Dj Fetty atangaza rasmi kuacha kazi ya Utangazaji

Tua Ngoma

JF-Expert Member
Apr 14, 2015
3,102
8,006
Dj fetty ametangaza kuachana na utangazaji na kuwa Mjasiriamali kuanzia leo

==================

fatuma.jpg

SURPRISE!
Aliyekuwa mmoja wa watangazaji wa kipindi maarufu cha burudani XXL cha Clouds FM, Fatma Hassan ‘Dj Fetty' leo Sept.15,2015 amewaaga rasmi wasikilizaji na wafanyakazi wenzake kwa madai ya kuachana na kazi ya utangazaji ili kuendeleza biashara zake mpya (Duka la Nguo la Fettylicious lililopo Dar free market).

Siku kadhaa zilizopita, Mwanachama mmoja wa JamiiForums katika jukwaa la Celebrities alihoji kuhusu ukimya wa Dj Fetty kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, hakika leo majibu yake yamepatikana!

Fetty amesikika kwenye kipindi hicho leo kwa mara ya mwisho kama sehemu ya kusema kwaheri.

Mtangazaji mwenza, Adam Mchomvu alipojaribu kuchombeza kwa kumhoji Dj fetty ni sababu ipi iliyomfanya aamue kuacha kazi yake ya muda mrefu kwa ajili ya biashara ya duka la nguo lililoanza juzi tu, huku akitolea mfano wa duka la Born 2 Shine lililoanza muda mrefu lakini mmiliki wake (B12) hakufikia uamuzi wa kuacha kazi, Fetty akajibu kwa ufupi tu kuwa 'majukumu hayafanani' na kila mtu ana namna anavyoshughulikia majukumu yake.

Katika hatua nyingine, kwa masikitiko makubwa mtangazaji huyo mahiri na mwenye mvuto wa kipekee katika utangazaji wa kizazi kipya alionekana mwenye majonzi na alishindwa kujizuia kutoa machozi na kufikia hatua ya kuvaa miwani ili kuficha taswira ya huzuni aliyonayo!


Pia, kuonyesha ni namna gani ameguswa na kuondoka kwa Dj Fetty, B-Dozen amekaririwa akisema,"Nakupenda sana fettythebest na siku ukitaka kuja kwenye #Xxl we niambie utakuja tu mana bado tunakuhitaji".

Kipindi cha XXL ambacho huongozwa na B Dozen akishirikiana na Adam Mchomvu sasa kimepata member mpya, Kennedy The Remedy aliyechukua nafasi ya Fetty akitokea East Africa Radio (The Cruise).

Kennedy The Remmedy ameungana rasmi na familia ya XXL.
 
Leo kwenye kipindi cha XXL cha clouds fm dj Fett ametangaza rasmi kupumzika kutangaza na kuendelea na biashara zake ambazo amezianza na kumaliza uzushi kuwa kafukuzwa kazi. Pia amesema kuwa atarudi tena kama ikiwezekana kuja kutangaza. Wishin u all da best
 

Attachments

  • dj.jpg
    dj.jpg
    12.9 KB · Views: 4,258
Hakika litakuwa ni Pengo kubwa mno ambalo Halitazibika Hapo Clouds FM kwani huyu dada yangu msela alikuwa ni mahiri mno na aliiinua sana Clouds FM.

Anahamia kati ya Uhai FM Radio ya tajiri Bakhresa au Radio mpya ambayo inatarajiwa kuanzishwa muda wowote na kijana Mjasiriamali na mchapakazi Millard Ayo.

Kila kheri dada yangu / yetu Dj Fety.
 
Imeingia Kama Vile INAVYOKUINGIAGA!

Ndugu kuna siku hata moja nilishawahi kukutusi, kukukashifu au hata kujibishana nawe humu jamvini? Ninaweza kukujibisha kwa lugha mbaya maana matusi nayafahamu pia ila kwasababu sio ustaarabu wangu, nakupuuza tu maana umejionyesha kuwa wewe ni mpuuzi.
 
Back
Top Bottom