Differences between a Lawyer and an Advocate (Tanzanian perspective)

nsangu

New Member
Mar 7, 2013
3
16
Tuanze kwa kubadili lugha kwanza, iko hivi; Lawyer ni mwanasheria, Advocate ni wakili.

Tuanzie hapa sasa:
Kila Wakili ni Mwanasheria, ila sio kila Mwanasheria ni Wakili

Kimsingi, mtu yeyote aweza kuwa Mwanasheria ikiwa atasoma taaluma ya sheria kwa ngazi ya shahada (LL.B), lakini ili kuwa Wakili ni mchakato mrefu zaidi.

Mchakato wa mwanasheria kuwa wakili:

Mchakato huu unawahusu tu wale waliohitimu shahada ya sheria kuanzia mwaka 2008 na kuendelea.

Kwamba baada ya kupata shahada ya sheria utatakiwa uende tena chuo cha sheria (law school) ukasome na kufaulu Post Graduate Diploma in Legal Practice ndipo upate sifa ya kuwa wakili.

Baada ya kuipata hiyo sifa bado hujawa wakili, wewe bado ni mwanasheria. Ili uwe wakili utatakiwa ufungue maombi maalumu (petition) kwenda kwa jaji mkuu kumuomba akupokee na akuapishe, naye baada ya kukufuatilia tabia na mwenendo wako, kukufanyia upembuzi wa maandishi katika nyaraka zako zote na mahojiano yakinifu ya mdomo (interview) akiridhika ndipo atapanga siku ya kukuapisha.

Ndipo baada ya kuapishwa sasa utakuwa wakili.

images%20(4).jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini wanajiita wakili msomi?
Mwanasheria "msomi" ni yule ambaye ni wakili.

Anaitwa msomi kwa sababu wakili katika utendaji wake ana uwezo wa kumwakilisha mtu mwingine mwenye fani yoyote mfano dokta, injinia, rubani n.k

Kwamba anapomwakilisha mtu mwingine, mtu huyo anayewakilishwa mahakamani humtegemea wakili kumsemea na kumwongoza kwa kila jambo hata yale ya fani yake pia.

Kwamba, wakili amefuzu kupembua na kupepeta mambo mbali mbali kwa wakati mmoja na kutengeneza mawazo ya msingi ambao unaweza kutumiwa katika maamuzi sahihi.

Hii haimaanishi fani nyingine haziwezi, lakini Wakili amepitia mafunzo pekee, na uwanja wake wa utendaji ni pekee(Mahakama)...na matumizi ya mafunzo yake ni pekee.

Kwa hiyo huyu ni msomi wa mambo yake na ya wengine kwa ujumla wao.

Kwa kifupi ni hivyo, natumai imeeleweka.

Nitaweka uzi wa hii mada.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanasheria "msomi" ni yule ambaye ni wakili.

Anaitwa msomi kwa sababu wakili katika utendaji wake ana uwezo wa kumwakilisha mtu mwingine mwenye fani yoyote mfano dokta, injinia, rubani n.k

Kwamba anapomwakilisha mtu mwingine, mtu huyo anayewakilishwa mahakamani humtegemea wakili kumsemea na kumwongoza kwa kila jambo hata yale ya fani yake pia...
Asante sana kwa ufafanuzi huo, hongera sana kiongozi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaa......wakili msomi nchi hii ni mmoja tu Tundu Lissu. Hivi ni nini Hatma ya Fatma Karume baada ya kupokwa uwakili wake?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom