Simchezo
JF-Expert Member
- Apr 10, 2012
- 463
- 374
Katika gazeti la mwananchi la leo amesikika Dk. Benson Bana akisema ana mpango wa kugombea ubunge jimbo la Bukoba vijijini kwa tiketi ya Chadema.Hii imekaaje wadau?
Chanzo: Gazeti Mwananchi | 14 Novemba,2014
...Kadhalika, Dk Bana alikanusha tuhuma zilizotolewa na Dk Slaa dhidi yake akisema hajawahi kuwa na uhusiano na Twaweza huku akidai kuwa hata yeye mwenyewe anatamani CCM itoke madarakani miaka mitano tu, ili wananchi wapate uongozi tofauti.
"Kwa kweli ningekuwa na simu ya Dk Slaa ningempigia. Chadema na Ukawa wakijipanga wanaweza kuchukua nchi maana wana ushawishi mkubwa kwenye vyombo vya habari na makundi ya jamii.
"Kosa walilolifanya ni kumtimua Zitto Kabwe, ni kama vile Barcelona bila (Lionel) Messi. CCM sasa hivi imechokwa wananchi wanataka kuona uongozi tofauti," alisema Dk Bana.
Alisema kitendo cha Chadema kumhusisha na CCM kitakwamisha mpango wake wa kujiunga na chama hicho ili agombee ubunge katika Jimbo la Bukoba Vijijini... "Ingawa familia yangu haipendi niingie kwenye siasa, bado naendelea kufikiri, lakini kwa mambo haya (Chadema) watanikubali kweli?" alihoji.
Chanzo: Gazeti Mwananchi | 14 Novemba,2014