Diwani wa Kata Ya Mondo Kondoa Dodoma asema ALOMTEKA DR. ULIMBOKA NI SHUJAA

Mjadala umepamba moto, matusi yanatawala, hoja hazijibiwi kwa hoja, ni vigumu kuelewa ni nani ambaye ni mjinga na ni nani muelevu.

Mnapojadili hii hoja jaribuni kuiangalia shilingi pande zote mbili

  1. Ikiwa baba yako na wagonjwa wengine wengi wamealazwa na wanahitaji operation muhimu siku Dr Ulimboka kaitisha mgomo wa madaktai. Na kwa bahati mbaya wakafariki kwa sababu Dr ambaye angewafanyia hizo operation naye aligoma kwa kuitika wito wa Dr Ulimboka
  2. Ikiwa Dr ulimboka ni kaka yako na yupo katika hali hiyo mpaka sasa.
Hapo ndio wanaJF mnaweza kuzungumza lugha moja.
 
Mjadala umepamba moto, matusi yanatawala, hoja hazijibiwi kwa hoja, ni vigumu kuelewa ni nani ambaye ni mjinga na ni nani muelevu.

Mnapojadili hii hoja jaribuni kuiangalia shilingi pande zote mbili

  1. Ikiwa baba yako na wagonjwa wengine wengi wamealazwa na wanahitaji operation muhimu siku Dr Ulimboka kaitisha mgomo wa madaktai. Na kwa bahati mbaya wakafariki kwa sababu Dr ambaye angewafanyia hizo operation naye aligoma kwa kuitika wito wa Dr Ulimboka
  2. Ikiwa Dr ulimboka ni kaka yako na yupo katika hali hiyo mpaka sasa.
Hapo ndio wanaJF mnaweza kuzungumza lugha moja.
mwerevu ni wewe unayeleta hoja za kitoto hapa
 
Kiongozi hakuna maelezo zaidi ya hapo.
picha yake uliyoipost pamoja na rangi zilizomzunguka vinaeleza mengi kuliko ambayo ningeweza kueleza mie.
kazungukwa na polluted yellow and green collours in political context of multipartism.

msamehe bure
 
attachment.php
ee mungu msaidie huyu mrangi kwa maneno anayoyaongea,wana jf naomba profile ya huyu jamaa yawezekana ametoka mirembo karibuni kwani ni dodoma hukohuko.
 
Haya bana,c 2najua chama chake ndo kilifanikisha hayo,kwahyo sitashangaa akisema hvyo.akili yake inamtosha mwenyewe
 
Hoja ipo wazi kabisa huyo bwana ni shujaa
kamaliza mgogoro na kuokpoa mamia ya masikini wasife

kweli wewe ni aina ya viongozi ambao ni janga kubwa la taifa letu pia type yako ya viongozi ndio mmelifanya taifa hili lifike hapa lilipo fika now na bado mnataka kuendelea kung'ang'ania madalaka. Mim ni nayangu machache ambayo ningeomba unijibu wewe una elim gani?? Kiwango gani na maanisha, je kwa fikra zako na akili yako ya ki ccm ccm unafikili walichokuwa au wanachokidai au madai ya madaktari ni sahihi au siyo sahihi. Je utolewaji wa huduma za afya hapa nchini unazionaje?? Je kitendo alichofanyiwa dr ulimboka ni sahihi tena kimefanywa na vyombo vya usalama. Hivi hicho kibuli,kejeri na zarau mnazipata wapi nyie vionhgozi wa ccm au ndio mmelewa madaraka?? Kama ni njaa na uloho wa madaraka ndio vinawafanya hivyo basi kaaeni mkijua ya kuwa day zenu zinzheabika.
 
Akili zenu zinawaruhusu kuhalalisha,
utekaji wa watu nchini Tanzania?
mimi nilidhani ni akina Kova na Jack tu?
kumbe kuna watu hatari kuliko,
maharamia tulio nao kwenye system!!!

Uwezo wenu wa kufikiri umegusa ceiling,
kumteka mtu hata kama ni muuaji,
ni kosa la jinai chini ya katiba ya JMT,
Utawala wa sheria ni lazima utekelezwe,
hata kama hatua zake ni ndefu na ngumu.

Kuna abilioni ya fedha yameliwa na,
Waziri wa afya katibu kuu na wakurugenzi wake,
na kusababisha ukosefu wa vifaa muhmu vya Tiba,
jambo liletalo vifo visivyo vya lazima,
sioni mtu akiomba shujaa ajitokeze,
kuwateka waziri na katibu wake,
au wakurugenzi ili awe shujaa wake.

Kuna siku mtu ataingia na bunduki,
na kuteka jopo zima la madiwani,
wezi wa fedha za halmashauri,
na kudai fedha au la anawamaliza wote,
mtu huyu atakuwa shujaa wa wananchi?

Kuna siku mtu atamteka waziri mwizi,
na kuleta madai yake au hata kumwua,
sijui mtu huyu atakuwa shujaa wa wananchi?

Serikali au makundi ya kiharamia,
yatateka watu wangapi ili kulazimisha,
wananchi kufuata maagizo yake?

Sehemu gani ya hatua ya mtekaji,
unaiona ni kigezo cha kumwita shujaa?
Kumteka na kumpiga?
Kumng'oa kucha na meno?
Kumbana kende kwa kolea,
kumtupa mabwepande baada ya kudhani kafa?




Comrade Sambala ‎....KAMA WEWE NDIO MASIKINI MWENZANGU AMBAYE...

BABA YAKO,
MAMA YAKO,
KAKA YAKO,
DADA YAKO,
SHANGAZI YAKO,
MJOMBA WAKO,
AMA MWANAO

ALIKUFA KWA SABABU TU MADAKTARI WALIGOMA MPAKA KWANZA WALIPWE MILIONI 7.

BASI UTAKUWA NA MIMI KUAMINI KUWA ALIYEMTEKA DK ULIMBOKA NDIO SHUJAA KWANI KAKOMESHA MGOMO
 
huyu ni yule aliesemwa na kova kuwa kaenda kuungama kwa gwajima



WANGU WA KARNE"

Kauli ya Diwani wa Kata ya Mondo-Kondoa,Dodoma(CCM) Namnukuu..........
"SIKU YA MASHUJAA NA SHUJAA WANGU WA KARNE...

Jana ilikuwa Siku ya Mashujaa Tanzania. Siku ambayo huazimishwa kila mwaka kuwakumbuka mashujaa wetu ambao wametoa mchango mkubwa wa kuikomboa Nchi.

Kwa upande wangu Shujaa wangu wa Mwaka na karne hii. AMBAYE NTAMKUMBUKA NI YULE ALIYEFANIKISHA NA KUMTEKA DKT ULMBOKA.

Aliyemteka Dkt Ulimboka ameleta Ukombozi mkubwa kwa watanzania masikini na hasa wagonjwa ambao walikuwa wakifa kwa sababu za mgomo wa Madktari Kudai Mishahara Zaidi.

Kwangu mimi Dkt Ulimboka ni Msaliti wa Taifa lake. Na aliongoza mgomo haramu ulioua watanzania wasio na hatia kwa Tamaa zake.
Tangu Shujaa huyo alipomteka Ulimboka afanikishe Azma yake alikomesha mgomo na Mijadala yote ya madaktari na mpaka sasa Haisikiki tena


HONGERA SHUJAA WETU WA MWAKA KWA KUKOMESHA MGOMO."

Mwisho Wa kunukuu.................

NAOMBA MNISAIDIE NYIE MMEMWELEWAJE NA HII KAULI YAKE?[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom