Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Djigui Diara ni Golikipa Mzuri sana na bora pengine kuliko kipa yoyote wa kutoka nje kuwahi kuja kucheza hapa Tanzania, lakini pia ndiye kipa kutoka nje amekuwa na nidhamu mbovu kuliko ila amekuwa anaruka sana vikwazo.
Mechi na Simba alimfuata mwamuzi kama hivyo kwenye video ya pili, akalambwa kadi ya njano, leo mwamuzi amekuwa wa ajabu anamtishia kwa kadi ambayo hakutoa, uamuzi wa ajabu na kizamani kuliko kawaida.
Katika namna ya kushangaza kabisa alichurupuka kwenye kibano cha Kamati ya masaa 72 baada ya kuonekana akimpiga kiwiko mchezaji wa Mtibwa pale KMC Complex kwenye mchezo wa raundi ya kwanza, leo amemvamia mwamuzi wa kati na Kanuni ya 41:5(5.3) itamfyeka kwa vyovyote.
Nimeangalia goli alilofungisha Diara na kujaribu kujificha kwenye faulo, sioni faulo hiyo alokuwa anaitafuta, mpirani kila ukiguswa ni faulo? Diara akubali makosa maisha yaende arekebishe na tabia zake yeye ni mchezaji wa kawaida kama wengine.
BİN KAZUMARI MTIPA.