Kamanda Asiyechoka
JF-Expert Member
- Sep 13, 2020
- 3,166
- 4,581
Amefunguka
👇
====
Alichokisema Hamis Kigwangalla katika majadiliano ClubHouse
Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini, Dkt. Hamis Kigwangalla amezungumza kwenye majadiliano ya Clubhouse na kuelezea msimamo wake kuhusu suala la kuapa kwa kutumia Quran na kashfa za rushwa zinazomkabili.
Akizungumza kwenye majadiliano hayo, Dkt. Kigwangalla alisema kwamba yeye ni Muislamu na anaweza kuapa hadharani kwa kutumia Quran kuthibitisha kwamba hakuchukua fedha za Urithi Festival na wala hakutumia ndege za TANAPA kwa maslahi yake binafsi.
Kuhusu suala la vibali kwa raia wa Tanzania kuingia na kutoka wanavyotaka na haki nyingine kama kumiliki ardhi, Dkt. Kigwangalla alisema kuwa hata kama kuna wasiwasi wa masuala ya usalama, ni vyema vibali hivyo vikutolewe ili kukuza uchumi. Alisema kwamba mambo mengi yanakwama nchini siyo kwa sababu watu hawajasoma, bali ni kutokana na ukosefu wa exposure.
Akizungumzia kashfa ya rushwa inayomkabili, Dkt. Kigwangalla alisema kwamba rushwa ni kitu kibaya sana na kiongozi yeyote anayehongwa huwezi kusimamia haki na kutoa maamuzi sahihi. Aliongeza kuwa yeye sio mtu wa kuchukua rushwa na kama kuna wanasiasa watatu nchini ambao hawachukui rushwa, hawezi kuachwa nyuma.
Kuhusu suala la uwajibishwaji, Dkt. Kigwangalla alisema kwamba uliopo ni mdogo sana na sio wa kiwango kinachotisha watumishi waliopo kwenye ofisi ili wasifanye ubadhirifu. Alisisitiza kwamba kuna haja ya kudai uwajibikaji zaidi.
Akitoa ufafanuzi kuhusu madai kwamba alitumia ndege za TANAPA kwenda kutalii na wanawake, Dkt. Kigwangalla alisema kwamba ni uongo tu na kwamba mara zote alikuwa analipa gharama zote kwa fedha zake mwenyewe.
Mwisho, Dkt. Kigwangalla alisema kwamba yeye sio mtu wa mambo ya kichini chini na anasema mambo hadharani ambayo siyo sawa. Alisema kwamba watu wanaofanya mambo chini chini na kuandika barua kwenda kwa wakubwa wanaonekana kuwa viongozi wazuri, lakini yeye na wengine kama yeye ambao wanasema mambo hadharani ndio wanaonekana kuwa viongozi wabaya.
Jamii Forums