Diwani aliyechomwa Kisu afariki dunia

easy tu,kama brother ben na mama anna.brother mguu,mama p.o.p kwani mmesahau?na walikua bdo magogoni.
 
aidha sijakuelewa
hawa ni viongozi they are model in the society

madhaifu ya kibinadamu yako palepale. Ndo maana madoc wanajua pathology za kila ugonjwa ila wao kazi yao kushauri tu. Wao ni wanywaji wa pombe,wavutaji wa sigara,waparamiaji wa wadada na wanakula vitu bila kunawa wakati wametoka kushika wagonjwa. Ni hasira ambayo inaweza kukupata wewe na mimi na tukafanya hivyo hivyo.
 
[h=2]27 DECEMBER 2011[/h][h=3][/h]

*Mtuhumiwa ni mpenzi wake, kiongozi wa chama

Na Mwandishi Wetu, Mvomero

DIWANI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Kata ya Mtibwa, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro, Bi.Tusekile Mwakyoma (28), amechomwa
kisu chini ya ziwa la kushoto na mchumba wake Mkurugenzi wa Mafunzo na Uenezi wa chama hicho, Bw.Songa Mgweno, mkazi wa Kijiji cha Kilimanjaro, ambaye alitoweka baada ya tukio hilo.

Akizungumza na Majira akiwa wodini katika Hospitali ya Misheni Bwagala, Bi.Mwakyoma alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana ambapo Bw.Mgweno, alikimbia na fedha zake sh.200,000.

“Huyu Bw.Mgweno ambaye ni mchumba wangu, alinipigia simu saa mbili usiku niende nyumbani kwake Kijiji cha Kilimanjaro ili nikachukue fedha zangu, niliamua kulala huko na ilipofika alfajiri, aliniamsha na kuniuliza nimefanya juhudi gani kuhakikisha wazazi wangu wanakubali anioe lakini nilimwambia sina jibu.

“Tuliendelea kulala lakini baada ya muda, alianza kunipapasa nikasikia maumivu makali chini ya ziwa la kushoto, baada ya kujichunguza, nikaona kisu kikining'inia,” alisema.

Aliongeza kuwa, Bw.Mgweno alimkaba koo na kuchomoa kisu hicho ili ampige kingine lakini alijitahidi kumdhibiti huku akipiga kelele kuomba msaada ambapo ndugu wa mwanaume waliamka na kwenda chumbani kwao kutoa msaada.

“Walipofika chumbani, walikuta Bw. Mgweno tayari amekimbia kupitia mlango wa nyuma,” alisema Bi. Mwakyoma.

Kwa upande wake, mpelelezi wa makosa ya jinai mkoani hapa, Bw.Hamisi Selemani, alisema jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa ili aweze kufikishwa mahakamani.

Mama wa Bi.Mwakyoma ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, alisema walimkataza mtoto wao asiendeleze uhusiano na Bw.Mgweno kwa sababu alikuwa na uhusiano na mwanamke mwingine ambaye ni kabila lake.

Baadhi ya wapiga kura katika kata hiyo, wamewaomba viongozi wa CHADEMA Taifa kumfukuza uanachama Bw.Mgweno kutokana na kosa alilofanya la kumshambulia diwani wao na kutaka kumuua.



 
Duh Mbona Wanachomana wao kwa wao! Mkurugenzi wa mafunzo anamchoma diwani!! Jamani acheni kuchomana.

Yaani na huyu diwani alichomwa na hakusikia kuwa kisu kimemchoma hadi anakigusa.

Pole diwani.
 
DIWANI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Kata ya Mtibwa, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro, Bi.Tusekile Mwakyoma (28), amechomwa
kisu chini ya ziwa la kushoto na
mchumba wake Mkurugenzi wa Mafunzo na Uenezi wa chama hicho, Bw.Songa Mgweno, mkazi wa Kijiji cha Kilimanjaro, ambaye alitoweka baada ya tukio hilo.

ALAA KUMBEE
 
MODS mbona hii ni habari ya siasa kabisa kwa kuwa inawahusu wanasiasa kwa nini mnaitoa kwenye Jukwaa la Siasa?
 
Duh Mbona Wanachomana wao kwa wao! Mkurugenzi wa mafunzo anamchoma diwani!! Jamani acheni kuchomana.

Yaani na huyu diwani alichomwa na hakusikia kuwa kisu kimemchoma hadi anakigusa.

Pole diwani.

mi mwenyewe nashangaa,yaani mtu anakuchoma kisu hupati maumivu na unaendelea kulala? Hii connection cjaipata. Hapa inaonekana kuna mkono wa ntu,wazazi wakigoma ndo umuue binti?
 
Mods mnatakiwa muunganishe hizi thread. Nyingine kama hii tumeitadili asubuhi.
 
Taarifa za kuaminika ni kwamba Diwani wa kata ya madizini Bi Tuse amefariki dunia leo mchana. Chanzo cha kifo ni kwamba alichomwa kisu mbavuni siku ya xmas na aliyekuwa mchumba wake, ambae baadaye bi Tuse alikataa jamaa kumposa ndipo jamaa akaamua kuwa bora akose na Tuse akose. Mungu amlaze pema peponi. Amin
 
Taarifa za kuaminika ni kwamba Diwani wa kata ya madizini Bi Tuse amefariki dunia leo mchana. Chanzo cha kifo ni kwamba alichomwa kisu mbavuni siku ya xmas na aliyekuwa mchumba wake, ambae baadaye bi Tuse alikataa jamaa kumposa ndipo jamaa akaamua kuwa bora akore na Tuse akose. Mungu amlaze pema peponi. Amin
Mungu ailaze roho ya marehemu peponi. Dah Uchaguzi mwingine tena na vurugu nyingine tena zikiandamana na uchakachuaji mwingine na Blah Blah zingine tena!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom