Dk. Idrissa Rashid katika tope jingine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Idrissa Rashid katika tope jingine

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtu66, Nov 21, 2009.

 1. Mtu66

  Mtu66 Senior Member

  #1
  Nov 21, 2009
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Na Aristariko Konga

  MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dk. Idrissa Rashid ametumia Sh. 49,122,800 kununulia maua, samani, sanamu na mapambo mengine ya nyumba.

  Maua hayo, mapambo, sanamu na vitu vingine vya anasa vimewekwa kwenye nyumba hiyo iliyopo kati ya mitaa wa Toure na Chaza Lane, kitalu namba 13, Oysterbay, Dar es Salaam.

  Zabuni ya mapambo ya nyumba hiyo ya TANESCO, ambayo inakaliwa na Dk. Rashid inahusu ununuzi wa maua ya plastiki na mapoti yake, fremu za kuwekea picha ukutani, saa za ukutani, mashine za kufulia nguo, vyombo vyote vya kulia, majokofu na mafriza, meza za urembo wa akina mama wanapojiremba na mazulia.

  Sh. 26,283,000 zimetumika katika zabuni ya kununulia seti ya maua, meza, viti, mazulia, fremu za picha oveni, taa ya umeme ya mezani, saa ya ukutani,mashine ya kuoshea, masofa na friza. Vilinunuliwa kutoka kampuni ya M/s McSOMS Furniture Mart T/A Royal Furnitures, ya Dar es Salaam.

  Kiasi kingine cha Sh. 12,586,800 kilitumika katika zabuni ya kununulia seti nyingine ya maua na mapoti yake, vitanda, meza, viti, mazulia, stuli na makabati. Vilinunuliwa kutoka kampuni ya M/s Haase General Enterprises Ltd, ya Dar es Salaam.

  Sh. 5,850,000 zilitumika katika zabuni ya ununuzi wa masofa kutoka kampuni ya M/s McSOMS Furniture Mart T/A Royal Furnitures, wakati Sh. 3,724,000 zilitumika kununulia friza, na mashine ya kuoshea. Vilinunuliwa kutoka kampuni ya M/s Game ya Dar es Salaam.

  Sh. 680,000 zilitumika katika zabuni ya ununuzi wa mazulia, yakiwamo ya Kichina, kutoka kampuni ya M/s McSOMS Furniture Mart T/A Royal Furnitures, ya Dar es Salaam.

  Zabuni za samani na mapambo zilifanywa bila ya kulinganishwa bei kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni kujitokeza kwa mzabuni mmoja kwa kila bidhaa.

  Kampuni ambazo zilikuwa zimeomba zabuni ya kutoa samani na mapambo hayo ni M/s McSOMS Furniture Mart T/A Royal Furnitures, ya Dar es Salaam, M/s Clock Tower Shopping Centre, Gift Land, Game Ltd na M/s Haase General Enterprises Ltd.

  Kila kampuni ilipendekeza bei za samani na mapambo hayo kama ifuatavyo: McSOMS Furniture Mart T/A Royal Furniture (Sh. 5,585,000), Clock Tower Shopping Centre (Sh. 895,000), Gift Land (Sh. 1,260,000), McSOMS Furniture Mart T/A Royal Furniture (Sh. 13,831,30, Haase General Enterprises Ltd (Sh. 26,283,000), Game Ltd (Sh. 3,724,000) na McSOMS Furniture Mart T/A Royal Furniture (680,000).

  Hata hivyo, timu ya tathmini ya TANESCO, ikiwa na wajumbe wanne, ilisema kuwa makampuni mawili kati ya hayo, hayakuwa na mwitikio mzuri wa kibiashara. Makampuni hayo ni Clock Tower Shopping Centre na Gift Land.

  Kutokana na hali hiyo, timu hiyo iliweza kutembelea makampuni matatu tu ili kukagua bidhaa. Makampuni hayo ni McSOMS Furniture Mart T/A Royal Furnitures, Haase General Enterprises Ltd na Game Ltd.

  Timu ta tathmini ya TANESCO iliwajumuisha Rajabu Mbiro kutoka Kurugenzi ya Raslimali Watu, Gracen H. Ndibalema kutoka kitengo cha Mipango na Miradi, Reward Nyerembe kutoka kitengo cha Mipango na Miradi na Justi Masaua, mhasibu wa miradi mikubwa. Timu hiyo iliteuliwa na mwenyekiti wa bodi ya zabuni ya TANESCO, ambaye jina lake halijatajwa.

  Tayari Dk. Rashid amekarabati nyumba ya shirika anayoishi hivi sasa kwa zaidi ya Sh. 500 milioni, jambo ambalo mbunge wa Sumve, Richard Ndassa, alililalamikia bungeni.

  Uchunguzi wa MwanaHALISI umebaini kuwa Dk. Rashid mkataba wake wa miaka mitatu hauruhusu kukaa kwenye nyumba ya shirika, na kwa hiyo ununuzi wa samani na mapambo hayo ni kwa manufaa binafsi. Mkataba wake ulianza Novemba, 2006 unakwisha mwezi huu.

  Mameneja wa Net Group Solution, ambao nao walikuwa na mkataba kama wa Dk. Rashid hawakukaa kwenye nyumba za shirika hilo.

  Mfanyakazi mmoja mwandamizi kwenye wizara ya nishati na madini anasema hata kama mkataba wa Dk. Rashid ulikuwa unamruhusu kukaa kwenye nyumba ya shirika, basi angekaa kwenye nyumba ambayo miaka yote ya uhai wa TANESCO, imetengwa kwa ajili ya mkurugenzi mtendaji.

  Nyumba iliyokuwa inatumiwa na mkurugenzi mtendaji kabla ya TANESCO kukabidhiwa kwa Net Group Solution ipo kitalu namba 7, Kenyatta Drive, Oysterbay, Dar es Salaam, ambayo inakaliwa na mkurugenzi mmoja wa shirika hilo, ambaye jina lake halikuweza kupatikana.

  Dk. Rashid analipwa Sh. Milioni 11 kwa mwezi na TANESCO.

  Taarifa za ndani ya TANESCO zinasema Agosti mwaka huu, Dk. Rashid alinunua magari ya bei mbaya aina ya Toyota Hilux na kuyatawanya nchi mzima.

  Hali hiyo ni kinyume na agizo la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwamba viongozi wa umma, wakiwamo mawaziri, kuachana na mtindo wa kununua magari ya kifahari.

  Habari zaidi zinasema kuwa Dk. Rashid amenunua gari jipya kwa ajili ya matumizi yake, lenye thamani ya Sh. 180 millioni.

  Dk. Rashid pia anadaiwa kuwa amewanunulia viongozi wengine sita wa juu wa TANESCO (Executive Management Members) magari yanayofanana na lake kwa thamani ya Sh. 160 milioni. Maofisa waliopewa magari mapya tayari walikuwa na magari mengine ambayo bado yalikuwa kwenye hali nzuri.

  Wafanyakazi wa TANESCO wanashangazwa na ununuzi wa magari hayo wakati ofisi za shirika hilo mikoani zina matatizo makubwa ya usafiri, yanayozorotesha huduma kwa wateja.

  Ofisi hizo zinashindwa kukidhi matakwa ya kuwafungia wateja umeme au kushughulikia matatizo ya dharura, kama nguzo zinapoanguka au waya kukatika.

  Mchakato wa kumpata mkurugenzi mtendaji mpya wa TANESCO unaendelea na MwanaHALISI limedokezwa kuwa majina 12 yamepatikana baada ya mchujo kutoka watu 30, ambao waliomba wadhifa huo ulipotangazwa.

  Kamati maalum yenye wajumbe kutoka bodi ya wakurugenzi, wizara ya nishati na madini na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Idara ya Uhandisi) walitarajiwa kukutana juzi na jana (tarehe 9 na 10 Novemba, 2009) ili kufanya usaili wa watu hao 12 na kupata majina matatu ambayo yangepelekwa ngazi za juu ili mmoja ateuliwe kushika nafasi ya Dk. Rashid.

  Habari zinasema kuwa Dk. Rashid ameonyesha nia ya kutokuendelea na wadhifa huo na wala hakuomba kuendelea, na hivi karibuni alituma waraka kwa wafanyakazi kuwashukuru kwa ushirikiano wao miaka mitatu aliyofanya kazi.

  Ingawa baadhi ya watu wanasema Dk. Rashid alifanya kazi nzuri akiwa TANESCO na kuimarisha hali ya shirika kifedha, wengine wanasema shirika liliimarika kutokana na mikataba ya Aggreko na Alstom, ya miaka miwili kukamilika, mkataba wa Dowans kuvunjwa, IPTL kusimamisha uzalishaji umeme na TANESCO kukataa kulipa malipo yake ya “capacity charges,” hivyo shirika likaweza kupeleka fedha sehamu nyingine, licha ya mkopo wa Sh. 280 bilioni, ambao mwaka 2007 TANESCO ilichukua kwenye mabenki kadhaa, yakiwamo Stanbic, CRDB, Exim na National Microfinance (NMB).


  Source: Mwanahalisi


  HIVI TANZANIA TUMELOGWA???????
   
 2. T

  Tongue blister JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2009
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa jipe jibu, Mtu wa jinsi hii nani atamfunga kengele shingoni.Ukifikiria mambo yanavyo kwenda ndani ya hii nchi unaweza kukata tamaa ya maisha kabisa.

  Watanzania tulio wengi tunawafaidisha walio wachache, Wakati mwingine nafikiria pia kwamba hakuna hata haja ya Rais kusafiri na kulipwa pa diem kwa kwenda kuomba misaada au kupokea misaada toka nje ya nchi kwani HAINA FAIDA YOYOTE KWA WATANZANIA WALIO WENGI.Misaada hiyo ni kama wana kwenda kujiombea wao wenyewe.
   
 3. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Hayo ndo maisha bora kwa kila mtanzania.
  Kama maua na samani zimetumia fedha hizo kwa mtu mmoja, je gharama nyingine zitakuwaje?

  Viongozi wanaendelea kusema nchi maskini.
   
 4. m

  mwanamasala JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2009
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Million 11 kwa mwezi?oh my dear!
   
 5. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  MAFISADI NDO WANAOJUA NCHI/KODI ZA WANACHI ZILIWAVYO.

  Nchi hii kwa sasa ni chuua chako mapema
   
 6. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Baada ya kizazi hiki yani mpaka 2025 wakishakufa wote

  Then kije kingine kitakachoishia 3000

  Baada ya hapo kizazi hicho cha tatu kitaweka mambo sawa
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwa nini Jk alimchagua fisadi huyu kushika usukani wa Tanesco hali aliboronga BoT katika sakata la benki ya Meridien Biao iliyofilisika lakini yeye akawa anaitetea tu?

  nadhani JK alikuwa anataka kumpiku Mkapa katika nani mwenye mbinu kubwa ya kuitokomeza zaidi Tanesco -- Net Group Sulotions au dr Rashid?
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Nov 21, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  JK analipa fadhila. Alipokuwa BOT Rashid alitoa msaada kwa JK.
   
 9. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #9
  Nov 21, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Mkuu Jasusi,Namfahamu vizuri Dr.Idris ni kama ilivyo kwa Rostam ni watu ambao hawamuogopi Rais na wala hawaogopi Authority ya Rais...Anaweza kufanya lolote akijua kwamba hakuna atakayefanya chochote.Urais wa Kikwete una Ubia.....Ni bora amalize muda wake na aondoke salama!
   
 10. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #10
  Nov 21, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mkuu, mbona unashangaa mtu wa nafasi kama hiyo kulipwa hizo fedha? Wakati mwingine sio kila kitu tukiweke pamoja na Ufisadi.Kwa uelewa wangu sidhani kama hizo ni fedha nyingi kwa nafsi kama hiyo.
   
 11. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #11
  Nov 21, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  I love this country! I'm happy to be born here. I love my Tanzania. Kule Nigeria waasi wameanza mapambano sasa. Ni vitu kama hivi vinavyokatisha tamaa vinapelekea watu kuasi nchi yao. Lakini in my Tanzania, hata mtu akuchokoe jichoni, wewe unatabasamu tu and life goes on. Go Idrissa!!!
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Nov 21, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  That is a pathetic reality!!!
   
 13. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #13
  Nov 22, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mie sijaona ufisadi wowote katika hii ishu yeyote zaidi ya smear campaign ya Dr Idrissa. Unlike Rada case inayoonyesha harufu ya ufisadi hii ni utendaji na haki ya kila mkurugenzi apewe. Ndio tofauti ya mtu wa kawaida na mkurugenzi wakati wewe ukiwahi kwako nyumbani na kuwahi kulala mkurugenzi huamka saa kumi na mbili ya alfajiri kulala saa tisa usiku hivyo vitu kama hivi ni vya kawaida.

  Tuache majungu na majiwivu yasiyokuwa na maana hapa hamna ufisadi wowote zaidi ya majungu matupu
   
 14. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #14
  Nov 22, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Wengine tulisema alipokorofishana na Tanga Cement kuwa huyu jamaa hafai. Wengi wakamtetea ati yeye ni mzawa anatetea maslahi ya nchi dhidi ya dhulmati wa kizungu! Matokeo ndiyo haya.

  Ni mtu gani anayejua quality anaweka nyumbani kwake maua ya plastiki? Ningependa kujua kwenye hizo zabuni za samani wangelinganishaje bei? Kwani wazabuni walipewa sampuli ya aina ya samani inayohitajika? Kama uamuzi wa aina ya samani uliachwa kwa mzabuni basi basis ya kulinganisha ingetoka wapi, maana kila mmoja angependekeza aina yake tofauti na mwengine!

  Yote haya tunayastahili kutokana na kutanguliza uzalendo feki! Wasemavyo wajanja, na bado!

  Amandla........
   
 15. JohnShaaban

  JohnShaaban JF-Expert Member

  #15
  Nov 22, 2009
  Joined: Aug 23, 2007
  Messages: 465
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mkuu Amani, sometimes tuzingatie 'distribution of wealthy'; Tanesco hapohapo kuna wafanyakazi wanalipwa around 100,000/= kwa mwezi. Of course, reason inaweza kuwa elimu na uzoefu lakini the gap is tooo big!! Anyway, nalitamani 'Azimio la Arusha' la kifikra!
   
Loading...