Wana chadema nimesoma katika gazeti la mwananchi la jana Dr Bana akilalamikia kauli ya Dr slaa kumhusisha na ccm katika matokeo ya utafiti yaliyotangazwa juzi.
Katika kauli aliyoitoa Dr Slaa alisema haya amini matokeo ya utafiti huo Kutokana na kumhusisha Dr Bana na taasisi yake.
Dr slaa aliongeza kuwa kabla matokeo ya utafiti huo kuwekwa hadharani alikuwa ameshapata na kuyasoma na katika utafiti wake alibaini kuwa yalikuwa na mkono wa kigogo mmoja wa serikali.
Dr slaa aliongeza kuwa alipata nakala ya barua pepe iliyotoka kwa kigogo huyo ikiishukuru taasisi hiyo kwa kazi nzuri Waliyofanya na mambo yamekwenda kama walivyo panga.
Katika utetezi wa Dr Bana anamlalamikia Dr Slaa kwa kumhusisha na ccm na kuongeza kuwa hata yeye anatamani Ccm iondoke madarakani japo kwa miaka mitano tu ili watanzania waone tofauti.
Dr Bana anaseme kauli iliyotolewa na Dr Slaa imemfadhaisha sana kwakuwa anampango wa kugombea ubunge kupitia chadema lakini kwa sasa anawasiwasi kama atapokelewa vizuri na wana chadema kutokana na kauli alitoitoa Dr Slaa.