Dini na Serikali zinapotumia meza moja isiyokuwa na viti

Madumbikaya

JF-Expert Member
Jun 6, 2018
637
1,901
Ni wangapi wanaabudu KKKT au Catholic hapa Tanzania ?

Ni wangapi ni wakristo Jina hapa Tanzania yaani wamebatizwa na kupokea sakramenti zote lakini hawapendi au hawahudhurii huko makanisani ?

Majibu ya maswali hayo mawili ndio yanaleta mikanganyiko katika mifumo yetu ya kiutawala kati ya serikali na Dini, Nitajadili hii mada kwa muktadha wa kutenganisha Dini na Siasa

Mosi, Viongozi wa Dini lazima watambue kuna maelfu ya watu ambao ni wapagani wasiosali kabisa, Kundi hili linahitaji nyaraka nyingi sana za kuhamasishwa au kuonywa na ndio kondoo waliopotea

Waraka wa TEC ya Catholic na KKKT hakuna mahala wamegusa Kundi hili la wapagani zaidi wamekimbilia kujibizana na mamlaka ya kiserikali, Hakuna utendaji ambao mpaka sasa umeathiri mamlaka hizi za kidini kufanya kazi zao

Pili, Mamlaka ya Serikali imekuwa ikijificha nyuma ya mimbari za makanisa zikitoa misaada na kuomba kuongea hasa wakati wa sherehe ili kujijengea umaarufu, Lakini mpaka sasa mamlaka za kidini hazikiri kama wameathirika kwa lolote toka mamlaka za kiserikali

Tatu, Mialiko katika warsha,Semina na sherehe. Mamlaka hizi zimekuwa zikisifiana na kupongezana kuwa zinajenga Taifa la kizalendo Huku mamlaka ya kikanisa ikisahau wao wanasimamia upande wa wachache wanaohudhuria kwenye mimbari yao wakiacha kondoo wengi wajichunge wenyewe

Ni nani wa kumvisha mwezake kengele mamlaka za kidini au mamlaka za kiserikali ?

Mamlaka za kidini hazina uwezo wa kumvesha serikali kengele kulingana na matukio mengi yaliyotokea kwa uzoefu na historia ya haya makanisa juu ya waumini wake, Kanisa hasa Afrika lilikuja kwa mgongo wa kutoa huduma yaani hospital, maji na barabara kitu kilichowafanya wawe karibu na mamlaka za kiserikali, Serikali nyingi baada ya kuona mamlaka za kidini zina nguvu walianza kutaifisha mali za makanisa

Waraka na nyaraka zinazotolewa leo nyingi zimejikita kusifia serikali wakati Kundi kubwa lisiliokuwa washiriki likilalamika juu ya mamlaka ya kidini, Wakati mamlaka za kidini zikikosoa sasa zinahitajika kusahihisha kauli zao mbele ya waumini wao na mbele ya kondoo waliopotea

Hitimisho, Ni muda muafaka kila mtu atumie meza yake mwenyewe kuonya na kuhubiri, kulazimisha kualikana kwenye mimbari na majukwaa Huku mkitambua kuna Kundi ambalo halipo kati yenu ndio yanayotokea sasa ya kuanza kuombana katiba na usajili upya
 
Makanisa yapigwe marufuku ili nchi itawalike kirahisi
Bujibuji hizi mamlaka zimezungukana wakati huu, kipindi cha katiba mpya mamlaka hizi zilitumika zote kuzima maoni ya wananchi

Kumbuka Gwajima wakati wa katiba ya warioba alipojibizana na Askofu Pengo kuhusu kuzima maoni ya wananchi

Leo mamlaka ya kidini na kiserikali lazima zitambue wananchi ndio wenye nchi wao ni watoa sera na miongozo acha waveshane kengele
 
Mwisho wa kanisa kutumika kama asasi ya CCM ni sasa
 
Dini na siasa havija achana hata siku moja. Kuna dini katika siasa na siasa katika dini kwani wote wanahudumia watu wale wale. Kwa nchi zinazoendelea taasisi za dini pia huwa na jukumu LA KIROHO la kuangalia mwenendo wa serikali katika kutawala, wakiona mistari fulani inavukwa ni jukumu lao kusema.
 
Maelfu wasio kuwa na access au upatikanaji wa hizo Waraka wanamsikiliza nani ? Hawa Viongozi wa dini ni kwa ajili ya waumini wao, Wengine sidhani Kama nyaraka zinawahusu kwani hawaamini katika Viongozi au makanisa hayo, Nyaraka zingetumika kujenga Kanisa na sio mapambano na watawala, watawala huja na wanapita haya makanisa Afrika yapo muda mrefu
 
This time halitabaki Jiwe juu ya Jiwe!! Kanisa linaenda kuamka na kushika hatamu.
Litaamka kuelekea wapi mkuu, kosa kubwa ni wao kuhusisha mambo yao ya mamlaka ya kiserikali kwenye mimbari za Kanisa
Acha wapeleke katiba ya 1963 ifanyiwe editing
 
Maelfu wasio kuwa na access au upatikanaji wa hizo Waraka wanamsikiliza nani ? Hawa Viongozi wa dini ni kwa ajili ya waumini wao, Wengine sidhani Kama nyaraka zinawahusu kwani hawaamini katika Viongozi au makanisa hayo, Nyaraka zingetumika kujenga Kanisa na sio mapambano na watawala, watawala huja na wanapita haya makanisa Afrika yapo muda mrefu
So hao wasiokuwa na access na Mambo ya imani na wao hawaguswi na vifo, utekaji, ajira na mengineyo?
 
I thought fools normally write short stupid, nonsense sentences, but i was wrong. Look at this fool!!! Maelezo mareeeefu halafu pumba tupu. Pole sana. Tuna safari ndefu sana....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom