dj fetty kutinga big bro stargame.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

dj fetty kutinga big bro stargame..

Discussion in 'Celebrities Forum' started by ney kush, Jun 7, 2012.

 1. ney kush

  ney kush JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 1,195
  Likes Received: 377
  Trophy Points: 180
  Dj wa kwanza wa kike nchini Tanzania Fatma Hassan aka Dj Fetty wa Clouds Fm amepewa heshima ya kuwa Dj wa kwanza wa kike kutoka Afrika Mashariki kutumbuiza kwenye mashindano ya Big Brother Africa. Kupitia ukurasa wake wa Facebook Fetty amesema, "Juma mosi hii na jumapili nitakua nikispin ndani ya Jumba la BBA STARGAME, nitume kwa kuniandikia playlist itakayo wapagawisha…na shinda very nice cape ya big brother na high quality Tshirt kutoka CloudsFm…legoooooo."

  Fetty ambaye kwa muda alikuwa amepumzika shughuli za udj na kuendelea na utangazaji wa kawaida, amesema imemlazimu kujifua tena ili kuhakikisha kuwa ‘haangushi maembe' (kumix vibaya nyimbo) wakati atakapokuwa akipiga ngoma. Amesema mwaliko huo ameupata katikati ya mwezi May na tangu hapo amekuwa akijikumbushia ujuzi kwenye ‘wheels of steel' kwakuwa hiyo ni nafasi kubwa inayohitaji maandalizi ya kutosha. Mwaka jana Dj wa kike kutoka kituo cha radio cha YFM cha Ghana Nana Kessewa Adu aka DJ Kess alialikwa pia kuburudisha kwenye Big Brother mplified.

  Hiyo si mara ya kwanza kwa Dj wa Clouds FM kupata mwaliko huo. Mwaka jana Dj Steve B naye alipewa fursa hiyo ya kuonesha ujuzi wa mikono yake kwenye 1 and 2!

  source bongo5
  VIA IPHONE 4s
   
 2. Mkare_wenu

  Mkare_wenu JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  thats good of her,ila huwa sielewi vgezo wanaangalia nin?
   
 3. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  Hongera kwake,lakini fanya marekebisho kidogo bana hii ni JF. Fetty(sipendi kumuita DJ) si DJ wa KWANZA wa kike Tanzania! DJ wa kike namfahamu DJ mmoja wa kike pale Club billicanas miaka ya tisini kama sikosei bahati mbaya jina lake silikumbuki ndie ninaemkumbuka na pengine yupo mwingine nyuma yao.Aliyekuwa DJ maarufu sana wa kike Tanzania na wengi wanamfahamu ni Rehema Chalamila a.k.a Ray C. huyu upigaji wake pale E.A radio ulifanya mimi binafsi kumshawishi aanze kujiita DJ.Ray C ame host vipindi yeye mwenyewe akiwa DJ na pia amepiga sana tu pale bilicanas.
   
Loading...