Dini na Siasa zinategemeana ndio maana Dkt. Slaa anaweza sana Siasa, Mungu ndiye wa Pekee!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
89,457
154,684
Siasa na Dini zinafanya kazi moja tu ya kuwaunganisha binadamu kwa njia ya kuwatawala ili kuwaletea maendeleo ya kimwili na ya kiroho.

Kiongozi wa dini siyo lazima awe anamuamini Mungu ndio maana kuna dini ya shetani.

Hivyo hakuna tatizo lolote endapo viongozi wa dini wataamua kuungana na mfumo fulani wa viongozi wa kisiasa ambao kupitia kwao wanaamini haki ya binadamu ya kuishi kwa salama na kujipatia maendeleo ya kimwili na ya kiroho itapatikana kwa pamoja

Kanisa ni Ufalme na mfalme ni Yesu Kristo, hivyo mahusiano ya mtu na Mungu ni ya moja kwa !moja kwa sababu njia ya kumfikia Mungu ni Yesu mwenyewe siyo dini.

Yesu alisema " mimi ndio iNjia Kweli na Uzima "

Hivyo viongozi wa dini kukutana na wanasiasa ni jambo jema tena la kawaida kabisa kwani nao ni binadamu wanaoishi.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kamati ya Amani na Haki inajadili Amani Tu haijadili Haki wakati ili kuwe na Amani Haki lazima Itendeke ,Haki haitendeki ndio Maana Haijadiliwi.
 
CCM ikizidiwa dakika za mwisho Dr Slaa atatumika majukwaani
Dr Slaa ameachana na siasa za majukwaani. Binafsi namuomba apumzike kweli maana kwasasa nchi haipo kwenye tishio la kuangukia kwenye mikono ya hatari kama 2015.

Tupo vijana wake tunatosha kabisa kupima joto na kuhakikisha nchi inabaki kwenye mikono salama
 
Slaa hakuweza vyote, aliasi upande mmoja mlamu!
Dr Slaa alihudumu hadi level ya kuwa katibu mkuu TEC! Unafikiri ni nafasi ndogo na unaipata kiubwete tu? Kuna mambo usiweke siasa, muacheni apumzike!
 
Dr Slaa alihudumu hadi level ya kuwa katibu mkuu TEC! Unafikiri ni nafasi ndogo na unaipata kiubwete tu? Kuna mambo usiweke siasa, muacheni apumzike!

Mwishowe aliasi, akaoa na kujikita kwenye siasa... ndo nukta yangu hiyo.
 
Dr Slaa alihudumu hadi level ya kuwa katibu mkuu TEC! Unafikiri ni nafasi ndogo na unaipata kiubwete tu? Kuna mambo usiweke siasa, muacheni apumzike!

..kuna wanaodai aliacha Upadre kwasababu alinyimwa nafasi ya kuwa Askofu kule kwao.

..akaondoka ccm kwasababu ya kunyimwa nafasi ya kugombea Ubunge wa Karatu.

..na akaondoka cdm baada ya kupigwa kikumbo na EL kuwa mpeperusha bendera wa Ukawa.

NB:

..Dr.Slaa angebaki CDM leo hii angekuwa amefumuliwa na kuumizwa kama TL.

..naamini huko aliko Dr.Slaa anamshukuru MUNGU kwa kumuepusha na mkono wa chuma wa awamu ya 5.

..mimi sikumpenda EL kabisa. nili-support chama / demokrasia / mageuzi / na siyo mgombea.
 
Mkuu hizo ni propaganda. Kama hujui hakuna anayeweza kupanga kuwa askofu maana ni uteuzi wa Papa. Alafu huu sasa ni unafiki maana hayo yote uliyotaja ambayo ni 90% ni kabla ya kujiunga CDM, ndio mmejua leo?

Sad, na wewe umekuwa propagandist wa vyama! Hivi ukisema uliunga chama mkono si mgombea unataka kusema nini? Zile sarakasi za kihuni pamoja na matokeo yake leo huna hata aibu bado unajiambatanisha nayo?

Kwanza hakika moja kubwa kabisa ni Chadema haitaweza tena kurudi ilipokuwa, walisaliti mageuzi ya kweli na ule ndio ulikuwa mwisho wao! Baada ya uchaguzi wa mwaka huu ndio utaelewa!

Naamini Watanzania wa leo si wa kesho, tutapata watu waaminifu wataoipeleka nchi ya ahadi lakini si hawa wanasiasa wa sasa wakiwemo wapinzani. Mpaka sasa JPM ndipo nafuu kubwa ilipo upende usipende! No options!
 
..Naomba unisome kwa utulivu na kituo.

..Lowassa aliingia CDM na kuwakuta wanachama wengi wazuri, waadilifu, waliokijenga chama.

..sasa mimi nisingeweza kuwatupa mkono hao kwasababu ya sarakasi na makando-kando ya kumpokea Lowassa.

..pia HAKI, mageuzi, demokrasia ya vyama vingi, utawala wa sheria na katiba, maendeleo, ni ajenda kubwa na pana ambayo imebebwa na vyama vya upinzani.

..zaidi, Lowassa ameshatimka kurudi "nyumbani," kwa hiyo utaona kwamba haikuwa busara kumsusia chama.

..Jpm siyo muumini wa demokrasia ya vyama vingi, hili mimi nilishaliona tangu alipokuwa waziri. kumuunga mkono ni sawa na kusema turudi miaka ya 60 ambapo mfumo wa vyama vingi ulifutwa. Na haijulikani huyu bwana mkubwa atakaa madarakani miaka mingapi.

..Zaidi, hii hali ya kumwaga damu za watu halafu baadhi yetu wanasifia na kufurahia mimi naona siyo sahihi kabisa, kabisa, kabisa.

..Miundombinu inawezekana bila kuua, kutia watu ulemavu, au kutweza utu wa waTz wenzetu.
 
Back
Top Bottom