Mafilili, thread yako inadhihirisha pasipo shaka madhara ya shule za kata, ambazo umesoma bila kufuata mitaala inayo eleweka. Na tatizo ulilo nalo linachagizwa zaidi na utumiaji wa viroba asubuhi badala ya chai, na kubwiya unga badala ya chakula.
Turudi kwenye mada ndugu; Mfumo wa Analogia / Digital unahusika vipi kuwafikishia wananchi ukombozi wa ki-fikra via M4C ?
CHADEMA imepeleka madaraka kwa wananchi kwa kupitia sera ya majimbo, hivyo basi wanashiriki moja kwa moja kuwachagua viongozi wao wanaowataka, hii ina maanisha wanaifahamu vizuri sana sera ya majimbo kwani wana shiriki kuitekeleza kwa vitendo na hawahitaji cha analogia wala Digital, kuliko wewe unayekesha kwenye key board hapo Lumumba kwa kufukuzia ujira wa sh. 7,000 /= kwa kila post.
Nijuavyo mimi, siku zote maCCM, Magambaz, Mafisadi, Misukule wa Lumumba na msiojitambua mnaiombea CHADEMA ife na ifutike kabisa katika uso wa dunia, kwa bahati nzuri Mungu yu upande wetu mmeshindwa na hamtashinda kamwe. Iweje leo muibuke na agenda ya kutorusha matangazo ya bungeni Live, ati kuiokoa CHADEMA kutokana na aibu ya Wabunge wake. Hiyo Roho nzuri mmeipata wapi ?
Mkuu Mafilili, kila mtu anajua agenda ya siri iliyogubika mfumo wa digital, labda wewe na familia yako ndo hamjui, na sijui mnaishi nchi gani? Sababu za kutaka kusitisha matangazo ya bungeni live zinajulikana hata kwa watoto wa darasa la pili, sijui utamdanganya nani?
Naomba nisikuchoshe kwa leo; Rai yangu kwako na misukule wenzako; Jiandaeni Psychologically jinsi ya kuishi mjini, otherwise mrudi kijijini mkalime, kwani mda si mrefu kibarua chenu cha kuandika taarab hapa JF kitaota nyasi, na siku za kuendelea kupokea ujira wa sh. 7,000/= kwa kila umbeya / uongo / Uharo/ Upumbavu / Ujinga / Uzandiki na takataka zote mnazo post hapa jamvini zinahesabika.