Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Kufuatia video aliyoipost mtangazaji Diva kwenye mtandao aliyokuwa akidendeka live na mpenzi wake GK, Diva amefunguka kuwa hayo ni maisha yake na kitu kinachompa furaha mno.
Diva ameenda mbali zaidi na kusema kuwa huwa hataki kusikia kitu kinaitwa mila na desturi za Kitanzania kama kile anachofanya kinamletea furaha katika maisha yake, anachojali yeye ni "kuwa happy".
Yuko tayari kufanya chochote kile, ilimradi kinampa tu furaha katika maisha yake.
Wiki hii mtangazaji huyo wa Clouds FM amesababisha mjadala mkubwa kwenye Instagram baada ya kupost video inayomuonesha akipigana French kiss na mpenzi wake rapper GK.
“Trying kanye west n kim k yummy tongie crazyyy kiss… guess what. wedding very soon #theregoesmybabyyyyy,” aliandika kwenye video hiyo.
“Nataka niishi the life that I want, mimi I don’t live to please anyone. I just live me as Diva, I just want to be happy,” Diva ameiambia Bongo5.
“The kiss to happiness – tongue kiss is the key to happiness ndio maana mimi sioni ajabu kumkiss mtu.”