GE2025 Digital memorial/Archive for Lives Lost in Tanzania’s Recent Violence

GE2025 Digital memorial/Archive for Lives Lost in Tanzania’s Recent Violence

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Girl Poet

Member
Joined
Sep 5, 2025
Posts
21
Reaction score
54
The last couple of days, tumeshuhudia ndugu, marafiki, na jamaa zetu, wakubwa kwa wadogo wakiuwawa bila huruma yoyote. 💔

MAY THEY REST WELL!

Tunayopitia ni magumu, ila kwa neema ya Mungu na kwakufarijiana, tutafika.😔

Kila nikiingia online nakutana na videos mpya za watu waliouwawa, ama wakipigwa risasi, na niki-scroll zaidi nakutana na picha za baadhi ya watu ambao maisha yao yamefupishwa wakililiwa na ndugu ama jamaa zao. Majina yao yanatajwa na wengine taarifa za walikuwa wapi, wakifanya nini, na namna gani walipoteza maisha zinawekwa wazi.

Kama hawa...
1762299217066.jpg

Hichi kitu kimenifikirisha sana.

Hundreds of people, or maybe even thousands lost their lives, tunawalilia lakini hatuwajui na tunawasikitikia kwa ujumla wao tu, which means, hata kuwakumbuka itakua hivyo hivyo. And it hurts to think of all our fallen brothers, sisters, mothers, fathers, daughters, and sons being reduced to nothing but a collection of bodies and unverified numbers. I feel like we need to do something to honour them in a way that makes sense, not just to mourn, but to remember them properly, leo, kesho na kesho kutwa.

JamiiForums mmeshaanza kwa kuanzisha special thread ya mkusanyiko wa videos & picha za mauaji yaliyotokea (asante sana Maxence Melo & uongozi wote wa JamiiForums for that 🙏🏾) na pengine mlishafikiria kuanzisha what I'm suggesting here, ila haigombi kukumbushana.

Naomba muangalie ni namna gani tunaweza kuanzisha database/ digital memorial ya ndugu zetu tuliowapoteza. Something simple but respectful ikiwa na taarifa zao muhimu (majina, umri, walipokuwepo & jinsi walivyouwawa, walichokuwa wanajishughulisha nacho ama ndoto zao kama bado walikua wadogo sana, na picha zao enzi za uhai wao), kadri zitakavyopatikana na familia zao zitakavyoruhusu.

Best way to collect data would be for families, friends, or anyone who knew them to share the information privately with an admin, taarifa kuwa verified, kisha kuwekwa kenye record.

Mpaka sasa hivi idadi ya waliopoteza maisha haijulikani kwa uhakika, yaweza kuwa mamia, yaweza kuwa maelfu, hii initiative itatusaidia pia kupata makadirio ya kweli zaidi.

What do you all think?

Pia kwa kuongezea, ninge-suggest kwenye ile thread ya video na picha za mauaji, admin tu ndio wapost. Wenye videos na picha watume kwa utarabu ili vitu viwe kwenye mpangilio mzuri badala ya kila mtu kupost tu kiholela na wakati mwingine kurudia.
 
Back
Top Bottom