Madumbikaya
JF-Expert Member
- Jun 6, 2018
- 638
- 1,902
Ni wangapi wanaabudu KKKT au Catholic hapa Tanzania ?
Ni wangapi ni wakristo Jina hapa Tanzania yaani wamebatizwa na kupokea sakramenti zote lakini hawapendi au hawahudhurii huko makanisani ?
Majibu ya maswali hayo mawili ndio yanaleta mikanganyiko katika mifumo yetu ya kiutawala kati ya serikali na Dini, Nitajadili hii mada kwa muktadha wa kutenganisha Dini na Siasa
Mosi, Viongozi wa Dini lazima watambue kuna maelfu ya watu ambao ni wapagani wasiosali kabisa, Kundi hili linahitaji nyaraka nyingi sana za kuhamasishwa au kuonywa na ndio kondoo waliopotea
Waraka wa TEC ya Catholic na KKKT hakuna mahala wamegusa Kundi hili la wapagani zaidi wamekimbilia kujibizana na mamlaka ya kiserikali, Hakuna utendaji ambao mpaka sasa umeathiri mamlaka hizi za kidini kufanya kazi zao
Pili, Mamlaka ya Serikali imekuwa ikijificha nyuma ya mimbari za makanisa zikitoa misaada na kuomba kuongea hasa wakati wa sherehe ili kujijengea umaarufu, Lakini mpaka sasa mamlaka za kidini hazikiri kama wameathirika kwa lolote toka mamlaka za kiserikali
Tatu, Mialiko katika warsha,Semina na sherehe. Mamlaka hizi zimekuwa zikisifiana na kupongezana kuwa zinajenga Taifa la kizalendo Huku mamlaka ya kikanisa ikisahau wao wanasimamia upande wa wachache wanaohudhuria kwenye mimbari yao wakiacha kondoo wengi wajichunge wenyewe
Ni nani wa kumvisha mwezake kengele mamlaka za kidini au mamlaka za kiserikali ?
Mamlaka za kidini hazina uwezo wa kumvesha serikali kengele kulingana na matukio mengi yaliyotokea kwa uzoefu na historia ya haya makanisa juu ya waumini wake, Kanisa hasa Afrika lilikuja kwa mgongo wa kutoa huduma yaani hospital, maji na barabara kitu kilichowafanya wawe karibu na mamlaka za kiserikali, Serikali nyingi baada ya kuona mamlaka za kidini zina nguvu walianza kutaifisha mali za makanisa
Waraka na nyaraka zinazotolewa leo nyingi zimejikita kusifia serikali wakati Kundi kubwa lisiliokuwa washiriki likilalamika juu ya mamlaka ya kidini, Wakati mamlaka za kidini zikikosoa sasa zinahitajika kusahihisha kauli zao mbele ya waumini wao na mbele ya kondoo waliopotea
Hitimisho, Ni muda muafaka kila mtu atumie meza yake mwenyewe kuonya na kuhubiri, kulazimisha kualikana kwenye mimbari na majukwaa Huku mkitambua kuna Kundi ambalo halipo kati yenu ndio yanayotokea sasa ya kuanza kuombana katiba na usajili upya