Dk balali aanza kampeni za urais zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk balali aanza kampeni za urais zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Feb 22, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,032
  Likes Received: 6,831
  Trophy Points: 280
  [​IMG] Ammiminia sifa Rais Kikwete
  [​IMG] Ataka awe mgombea pekee  [​IMG]
  Rais Jakaya Kikwete  Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar, Dk. Mohamed Ghalib Bilal, ameanza mbio za kuwania Urais wa Zanzibar kwa kummwagia sifa Rais Jakaya Kikwete kuwa ni kiongozi shupavu na mwenye busara aliyeweza kuchukua hatua dhidi ya kashfa kadhaa zinazoikabili nchi.
  Amesema licha ya kuibuka kwa kashfa nyingi na misukosuko inayohusu ufisadi likiwemo sakata la wizi wa mabilioni ya fedha kutoka Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na mkataba tata wa Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond LLC ya Marekani, Rais Kikwete ameweza kuchukua hatua kwa kutumia busara na kuvuka vikwazo vilivyojitokeza bila kutetereka.
  “Tanzania ina kiongozi shupavu mwenye busara anayeweza kumaliza matatizo yote kwa kutumia busara," alisema na kuongeza:
  "Tunaweza tukakerana lakini tukawekana sawa kwa kuelewana kutokana na viongozi wetu kuwa imara.”
  Dk. Bilal ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza katika sherehe za kuhitimisha kumbukumbu ya miaka 33 ya kuzaliwa kwa CCM ambazo kimkoa zilifanyika wilayani Mkuranga. Sherehe hizo pia zilikwenda sambamba na ufunguzi wa jengo jipya la chama hicho Wilayani Mkuranga.
  Ingawa hakufafanua zaidi, lakini alionekana kumsifia Rais Kikwete kwa kutumia busara katika kujaribu kuyapatanisha makundi hasimu ndani ya CCM, hususan miongoni mwa wabunge yaliyoibuka baada ya kuzuka kwa kashfa ya Richmond.
  Kuibuka kwa uhasama baina ya makundi hayo, moja likiwahusisha watuhumiwa wa ufisadi na lingine likiwahusisha wabunge wanaojipambanua kama wapambanaji dhidi ya ufisadi, kuliilazimisha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kuunda Kamati Maalum ya usuluhishi ikiwajumuisha Rais Mstaafu, Ali Hasan Mwinyi (Mwenyekiti); Spika Mstaafu, Pius Msekwa (Katibu) na Abduralhman Kinana (mjumbe).
  Wiki iliyopita, Rais Kikwete alipendekeza kwa NEC Kamati hiyo iongezewa muda kuendelea kusaka suluhu, baada ya kubainika kuwa suluhu haijapatikana. Wajumbe waliiongezea miezi miwili.
  Aidha, Dk. Bilal ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Pwani, alisema kuwa mgombea wa nafasi ya urais kupitia tiketi ya CCM kwa mwaka 2010 anapaswa kuwa ni Rais Kikwete pekee.
  Dk. Bilal ambaye anatajwa kuwa ni mmoja kati ya wanachama wa CCM wanaotarajiwa kuomba uteuzi wa chama hicho kugombea Urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, alisema kuwa Rais Kikwete anapaswa kuwa mgombea pekee kutokana na ushupavu na busara aliyoonyesha katika uongozi wake.
  Dk. Bilal aliwania nafasi hiyo mwaka 2005 lakini Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM ilimpitisha Rais Amani Abeid Karume, licha ya Dk. Bilal kuwashinda wagombea wote waliojitokeza kuomba uteuzi katika kikao cha Kamati Maalum ya NEC Zanzibar.
  "Nchi yetu ni tulivu kutokana na busara na uongozi uliopo, tuna viongozi imara na kila mmoja ameweka alama ya mfano; Hayati Mwalimu Julius Nyerere ameweka alama ya kuliunganisha taifa. Nchi ina makabila tofauti lakini alituunganisha sote kwa kutumia lugha moja. Tumejenga imani kwake kutokana na kazi yake, hivi sasa kila tunapotembea kila mmoja anatembea kifua mbele," alisema.
  Aliwakumbusha wanachama na viongozi wote wa chama hicho kufanyia kazi maelekezo aliyoyatoa Rais Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM taifa katika maadhimisho ya sherehe ya miaka 33 ya chama hicho, kubwa zaidi likiwa ni mapambano dhidi ya rushwa.
  "Katika kukabidhi wanachama wapya kadi tulielewe hilo, tufahamu nini rushwa, vipi tunajikinga nayo… Ni kazi ambayo itafanywa na wilaya, ienezeni vizuri sana,” alisema.
  Akizungumzia Muungano, Dk. Bilal alisema kuwa inashangaza mara kadhaa kuzungumziwa sana kwa kero za Muungano huo lakini faida zake hazizungumziwi.
  "Tangu Afrika ipate uhuru ni nchi ngapi zenye muungano? Hamna hata moja ila ni Tanzania pekee. Kulikuwa na nchi kadhaa zilizojaribu muungano zikashindwa lakini sisi tumeweza. Kama kuna mtu anaweza kuuvunja muungano atashindwa kufanya hivyo na ndio maana tunaona Waunguja wanacheza ngoma za wabara na wabara nao wanacheza ngoma za visiwani.
  "Tunapendana, tunaheshimiana, uliopo ni utani wa watu tu, heshima inabaki palepale. Tutautunza Muungano milele na milele,” alisema.
  Kuhusu makundi na migongano miongoni mwa wanachama na viongozi wa chama hicho mkoani Pwani, Dk. Bilal aliwataka kukaa pamoja ili kujenga maelewano miongoni mwao kwa kuacha kuhitilafiana na kusahau tofauti zao kabla ya mchakato wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu kuanza.
  "Kamati za siasa za kata, wilaya hadi mkoa zifanye kazi ya kumaliza visa hivyo bila kufichana kwa vile itazidisha magomvi yasiyokwisha. Zifanye kazi hizo, tuwe wazi kwani tukifichana tutaficha ugomvi na vidonda. Tuna wajibu wa kujipanga vizuri kwa kuhakikisha mambo yanakwenda sawa," alisema.
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  Feb 22, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Dr Bilali ama balali mkuu, angalia vyema hiyo Title yako.
   
 3. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Jaribu kuandika tena jina lako maana unaweza kusema kuwa ni Dr Balali masuala ya EPA ee jaribu kuedit tena
   
 4. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #4
  Feb 22, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,754
  Trophy Points: 280
  Mkuu rekebisha hilo jina,nadahani hatuanagalii vizuri headings zetu kabla hataujapost.hili ni kosa la pili kwa leo tu hapa jamvini
   
 5. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #5
  Feb 22, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,754
  Trophy Points: 280
  ok,sasa tunaweza kuendelea,umesharekebisha sasa
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  Feb 22, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  bila shaka Bilali huu ni wakati wake wakuchukua nnchi baada ya kina mkapa kumuwekea mtima nyongo, na kumpa Karume ambae alipitwa kwa kura nyingi, kamati kuu chini ya mkapa ilimkatili sana.
   
 7. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Pamoja na hayo mimi sijaona waziwazi katika habari hii kwamba Dr. Bilali ameanza kampeni. Ni hisia tu. Hata hivyo kama kweli anataka kugombea Urais Zanzibar 2010 sioni wa kumpiga STOP safari hii. Mvumilivu ula mbivu. Zanzibar kuna mafuta jamani.
   
 8. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,873
  Likes Received: 2,640
  Trophy Points: 280
  Byase una vituko sana.
  I like that!
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Feb 22, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 43,137
  Likes Received: 27,112
  Trophy Points: 280
  mambo y muungano yatamkosesha kura. labda wapange matokeo.
   
 10. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,632
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Naungana na maoni yako, kichwa cha thread hii hakiendani kabisa na maelezo yanayohusishwa na hotuba ya Dr. Bilali aliyoitoa huko Mkuranga!! Hakuzungumzia kabisa juu ya Urais wa Zanzibar lakini nadhani muanzisha thread ana lake jambo; hata hivyo nadhani Dr. Bilali will be the right candidate for the Isles. Ni mtazamo wangu TU!!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...