Dini ni Utamaduni wa watu fulani

Ili swala la dini kuna mida unalibeba kama lilivyo na muda unaacha kama lilivyo ..mimi kwa upande wangu nishaacha kutoq sadaka na mchango wowote kanisani ,nikitoa ni mia 5 mwisho. Wakati mwingine sadaka yangu naona nipeleke kwa wenye uhitaji
 
Ili swala la dini kuna mida unalibeba kama lilivyo na muda unaacha kama lilivyo ..mimi kwa upande wangu nishaacha kutoq sadaka na mchango wowote kanisani ,nikitoa ni mia 5 mwisho. Wakati mwingine sadaka yangu naona nipeleke kwa wenye uhitaji
Bora kuwa baridi au Moto kuliko kuwa vuguvugu ukiamua kuachana nao wateme moja kwa moja sio unaenda afu hutoi sadaka.. illogical
 
Kuna maandiko yenye akili kubwa sana(wakatoliki watanisahihisha) kama ya Saint Thomas Aquinas na Ignas of Loyola. Kama wangeishi kabla ya Biblia, maandiko yao yangetumika kama 'kitabu kitakatifu' na pengine wangeitwa Mitume wa dini fulani.
una vitabu vyao? unaweza share
 
Uko 2000% right mkuu
Siku: Jumatano
Tarehe : kumi na tano /7/2020
Kipindi : witness
Tv: al jazirra
Master Wa temple ACC : Hui Liu
Nchi:Malawi

Ni kipindi kilichokuwa kikionesha jinsi M Buddha kutoka nchini Taiwan walivyokuwa wakichukua watoto na kuanza kuwafundisha watoto Wa Kimalawi utamaduni wao Wa ki Buddha na kusema wazi kuwa wamechelewa kuja Africa na kufundisha utamaduni wao huo(dini) na Laiti wangeanza wao kuja Africa Basi na sisi tungekuwa ms Buddha badala ya kuwa waislamu na wskristo, nikajiuliza waafrika tumekosea wapi? Kwanini Kila imani utufanye punching bag na kuleta maimani yao kwetu?
Big up kwa wamalawi waliokinukisha na kupigana na M master wa ki Buddha na kawaleta polisi na ma master wa ki Taiwan hao kurudishwa kwao
Dole la kati nawaonesha familia ya enock ambaye ma Buddha Hawa walimpa jina la alu(hajui lina maana gani kwa kichina) kwa kumshinikiza dogo enock aende Taiwan na kujifunza zaidi tamaduni hizi za kigeni.
Africa tukataeni hizi tamaduni za wageni (uislam ,ukristo,u Buddha n.k)
Nalog off
 
Funguka vizuri, sijakusoma fresh mkuu.
 
Uislam kwakuwa ni utamaduni wa kiarabu, wao Hadi leo huamini Mungu anajua kiarabu tu. Hakijabadilika chochote. Ni utamaduni tu, hata kichina na kijapani Mungu anakisikia.

***************
Hili linaukakasi kwakua si kila utaratibu hutumia kiarabu ikiwa ni shuruti Bali hii huwa shuruti katika zile swala tano na zile za ziada tu ila mengine hufanyika kwa lugha ya wenyeji wa nchi hiyo.


***********************************
KUHUSU UZI
Umenena vyema sana. Utamaduni ni kipengele tu katika dini. Dini huenda mbali na kujikita katika;

1. Tambuzi za uwepo wa nafsi
2. Yahusuyo Roho (kwa uchache wake)
3. Maisha baada ya kifo
4. Simulizi za maisha ya Kaburini
5. Uwepo wa Pepo na Moto na sifa za kuingia katika kimoja wapo

Aidha my personal observation ni kwamba unapochanganya Mambo ya Mungu na Tamaduni za kibinadamu mawili hutokea;

1. Huwezi mzungumzia binaadam bila kutambua uwepo wa chanzo chake ambacho ni Mungu

2. Huwezi mzungumzia Mwenyezi Mungu bila kuwa taja binaadam

Hivyo hao wanaojiita wapagani/sijui wanaoabudu Jua, Nyota nk. Ni kama kuamua kuchagua kiungo kimoja katika mwili na kuamua kukitukuza na kusahau kwamba mwili ni system inayotegemeana...
 
Ila ukinunua gadget na ukakuta user guide katika box la kifaa husika ni sawa?
 
Funguka vizuri, sijakusoma fresh mkuu.
Namaanisha siku ya Juma tano ya mwezi huu na mwaka huu,television ya al jazirra walirusha kipindi kiitwacho witness, kulikuwa kikionesha ma master wa ki Buddha kutoka nchini Taiwan ambao wako nchini Malawi jinsi wanavyoisambsza dini yao hiyo na kusema sasa ni wakati wao kuisambaza dini yao hiyo ya ki Buddha barani Africa.
Nikajiuliza Kwanini sisi waafrika ndio tuwe wapokezi Wa imani za watu wengine?
Africa tukataeni hizi tamaduni za wageni( uislam , ukristo,u Buddha n.k)
Nalog off
 
Mkuu umenena vyema. Hivi dada zetu walipokuwa wanaingia katika hedhi kipindi Waafrika hatuvai nguo uliwahi kupata simulizi walikua wanajisitiri vipi?

Waswana hadi leo hii watoto wa kike hawavai sidiria na kuyaacha matiti yao wazi? Unadhani wanaume waliouzoea utamaduni huo huhisi wanawake wale wanajidhalilisha?

Yapo mengi ya kujifunza usikimbilie kwenye lawama?
 
We ndo umeharibu kabisa sasa[emoji3][emoji3][emoji3]

Utamaduni sio sehemu ya dini, bali dini ndo sehem ya utamaduni. Rudi shule ukasome elements of culture mkuu[emoji3]
 
Kwahiyo kupaa/kutembea juu ya maji ndio kuwa mtu wa Mungu au Mungu kuonyesha uwepo wake?

Tunakosea sehemu moja kumtafuta Mungu kupitia vitabu vya Dini. Viweke pembeni hivyo vitabu kwanza kisha tafakari kwa kujiuliza zile impossible possibilities huko ndio sasa utatambua uwepo wa Mwenyezi Mungu
 
We ndo umeharibu kabisa sasa[emoji3][emoji3][emoji3]

Utamaduni sio sehemu ya dini, bali dini ndo sehem ya utamaduni. Rudi shule ukasome elements of culture mkuu[emoji3]
Nisaidie Mkuu kipi humbeba mwenzie kikubwa au kidogo?
 

Asante mkuu
Uzi umekuwa mfupi labda kutokana na uvivu wangu wa kuandika. Hayo yote uliyoorodhedha sijayatolea ufafanuzi lakini yapo vema na wazi katika 'culture'
~uwepo wa nafsi
~simulizi za maisha ya kaburi
~uwepo wa pepo na moto
~kuhusu roho
~maisha baada ya kifo
Hayo yote yanaingia kwenye 'Myths and Lengends' imani na Hadithi. Kuna hadithi nyingi za kiarabu na za kiafrika(kulingana na kabila husika) zinazoelezea hayo yote. Hadithi na imani hizo pengine tumezigeuza kuwa sehemu ya dini, Waarabu na wazungu walipofika Afrika walitukuta tuna knowledge kuhusu Roho, pepo,maisha baada ya kifo....yote yalikuwapo. Wakaleta yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…