Dk 45 ITV: Kwanini wapinzani hawaalikwi humu?

Kusema kweli huyu Suleiman Semunyu anapwaya sana! Sijui anakkuwa hakujiandaa. Hivi huwa haangalii vipindi vingine kama hivyo mfano HARD TALK. Nilishangaa badala ya yeye kuuliza maswali Wassira ndiye akawa muulizaji maswali. Tena akajigamba kwamba anamfundisha Semunyu.

Mfano mdogo Wassira aliponda kwamba CDM kusema leo 2012 watachukuwa nchi 2015 ni propaganda na CDM ni wapiga ramli because siasa eti zinaongonzwa na matukio, hivyo hata yeye Wassira hajui kama 2015 atashinda.

Mimi nilitegemea Semunyu umuulize hapo hapo kuwa CCM wamewahi kutamba hadharanai kwamba wataongoza nchi kwa miaka 100, tena wengine wakakufuru kwamba wataongoza MILELE. Je, kama wao CCM wana uwezo wa kujua matokeo ya miaka 100 ijayo, Kwanini iwe vigumu kwa CDM kujua matokeo ya miaka 3 tu ijayo. Lakini Semunyu hakuweza hata ku-link hiyo hoja akaichia ikapita tu. Mifano ni mingi inayoonesha Semunyu huwa hajiandai bali anakuja kusikiliza propaganda za hao mawaziri. Semunyu if you can't sustain the heat quit the kitchen. Kipindi hicho inaonyesha ni maji marefu kwako na kimekosa ladha.
 
Shukrani kwako ulieanzisha huu uzi na mods pls msiutoe.mwongoza kipindi hafai au hajui wajibu wake.nilikuwa mpenzi sana wa hiki kipindi nilipoona waalikwa wanarusha madongo kwa upinzani na wapinzani hawapewi muda kuja kuzijibu nikaamua kuachana nacho.kingine ni tabia ya mtangazaji kuachia mgeni wake aendeshe kipindi na yeye kubaki kama anaduwaa vile.Nawashauri itv wawe wabunifu watafute maswali yenye tija na c waalikwa kujisafisha.
 
Mbona hata mh sharif hamad katibu mkuu wa cuf, ameshawahi kushiriki.
 
Ni kweli mkuu sijawahi sikia/ona kiongozi yoyote toka chama cha siasa cha upinzani, hata huyo mtangazaji hana maswali ama hoja zenye mashiko ama ukomavu kulingana na taaluma yake.

Ni kweli hajakomaa. Haiwezekani Mgeni wako kwenye kipindi akuongoze umuulize maswali ya namna gani. Kwa ujumla anadhibitiwa kirahisi na wale anaowahoji.
 
Jana WASSIRA alifika na HOTUBA na mtangazaji hakuwa amejipanga pia hajui kuhoji, mfano aliuliza matusi wakati wa uchaguzi Arumeru majibu hayatoka na hakuweza kukumbusha swali lake la msingi.
Huyu mtangazaji hana uwezo ndugu zangu, mnaoweza kuwaona wakuu pale ITV watafute/wakodishe mtangazaji mahiri kama TIDO MHANDO.
 
Hao watangazaji wa ITV hawawezi kubadilika. Wamekaa kinafiki sana sasa wanajua wanaweza kuteuliwa kuwa wakuu wa wilaya. Sasa uanze kumbana waziri kwa maswali, au uanzishe urafiki na wapinzani si ndio unasahau ukuu wa wilaya?
 
Hicho kipindi ni cha kipuuzi kabisa, dunia ya sasa unaweka kipindi recorded? maana utakuta juma pili anaanza kurusha dondo kwa yaliyongelewa. maana yake watakuwa waneongea Alhamis au ijumaa, wakafanya editing kwa siku 2-3 ndio wanarusha jumatatu! sasa hapo unasikiliza nini hapo?

Hivi mkuu unafikiri kuna waziri wa magamba atakayekubali maswali ya papo kwa papo?Kwa taarifa yenu huyo mtanagazaji
wakimbadilisha na kuweka mzoefu mawaziri wote wataingia mitini.
 
Mbona hata mh sharif hamad katibu mkuu wa cuf, ameshawahi kushiriki.

Wewe kweli una degedege kama jina lako. Hivi hujui Maalim Seif Sharif Hamad ni Makamu wa Kwanza wa SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR. The operating word here is SERIKALI. Get real dude.
 
Back
Top Bottom