Dk 45 ITV: Kwanini wapinzani hawaalikwi humu?

Sisi CHADEMA tuko busy na wananchi na si kipindi cha magamba kutushambulia. Mtangazaji jana alionesha upendeleo kwa kumrudia mara nyingi waziri wa misitu.
 
Ni kweli mkuu sijawahi sikia/ona kiongozi yoyote toka chama cha siasa cha upinzani, hata huyo mtangazaji hana maswali ama hoja zenye mashiko ama ukomavu kulingana na taaluma yake.
 
Nashukuru kwa kuanzisha uzi huu, kipindi ni kizuri lakini ukweli narudia ukweli kuwa mtangazaji anapwaya sana, wanaoalikwa wanaongoza mazungumzo nayeye anafuata nyuma, ni mara kadhaa hana uhakika na hoja zake na hivyo waalikwa baada ya kuulizwa swali, wanaligeuza wanavyotaka wao na yeye haoneshi kuwa ni mtangazaji aliyeiva kushikiria swali lake na maudhui ya swali lake, ANAPWAYA SANA MTANGAZAJI HUYU, ITV kama ina watangazaji walioelimika basi wapewe kipindi hicho.

Wassira jana kapindisha maswali kibao harafu mtangazaji hajui la kufanya, anapunguza wasikilizaji wa kipindi badala ya kuwaongeza, swali kuhusu kuzomewa, swali kuhusu ccm kuwa makundi makundi na kushindwa 2015 mfano wake ulikuwa hoja za maige, yeye akajibu mfano wa swali (eti siwezi kumzungumzia maige) sio swali lenyewe, MTANGAZAJI alikuwa wapi???; Makundi anajibu hata vyama vingine yapo, sasa kweli hilo ndo jibu la hilo swali??? mtangazaji uwezo kiakili am very sorry unapwaya.

Mimechukua mifano michache tu lakini kila nikisikiliza kipindi hicho mtangazaji anapwaya sana, aidha hana uwezo kielimu au kiasilia hawezi vipindi vya aina hiyo; apishe vijana wenye uwezo au abadilike sana, ajue agenda yake kwenye swali ni nini na asimamie maswali yajibiwe, ni afadhali swali likose jibu kuliko blabla tu.

Kipindi ni cha maswali yenye utata/magumu sio maswali ambayo kila mtu analojibu haitakuwa na maana kabisa; aandae maswali vigongo yenye manufaa kwa TZ, aombe yajibiwe, asimamie swali lijibiwe sio mtu atunge lake harafu aanze kujibu.
 
Ahsante kwa kuweka thread hii jamvini, mimi nimewahi ku-comment mara kadhaa juu ya uboreshaji wa kipindi hiki. Kama ni viongozi wawe wale wote wanaowajibika kwa wananchi, si wale tu walio serikalini! Kama ITV ingelikuwa ni ya serikali, hapo sawa.

Kama ni viongozi wa kisiasa, si hao tu walio serikalini. Lakini pia wangeshirikisa hata viongozi wa dini (wazungumzie mambo kitaifa na ya jumla tu), viongozi wa mashirika ya umma na yasiyo ya umma, n.k.

Wakati mwingine huwa naingiwa na mashaka na huyu Seleman Semunyu, kwamba huenda ana ajenda fulani nao, kwa mfano hata kama kipindi hicho kilibuniwa kwa ajili ya mawaziri tu, ni kigezo gani anachotumia kumwalika waziri fulani hata mara 4, wakati kuna ambaye hayawahi kualikwa hata mara moja?!

Na ukifuatilia hao wanaoitwa mara kwa mara, kila inapotokea huwa wamekuja (sijui niite kuoshwa) mara yakuwepo uvumi wa kuchafuliwa na matukio kadhaa, lakini kingine kinatia mashaka, ni pale anapokuja mtu fulani, anaulizwa swali wakati wa kujibu, anaonekana dhahiri akisoma majibu yaliyoandaliwa kwenye "note book" na majibu yake huyasoma kwa mtiririko wa namna alivyoandaa, yaani ukurasa mmoja baada ya mwingine, je hii haijengi mashaka kuwa huwa kunakuwepo mawasiliano kati ya hao wawili? Ni mtizamo wangu, I might be wrong!
 
ni lazima watu itv kama ilivyo haifungamani na chama chochote cha siasa. Ni chombo cha raia wote sasa ukisema chama fulani kiende kufanya interview kuna wengne hawataridhika
 
ITV wanatakiwa watafute mtu anayeweza kuhoji vizuri, yule mtangazaji wa sasa anabaki anashangaa haeleweli hata kitu, ndo mana Mkapa huwa hataki kuongea nao mana wako shallow mno
 
Nashukuru kwa kuanzisha uzi huu, kipindi ni kizuri lakini ukweli narudi ukweli kuwa mtangazaji anapwaya sana, wanaoalikwa wanaongoza mazungumzo nayeye anafuata nyuma, ni mara kadhaa hana uhakika na hoja zake na hivyo waalikwa baada ya kuulizwa swali, wanaligeuza wanavyotaka wao na yeye haoneshi kuwa ni mtangazaji akiyeiva kushirikia swali lake na maudhui ya swali lake, ANAPWAYA SANA MTANGAZAJI HUYU, ITV kama ina watangazaji walioelimika basi wapewe kipindi hicho.

Wassira jana kapindisha maswali kibao harafu mtangazaji hajui la kufanya, anapunguza wasikilizaji wa kipindi badala ya kuwaongeza, swali kuhusu kuzomewa, swali kuhusu ccm kuwa makundi makundi na kushindwa 2015 mfano wake ulikuwa hoja za maige, yeye akajibu mfano wa swali sio swali, MTANGAZAJI alikuwa wapi???; Makundi anajibu hata vyama vingine yapo, sasa kweli hilo ndo jibu la hilo swali??? mtangazaji uwezo kiakili am very sorry umapwaya.

Mimechukua mifano michache tu lakini kila nikisikiliza kipindi hicho mtangazaji anapwaya sana, aidha hana uwezo kielimu au kiasilia hawezi vipindi vya aina hiyo; apishe vijana wenye uwezo au abadilike sana, ajue agenda yake kwenye swali ni nini na asimamie maswali yajibiwe, ni afadhali swali likose jibu kuliko blabla tu.

Kipindi ni cha maswali yenye utata/magumu sio maswali ambayo kila mtu analojibu haitakuwa na maana kabisa; aandae maswali vigongo yenye manufaa kwa TZ, aombe yajibiwe, asimamie swali lijibiwe sio mtu atunge lake harafu aanze kujibu.

Kwa hakika nashukuru sana ulinitangulia kuanzisha uzi huu leo.Nilipanga kuandika juu ya kipindi kwa kadiri nilivyokitazama jana. Ki ukweli mimi si mtazamaji wa kipindi hicho toka kiwe hewani nasikia tu fulani kaongea hiki. Na nilisoma maoni ya Karugendo gazetini siku moja akikosoa kipindi hiki.Jana wakati natafuta vipindi vya kutazama nikamwona wasira na semunyu wakiwa wanaanza tu mazungumzo yao.Nikashawishika kutazama nimsike wasira anaongea nini. Mapungufu(japo si kiswahili sanifu) niliyoyaona ni kama yafuatayo;
1. Mtangazaji hajiandai kumhoji mhusika.Kwanini?Sikuliona swali la kiujuzi alilioulizwa Wasira. Hata maswali aliyoulizwa wasira mengine alikuwa hajibu au kupindisha swali alilioulizwa na mtangazaji anamwacha tu.Hang'ang'anii swali lake lipewe jibu.Mfano swali kuhusu siasa za vyama vingi, mahusiano yakoje hivi sasa reference Semunyu akitoa ile ya Arumeru.Hili Wasira hakujibu akarukia kwingine na kusema ya Arumeru achana nayo.
2. Semunyu ana woga wa kuuliza swali la kuudhi.Mtangazaji siku zote hasa katika vipindi kama vile vya mahajiano anatakiwa aondoe woga wa kuuliza swali la kumkasirisha au kumuudhi anayemhoji.Chukua mfano wa makundi ndani ya CCM.Wasira swali hili badala ya kuuliza akarukia kumhoji mtangazaji, chama kipi hakina makundi nitajie.Akaanza, CUF wanamakundi, Chadema wana makundi.Hapa Wasira alikazania sana.Chadema kina kundi la Mbowe, Slaa na Zitto, wewe hujui hili.Hapa nikaona kuna upungufu kwa mwandishi.Hakutaka kumdadisi hayo makundi ni yepi wala kumlazimisha kujibu hoja aliyoulizwa ndani ya ccm.
3. Kwa jana, niliona, Wasira alikuwa naonekana ni mwenye dukuduku na kisilani hasa na chadema, kwani maswali mengi aliyohojiwa alikuwa anakimbilia aidha kukitaja chadema au kukilaumu au kukikebehi chadema.Chukua mfano wa swala la kuvuana magamba ndani ya ccm.Badala ya kujibu swali kama alivyotakiwa akarukia kusema chadema wana endesha change sijui change ya nini?anahoji.Change ya kurudi nyuma au kwenda mbele maana zote ni change.
Hapa kiufupi Wasira nilivyomsoma ni kuwa hafurahishwi na kampeni ya chadema bali ana hasira nayo.
4. Semunyu anapaswa kuwabadilisha au kuwaleta watu wawili awe anawahoji.Mfano kama jana alitakiwa kwa vile kamleta waziri wa mahusiano, alipaswa pia amlete mtu mmoja toka kwenye vyama vya siasa aweze kusema kama mahusiano ya vyama vya siasa ni mazuri au la.Au ushauri mwingine ni kuwa aite na vyama vya siasa badala ya kuwaleta mawaziri ambao wanaongea kusifia serikali zaidi.Mfano aliyoongea wasira yanapaswa kujibiwa pia na wengine hasa wale aliowagusa.
Hayo ni baadhi tu niliyoyaona.
 
Ingekuwa vizuri Mtangazajia aandae maswali, halafu asimamie majibu, kama akiona Muhusika anayeenda nje ya mada amrekebisha na kumrudisha kwenye mada. Mara nyingi Mtangazaji anamwachia Mhusika kujieleza anavyotaka mpaka mtangazaji anashtuka muda umeisha !!! Hata hivyo, inavyoonekana na ndivyo ilivyo yale maswali sio ya papo kwa hapo kwa sababu Mhusika anasoma kutoka kwenye taarifa iliyoandaliwa na ikiwa ni pamoja na takwimu mbali mbali. Hii inatia shaka kama mtu anayehojiwa ana uelewa na jambo analojibu kwa sababu anasoma majibu ambayo tayari yameendaliwa. Kama hiyo ndiyo kazi yake, kwa nini asiongee bila kusoma ? Kipindi kiwe Live na kuruhusu maswali kutoka kwa watazamaji.
 
Hicho kipindi ni cha kipuuzi kabisa, dunia ya sasa unaweka kipindi recorded? maana utakuta juma pili anaanza kurusha dondo kwa yaliyongelewa. maana yake watakuwa waneongea Alhamis au ijumaa, wakafanya editing kwa siku 2-3 ndio wanarusha jumatatu! sasa hapo unasikiliza nini hapo?
 
Kimsingi jamaa anaboa, hadhi ya kipindi ilitakiewa kufanana na hard talk ya BBC lakini semunyu amebaki kuwa msikilizaji tu hadi huwa natamani kuzima tv, afadhili angepewa hata fatma nyangasa au mzee masako huenda kingechangamka
 
Kwanini wapinzani hawaalikwi katika kipindi hiki, tumechoka na longolongo za hao wanaokuwepo humo, wanaongea visivyoeleweka, wanadanganya na kukataa ukweli tu, uongozi ITV tendeni haki kama kweli mna nia njema na watanzania


Huilo nalo ni neno.
 
Hicho kipindi ni cha kipuuzi kabisa, dunia ya sasa unaweka kipindi recorded? maana utakuta juma pili anaanza kurusha dondo kwa yaliyongelewa. maana yake watakuwa waneongea Alhamis au ijumaa, wakafanya editing kwa siku 2-3 ndio wanarusha jumatatu! sasa hapo unasikiliza nini hapo?


Enheeee, ndio upuuzi huohuo twataka wapinzani wauonyeshe na kuupinga. Ni vizuri kuwapo na wapuuzi kwenye jamii, maana hao watatusaidia kupata kitu cha upuuzi tutakachokizungumzia na hatimaye kuondoa upuuzi katika jamii.
 
Back
Top Bottom