili. Idadi ya wanyamapori imeongezeka,” alisema.

“Ninaona katika kazi ambazo sasa nitapambana nazo ni malalamiko ya wabunge, madiwani na wananchi kuhusu wanyamapori kuingia katika maeneo yao kwa sababu wameongezeka,” alisema.

“Kila siku napokea simu za taarifa za mafanikio ya vita ya ujangili lakini siwezi kuziweka wazi kwa sababu ya kiintelijensia. Nina taarifa nyingi za watu wengi wanaojishughulisha na ujangili.”

Mikataba ya hoteli

Akizungumzia mchakato aliouanzisha wa kutwaa hoteli ambazo uendeshaji wake unakiuka mikataba ya uuzaji, Dk Kigwangalla alisema hoteli 10 kati ya 17 zilizobinafsishwa zitatwaliwa na Serikali.

“Mikataba iliyoingiwa (ina maelezo) ya namna ya kuivunja kama mwekezaji hatazingatia matakwa ya mikataba. Tangu zimenunuliwa hadi leo, 10 kati ya 17 hazijakidhi masharti ya mauzo,” alisema.

“Ndiyo nikasema kuna kila sababu ya kuzirudisha ndani ya Serikali ili watafutwe wawekezaji wapya ambao watakidhi masharti ya uendeshaji. Tutawakodishia wawekezaji makini,” alisema na kuongeza kuwa kuna mpango wa kuanzisha hoteli mpya 20 katika maeneo ya hifadhi.
 
Kigwangala aweke Akiba ya Maneno

Kigwangala hawezi kuaminika kwa Magu kwanViwango vya Charles Kitwanga na Ombeni Sefue
 
Nadhani kila wizara, idara, shirika na sehemu mbali mbali huo ndiyo ulikuwa utaratibu. Rushwa tuuu. Naamini hata yeye analijua hilo. Nampongeza kwa kuonyesha nia. Lakini hii ni wizara moja tuu na initiative ya waziri mmoja. Nadhani hii vita ya kuirekebisha nchi ingefanywa kwa approach tofauti kabisa. Naendelea kufikiri the best way or approach...
 
ina maana hayo yote kigwangala ndo kayaona wengine walikuwa vilaza huyu katumwa huyu kuua soo ya kukimbiwa ........................... hata kama walikuwa wapi eti mpaka kigwangala kahamia maliasili ndo ameona uongooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
na kama ni kweli wamchukulie hatua hatutaki porojo zao tangu kitambo anasakamwa Lowassa na mpaka sasa sijasikia hata kaparuliwa sanasana wanamlinda ile mbaya
 
Vizuri

Hapa kazi tu

Ila kila akiongea hizo nita.. nita.. nyingi abadili siku ingine tumsome au kumsikia akianzia nili.. nili..

Tujue kweli anayosema yametendeka sio nita nita then hatupati updates tena na mahakama ya mafisadi ilivyo.. mpaka leo mimi sijasikia juu ya kesi yake hata moja.

Awamu ya tano inanikumbusha mchaka mchaka wa asubuhi.
 
Kila Mjuzi kuna Mjuzi zaidi yake.., ila atambue kuwa baadhi ya hao waliopita hapo kulikuwa na Wajuzi zaidi yake hivyo kila alifanyalo aweke na tahadhari pia!
 
Kwa ufupi

Kigwangalla anasema rushwa katika ugawaji vitalu; migogoro ya ardhi kati ya wananchi na hifadhi na utoaji vibali vya uvunaji magogo ndizo sababu kuu zilizowaondoa watangulizi wake.
By Daniel Mjema, Mwananchi dmjema@mwananchi.co.tz

Dk Hamisi Kigwangalla amekuwepo ndani ya Baraza la Mawaziri kwa takriban miaka miwili, na amemaliza mwezi mmoja tangu ateuliwe kuwa waziri wa Maliasili na Utalii, lakini anajua siri tatu ambazo zimekuwa zinawang’oa mawaziri waliomtangulia.

Kigwangalla anasema rushwa katika ugawaji vitalu; migogoro ya ardhi kati ya wananchi na hifadhi na utoaji vibali vya uvunaji magogo ndizo sababu kuu zilizowaondoa watangulizi wake.

Wizara hiyo pamoja na iliyokuwa ya Nishati na Madini, ambazo ni sekta nyeti katika uchumi wa Tanzania zinaongoza kwa mawaziri wake kung’oka kutokana na kashfa za ufisadi, kutosimamia vizuri maliasili, mikataba mibovu na wizi.

Baadhi ya mawaziri waliondolewa baada ya kutumikia kwa muda mfupi.

Na hata suala la uwekezaji katika eneo la Loliondo ambalo limekuwa na mgogoro wa muda mrefu, waziri huyo anasema anajua sababu za mgogoro huo na anadai ana orodha ya watu waliowekwa mfukoni na mwekezaji wa eneo la Loliondo kutoka Falme za Kiarabu (UAE), ambaye ameahidi kuikabidhi Takukuru.

Waziri huyo alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki katika mahojiano maalumu na gazeti hili nyumbani kwake eneo la Area D mjini Dodoma.

Rushwa kwenye vitalu

Dk Kigwangalla alisema rushwa na upendeleo katika ugawaji wa vitalu zinachangiwa na mfumo uliojengwa katika kifungu namba 38 cha Sheria ya Wanyamapori ya mwaka 2005 kinachozungumzia ugawaji wa vitalu.

Alisema utaratibu uliowekwa Loliondo ni ukodishaji wa kiutawala, ambao unataka kuwapo na kamati ya ushauri wa ugawaji wa vitalu ambayo hufanya takwimu ya watu wanaovihitaji na baadaye kumshauri waziri.

Lakini anasema kumekuwapo na washauri ambao wanapewa rushwa na waombaji.

“Mawaziri wanakaa kwenye kiti moto kwa sababu mwisho wa siku watafanya uamuzi wa kugawa vitalu nao watahusishwa kwa sababu mwisho wa siku watagawa vitalu wenyewe kwa kalamu zao,” alisema Dk Kigwangalla.

“Anaweza kumpa mtu kitalu kwa uamuzi wake kwa sababu atagawa yeye, ama anaweza kugawa kwa sababu ameshawishiwa kwa namna yoyote ile. Si lazima kwa kutumia fedha.”

Kwa hiyo, Dk Kigwangalla alisema mfumo ndio tatizo kwa sababu unaruhusu mtu mmoja afanye uamuzi.

“Mfumo wa namna hiyo unajenga mazingira ya rushwa. Inawezekana hata rushwa isiwapo. Inawezekana hata upendeleo usiwapo, lakini ule mfumo tu ulivyokaa unajenga shaka,” alisema.

Alisema mawaziri wengi hawakubadilisha utaratibu kwa kuwa unawapa mamlaka, lakini kwa wale wanaopenda kupokea rushwa unawapa fursa.

Dk Kigwangalla alisema baada ya kuteuliwa aliipitia sheria na kutafuta sababu ya mawaziri wengi kuanguka na akagundua mojawapo ni mtego ulioko katika ugawaji wa vitalu.

“Nilipogundua hilo nikasema mimi sitagawa vitalu kwa njia hiyo,” alisema naibu waziri huyo wa zamani wa Wizara ya Afya.

“Nitabadilisha utaratibu. Niligundua utafiti umefanywa ambao ulipendekeza tutumie njia ya mnada wa wazi. Mfano kitalu cha daraja la kwanza kinaweza kuuzwa hadi Dola 2 milioni za Kimarekani ambazo ni karibu Sh4 bilioni za Tanzania. Lakini sisi tunakiuza kwa Dola 60,000 ambazo ni kama Sh120 milioni,” alisema.

“Si hizo tafiti tu, lakini maelekezo yaliyopo katika Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo (2016-2021) na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) wamependekeza twende kugawa vitalu kwa mnada.”

Alisema kundi jingine lenye masilahi katika utaratibu huu ni wamiliki wa vitalu kwa sababu utaratibu wa zamani unatoa fursa ya wanaohitaji kujadiliana na wagawaji.

“Ukishajuana na wale wanaohusika na ugawaji vitalu unajihakikishia kukipata. Kwa hiyo, nikaamua kufuta ugawaji wa vitalu uliofanyika kwa vile ulikuwa kinyume cha sheria. Vitalu vilitakiwa vigawanywe mwishoni mwa 2017, lakini viligawanywa mwanzo mwa 2017. Mchakato ulikuwa batili na mimi nikaufuta ili tuweke uwanja mpya wa kugawa vitalu kwa mnada,” alisema.

Waziri Kigwangalla alisema tayari ameanza mchakato wa kubadili sheria na kanuni na kama Bunge na Rais wataridhia na kupitisha sheria, atagawa vitalu kwa njia ya mnada.

Waziri huyo alitaja kundi jingine linalonufaika kuwa ni watu wenye mtandao ndani ya Serikali ambao huchukua kitalu kwa dola 60,000 za Kimarekani (sawa na Sh120 milioni) na kukikodisha kwa kati ya dola 200,000 hadi 500,000.

“Ni kama walikuwa wanafanya biashara ya kukodisha na wao wanapata kodi. Niliposema nafuta huo mchakato, kumetokea mtafaruku mkubwa katika sekta ya uwindaji wa kitalii,” alisema.

Alisema wadau hao wameamua kumshambulia, lakini wakienda kwenye mnada watakuwa wametatua jambo moja ambalo limekuwa likiwaangusha mawaziri wengi.

Utoaji vibali vya kuvuna magogo

Dk Kigwangalla alitaja sababu nyingine iliyowaangusha mawaziri waliomtangulia ni ugawaji wa vibali vya kukata magogo, ambayo yanatafutwa duniani.

“Mti ambao ni maarufu sana China na Mashariki ya Mbali ni mkulungu. Ukiwa na mkulungu hapa ukipiga simu Wachina wanapanda ndege saa hiyohiyo kuja kuununua,” alisema.

Alisema mti huo unavunwa kwenye mapori ya Tabora na Katavi kwa kiasi kikubwa.

“Mawaziri wengi wamekuwa wakifanya kazi ya kukata magogo au wakitumia watu wao wa karibu na wakishapata vibali wanaviuza. Wakati mwingine wanawapa marafiki zao vibali,” alisema.

“Hii nchi haina siri. Ni imara sana katika kukusanya taarifa za kiitelijensia. Vyombo vyetu hupata taarifa hizi za deal chafu. Hili ni eneo linawaangusha sana mawaziri.”

Migogoro ya wafugaji na hifadhi

Dk Kigwangalla alitaja eneo jingine kuwa ni migogoro kati ya wafugaji na mamlaka zinazosimamia maeneo yaliyohifadhiwa kisheria.

“Usiposhughulika nayo vizuri ni maeneo ambayo yatakuangusha. Ukumbuke idadi ya watu wetu imeongezeka, lakini eneo haliongezeki. Watu wetu hawafugi kisasa,” alisema.

Alisema kwa miaka ya karibuni kumekuwa na usimamizi mkali wa maeneo yaliyohifadhiwa kwa sababu hilo lisipofanyika nchi itaelekea kuwa jangwa.

“Ukiendesha tu operesheni halali, lazima moto uwake bungeni kwa sababu unagusa masilahi ya wananchi na ambayo ndiyo masilahi ya wabunge na iwe isiwe watakuchukia tu,” alisema.

Hongo kwa mawaziri

Dk Kigwangala alisema ana orodha ya watu waliowekwa mfukoni na mmoja wa wamiliki wa Loliondo.

Alisema amejiridhisha na kuna mtumishi mmoja wa wizara yake ambaye ni kiungo.

“Nimeona (mtu ambaye ni kiungo na mwarabu) atatuvuruga kadri tunavyoendelea,” alisema.

“Anavujisha siri za Serikali na anaweza hata kuhatarisha maisha yetu, maana tunashughulika na majangili na watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha. Ni jambo la hatari sana kwa maisha yetu.

“Ninalipeleka jambo hili Takukuru, wakithibitisha wachuke hatua na wakiona hahusiki basi wamwachie,” alisema Dk Kigwangalla bila kumtaja kwa jina ofisa huyo.

Apongeza watangulizi wake

Hata hivyo, Dk Kigwangalla amewapongeza mawaziri waliomtangulia kwa kazi waliyoifanya katika kupambana na ujangili na majangili.

“Katika maeneo ambayo watangulizi wangu wamefanya kazi kubwa ni suala la ujangili. Idadi ya wanyamapori imeongezeka,” alisema.

“Ninaona katika kazi ambazo sasa nitapambana nazo ni malalamiko ya wabunge, madiwani na wananchi kuhusu wanyamapori kuingia katika maeneo yao kwa sababu wameongezeka,” alisema.

“Kila siku napokea simu za taarifa za mafanikio ya vita ya ujangili lakini siwezi kuziweka wazi kwa sababu ya kiintelijensia. Nina taarifa nyingi za watu wengi wanaojishughulisha na ujangili.”

Mikataba ya hoteli

Akizungumzia mchakato aliouanzisha wa kutwaa hoteli ambazo uendeshaji wake unakiuka mikataba ya uuzaji, Dk Kigwangalla alisema hoteli 10 kati ya 17 zilizobinafsishwa zitatwaliwa na Serikali.

“Mikataba iliyoingiwa (ina maelezo) ya namna ya kuivunja kama mwekezaji hatazingatia matakwa ya mikataba. Tangu zimenunuliwa hadi leo, 10 kati ya 17 hazijakidhi masharti ya mauzo,” alisema.

“Ndiyo nikasema kuna kila sababu ya kuzirudisha ndani ya Serikali ili watafutwe wawekezaji wapya ambao watakidhi masharti ya uendeshaji. Tutawakodishia wawekezaji makini,” alisema na kuongeza kuwa kuna mpango wa kuanzisha hoteli mpya 20 katika maeneo ya hifadhi.
LaTakukuru sijaona tofauti kati ya Hosea na mrithi wake. Bora apeleke kwa JPM atumbue mwenyewe.
 
Huyo kigwa kichwani hana tofauti na le mutuz au bashite yani ni mtupu kiwango cha debe la pumba za mahindi
 
Ni vyema akatueleza zile tuhuma alizompachika balozi kagasheki zimeishia wapi
 
Back
Top Bottom