Diwani Vs Spika wa Bunge nani atashinda? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani Vs Spika wa Bunge nani atashinda?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tankthinker, May 18, 2011.

 1. Tankthinker

  Tankthinker Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: May 1, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Diwani Vs Spika wa Bunge nani atashinda?

  DIWANI wa Kata ya Kijitonyama, Ulole Juma Athuman, amemtaka Spika wa Bunge, Anne Makinda kuifungua barabara inayounganisha eneo la Sinza na Kijitonyama akitishia kwamba, asipofanya hivyo ataitisha mkutano wa hadhara wa wananchi utakaoamua kuwapo au kutokuwapo kwa njia hiyo.
  Akizungumza Dar es Salaam jana, diwani huyo alisema katika suala hilo hakuna mjadala na kwamba kama unahitajika utafanyika baada ya barabara hiyo kufunguliwa na wananchi kuitumia kama ilivyokuwa awali.

  Ulole alisema kuwa kitendo cha Spika Makinda kufunga barabara hiyo, ni ukiukwaji wa sheria na mamlaka zilizopo kwani hatua hiyo ilipaswa kufuata taratibu za vikao husika, kabla ya uamuzi kufikiwa na kwamba kitendo hicho hakikupaswa kufanywa na mtu wa ngazi ya Makinda.
  “Sisi viongozi tunategemewa na wananchi kuwa mfano na pia ndiyo kioo cha jamii tunayoiongoza, sasa katika hali kama hii iliyojitokeza wananchi watakuwa wanajifunza nini?” alihoji diwani huyo na kudai:
  "Alichofanya Spika Makinda kina nia ya kuongeza ukubwa wa eneo la kiwanja chake na si vinginevyo."
  Alisema kwamba Spika Makinda alitakiwa kuwasilisha suala hilo katika ngazi ya mtaa na ama lingepitishwa katika hatua hiyo, lingepelekwa katika ngazi ya kata na kamati ya maendeleo ya kata pia ingelipitia na kutoa uamuzi kulingana na mapendekezo ya wananchi.
  Katika sakata hilo, jana Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana aliwaita ofisini kwake, Kaimu Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kijitonyama na Ofisa Mtendaji wa Mtaa na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mpakani ‘B’, Balbo Kalinga kujadili suala hilo.
  Hata hivyo, inadaiwa kuwa watendaji walioitwa na Rugumbana siyo wa mtaa ilipo barabara inayolalamikiwa kufungwa.Rugimbana alipoulizwa kuhusu suala hilo alikana kuwa na kikao na watendaji hao lakini akasema alichofanya ni kuwaita ili kusikia kutoka kwao kuhusiana na sakata hilo la kufungwa kwa barabara na kwamba hakikuwa kikao rasmi.
  “Sikuitisha kikao, nimewaita kama Mkuu wa Wilaya ili kujua kitu kinachoendelea katika eneo hilo na niliowaita ndiyo ambao nimewahitaji,” alisema Rugimbana
  Diwani Ulole alisema Mkuu wa Wilaya amelichukulia suala hilo kisiasa akisema licha ya kutokuwa wa eneo lenye mgogoro, aliowaita ni wanaCCM na kumwacha yeye ambaye anatoka Chadema.
  Hata hivyo, Rugimbana alisema tangu kuanza kwa sakata hilo amezungumza na watu tofauti lengo likiwa kupata ukweli kuhusiana na malalamiko yalijitokeza, akisema leo atakutana na watendaji wake wa manispaa wakiwamo wa mipango miji ili kutatua tatizo hilo.
  “Nitafute kesho nitakupa taarifa rasmi baada ya kukutana na watendaji wangu” alisema Rugimbana na kuongeza kuwa yeye ndiye anayejua anaongea na nani na wakati gani.Sakata la kufungwa kwa barabara hiyo liliibuka mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya wananchi wanaoishi jirani na eneo hilo kulalamika.

  Source: Mwananchi.
   
 2. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Atashinda DIWANI!
   
 3. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Don't under estimate him. Watu wengine ni sawa na jeshi la Mtu Mmoja!
  Anaweza asipate support ya Mkuu wa wilaya+CCM lakini ana uhakika wa support ya wana-Kijitonyama.
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  umma/diwani

  Makinda a woman with no place/no use
   
 5. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  When we said this Mama is useless some people almost broke our necks......there she is at it again........she must have left her brains in ana exam room last time she did her exams
   
 6. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  wengine tunajenga kinyerezi huku hewa safi...yeye anajenga palipojaa tayari halafu anafunga bara bara?!!!! wa wapi huyu?
   
 7. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2011
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,406
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Kimsingi diwani ndio mwenye kauli na mtaa huo, huyo mama ukubwa wake ni huko mjengoni yeye pale ni mkaazi kama walivyo wengine,( nakumbuka miaka ya nyuma pele msasani MWL Nyerere alikuwa na mjumbe wa nyumba kumi kumi basi ktk vikao vya mtaa alikuwa anashiriki kama mkaazi na wala si Rais wa nchi) bali kuna tofauti kubwa ktk ya viongozi hawa na mwl Nyerere , kwani hawa wa sasa hawatofautishi KIONGOZI NA MTAWALA.
   
 8. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tunaposema serikali ya CCM inanuka kwa rushwa, ukandamizaji na uonevu hatukosei. Sasa wewe mama mzimaa anafuka barabara ili wananchi anaowaongoza wasipite? bogas kabisa huyo. Ndo kusema akina mama tunawezaaaa, mbona sasa anawadhalilisha wenzake?sheme on her!
   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Perception mbaya kabisa ya Ukubwa!
  Mi nilijua kuwa ukubwa ni utumishi kwa watu!
  Sasa anategemea jirani zake watapita wapi, kama si unyama huu?
  Mambo yakiwa magumu nguvu ya UMMA itumike...Haiwezekani mtu mmoja atese watu 300.
   
 10. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Anaona hata aibu.......

  [​IMG]
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hakuna kubembelezana nguvu ya umma itumike..
   
 12. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #12
  May 18, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Diwani atatumia nguvu ya umma
  na sija wahi sikia nguvu ya umma kushindwa mahali popote hapa Duniani,k
   
 13. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  diwani kishashinda kwa kuwa anazo support za wananchi na mimi nikiwamo!!

  nchi yetu haiishi vituko, sita alipopata uspika tu tukasikia bili ya matibabu yake ikwa around tshs. 1 or 2m kwa wiki (sikumbuki vizuri), mara tukasikia kajenga ofisi ya spika jimboni kwake urambo utadhani urambo ndiyo jimbo litakalokuwa likitoa maspika wa tz milele,

  sasa leo mtu mmoja kafunga barabara ili kupanua kiwanja chake!, mara eti sababu za kuisalama. osama bin laden (samahani kwa mfano huu ila nataka tu nieleweke vizuri) ndiye aliyekuwa akihitaji usalama mkubwa zaidi ya spika wa tz lakini nyumba aliyokuwa akiishi tuliona kwenye tv ikiwa na barabara kando yake!

  inaonekana watz wakipata madaraka fulani tu hupata ugonjwa fulani kwa ghafla!!

  yetu macho, ila for sure, nguvu ya umma itashind!
   
 14. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Aaah! Shangazi, hata huko ugenini unafanyaga yenyewe mambo hayo! Ishi vizuri na watu.
   
 15. s

  sawabho JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Diwani atatumia sheria ya mipango miji kushinda ikiwa barabara ilyozibwa iko kwenye ramani ya Kijitonyama.
   
 16. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kitu obvious kama hicho, mipango miji ya nini?? hapo ni nguvu ya umma tu basi, kibibi gula kinaenda kukenulia makanwa yake huko idodomya! shit!
   
 17. m

  msambaru JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Waheshimiwa wana JF naomba kujulishwa juu ya sakata la bibi makinda kufunga njia kwenye mtaa wake kumesababishwa na nini? au ndo sababu za kiintelejensia?
   
 18. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  nilitoa maoni on this matter hapa JF lakini wenye forum yao wakaamua kuichakachua bila sababu zozote zile

  just when you thought kuwa JF ingekuwa mtetezi wa wanyonge!
   
 19. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,472
  Trophy Points: 280
  si ilishafunguliwa?
   
 20. m

  msambaru JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Kama imefunguliwa kwanini aliifunga?
   
Loading...