Kichuchunge
JF-Expert Member
- Dec 2, 2020
- 338
- 891
Aliyekua beki wa klabu ya Yanga raia wa kimataifa wa Congo Djuma Shabani ametimkia klabu ya Azam ya jijini Dar-Es-Salaam kwa mujibu wa taarifa mbalimbali.
Beki Djuma Shabani ameonekana kwenye viunga vya Azam akiwa anafanya mazoezi na klabu hiyo, huku vyanzo mbalimbali vikithibitisha beki huyo amejiunga na waoka mikate hao.
Beki huyo aliingia kwenye mgogoro kidogo na klabu yake ya zamani ya Yanga baada ya kuomba kuondoka klabuni hapo, huku klabu yake ikelezwa kumcheleweshea barua ya kumuachia aondoke ndani ya timu hiyo.
Wiki kadhaa nyuma klabu ya Yanga ilifanikiwa kutoa barua ya kumruhusu mchezaji huyo kuondoka klabuni hapo kama ambavyo aliomba, Baada ya mchezaji huyo kuondoka Yanga inaelezwa matajiri wa Dar-es-salaam wamepita nae na kumsajili.