Digitali Yaisadia CHADEMA Kisiasa

Digitali Yaisadia CHADEMA Kisiasa

MAFILILI

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Posts
2,377
Reaction score
1,200
Mfumo wa Digitali umeleta faida kubwa kwa CHADEMA ambao wanaendesha harakati zao za kisiasa kupitia TV; kuzimwa kwa mfumo wa analojia kwenye baadhi ya mikoa nchini imekuwa ni kupunguzwa kwa watazamaji wa TV ambao walikuwa wanapata sera za CHADEMA kupitia matangazo husika. Mfumo wa digitali ambao umekuja na matumizi ya ving'amuzi umepunguza idadi ya watazamaji wa TV hivyo kusababisha watanzania wengi kutopata uhalisia wa viongozi wa CHADEMA huku tukielekea chaguzi za 2014 na 2015.

Kutoangaliwa na wananchi wengi imesaidia CHADEMA kutojulikana kiundani juu ya sera zao za kugawanya watanzania kwa misingi ya jiografia na kiimani. Pia wabunge wa CHADEMA wamefaidika kwa kutoonekana wakati wanaposhiriki vikao vya bunge; vinginevyo wananchi wangekata nao tamaa kutokana na MTINDO WA WABINGE WA CHADEMA KUWEKA MBELE MASLAHI YA CHAMA BADALA YA MAJIMBO HUSIKA, suala ambalo ni kuweka rehani ubunge wao.

Yote kwa yote teknolojia mpya imeleta faida kubwa kwa CHADEMA kwa vile AIBU zao hazionwi na watanzania wengi hivyo kuwanyima wanannchi wengi fursa ya kupata udhaifu wa chama hicho kisicho na mtazamo wa kuenea katika pande zote za nchi :embarassed2:
 
MAFILILI hivyo unashauri turudi analogia?
 
kwa sasa cdm imejikita vijijini inapiga m4c balaa,na imeshapanga safu zake za kugombea nafac zote kuanzia ngazi ya kitongoji/mtaa hadi ubunge.we subiri uone.
 
Nifafanulie yupi anaboroga bungeni kama sio mbunge wa CCm mi nadhani wabunge wa upinzani wanafahamu wanachokifanya bungeni
 
kwa sasa cdm imejikita vijijini inapiga m4c balaa,na imeshapanga safu zake za kugombea nafac zote kuanzia ngazi ya kitongoji/mtaa hadi ubunge.we subiri uone.

hata sangala ulisema hivi,sasa wapi sangala yenu
 
Nifafanulie yupi anaboroga bungeni kama sio mbunge wa CCm mi nadhani wabunge wa upinzani wanafahamu wanachokifanya bungeni

Lema ni kinara wa kuanzisha vurugu bungeni, tangu aingie bungeni hajawahi kuuliza ama kuchangia hoja za kimaendeleo
 
Nifafanulie yupi anaboroga bungeni kama sio mbunge wa CCm mi nadhani wabunge wa upinzani wanafahamu wanachokifanya bungeni

wenje,msigwa,sugu na lema hawarudi mimi na weka mil 2.mungu atupe uhai tufike 2015.tuone
 
Kwa hiyo ccm wameingia hasara kwa kuikosa analojia.?
 
wapeleke ving,amuzi kwa kila mwananchi huko vijijini wanahela za wazungu hawa lkn wasisahau kununua na tv mana ni isseu pia kule kwetu utakuwa mwanzo mzuri :heh:
 
kwa sasa cdm imejikita vijijini inapiga m4c balaa,na imeshapanga safu zake za kugombea nafac zote kuanzia ngazi ya kitongoji/mtaa hadi ubunge.we subiri uone.

Kwa taarifa yako CDM haijawahi kukanyaga katika vijiji vilivyoko wilaya ya Tunduru, Kilwa, Liwale, Mbinga, Namtumbo, Pangani, Kilindi, Kilombero, Mafia hizo ni baadhi ya wilaya ambazo CDM haiwezi kupata uongozi wa vijiji. Wilaya za mkoa wa Mtwara, CDM ilifanya mikutano ya zimamoto ambayo haijaacha ofisi endelevu
 
Lema ni kinara wa kuanzisha vurugu bungeni, tangu aingie bungeni hajawahi kuuliza ama kuchangia hoja za kimaendeleo
Mimi nishamuona mara chungu nzima anauliza maswali labda wakati huo unakuwa umelala
 
Kwa taarifa yako CDM haijawahi kukanyaga katika vijiji vilivyoko wilaya ya Tunduru, Kilwa, Liwale, Mbinga, Namtumbo, Pangani, Kilindi, Kilombero, Mafia hizo ni baadhi ya wilaya ambazo CDM haiwezi kupata uongozi wa vijiji. Wilaya za mkoa wa Mtwara, CDM ilifanya mikutano ya zimamoto ambayo haijaacha ofisi endelevu

Basi wamekusikia mtoto mzuri
 
Ni dhairi kuwa huo ni mtazamo wa mtu aliyefilisika kifikra ama aliyeamua kuweka kando uwezo wake halisi wa kufikiri na kupambanua masuala/mambo na kujitwika ujuha kwa maslahi ya ndugu tumbo.

Kama wewe nimakini na mfuatiliaji wa masuala ya siasa nchini , ni wazi kuwa utakubaliana nami kuwa kuzimwa kwa mitambo ya analojia na kukimbilia dijitali( hata kabla ya deadline ya UN-2015) unakisaidia sana chama cha mapinduzi, kwani kwa sasa watanzania wengi hawezi kupata habari njema za ukombozi zinazohubiriwa na CHADEMA kote nchini.
Serikali yako imefanya hivyo makusudi ili kuinusuru CCM na aibu inayowapata.

Pia utambue kuwa vyombo vya habari hasa vya televisheni (mfano TBC1) vimekuwa vikifanya ubaguzi wa wazi kuripoti habari zihusuzo CHADEMA na upinzani kwa ujumla, hivyo kwa kutambua hilo CHADEMA imeamua kwenda kwa wananchi moja kwa moja, kijiji kwa kijiji ili hatimaye habari hii njema iwafikie wote licha ya vikwazo vyenu.

WASWAHILI HUSEMA HUWEZI KUZIBA TUNDU/SHIMO LA PANYA KWA MKATE......TAFAKARI
 
Lema ni kinara wa kuanzisha vurugu bungeni, tangu aingie bungeni hajawahi kuuliza ama kuchangia hoja za kimaendeleo

kama Serukumba, Mwigulu, huy wa Dodoma mjini nani huyu bubu..., Lusinde, Vicky.... na wengineo...
 
Kwa taarifa yako CDM
haijawahi kukanyaga katika vijiji vilivyoko wilaya ya Tunduru, Kilwa,
Liwale, Mbinga, Namtumbo, Pangani, Kilindi, Kilombero, Mafia hizo ni
baadhi ya wilaya ambazo CDM haiwezi kupata uongozi wa vijiji. Wilaya za
mkoa wa Mtwara, CDM ilifanya mikutano ya zimamoto ambayo haijaacha ofisi
endelevu

yawezekana hujui kinachoendelea,cdm ni chama dume kwa taarifa yako mikakati inayoendelea mtapata pigo takatifu.
 
Back
Top Bottom