Wakuu...maelezo yote nimeyapenda ila ninapata shida ya lugha mnayotumia kuelezea hizo AC na DC.
Mnaposema AC inakwenda mbele nyuma, DC mbele kwa mbele mnamaanisha nini??? Na hasa hiyo mbele nyuma.
Alternating Current(AC) - Mkondo geu
Direct Current(DC) - Mkondo mnyoofu.
Nadhani AC inapotumika kuwasha balbu ile kama mtungi yenye filament, balbu huwaka na kuzima mara 50 kwa sekunde moja, hii ni kwa mfumo wa TZ na baadhi ya nchu tutumiazo 50Hz.
DC inapotumika kuwasha balbu iliyo kama mtungi, balbu itawaka bila kuzima kwa muda itakayokuwa imeungwa kwenye chanzi cha DC.
Sehemu kubwa ya vifaa vya electronics vinatumia DC supply i.e TV, Radio, Simu, n.k Unaweza ona supply ya TANESCO ndio inayoingia kwenye vifaa vyako(Tanesco ina-supply AC) ila kimsingi ni kwasababu si ghali sana kusambaza AC kama ilivyo DC, hivyo vifaa vingi vya electronics vinapokea AC kwa TRANSFORMER, AC inapoozwa pengine kutoka 240VAC mpaka 24V au 12VAC kwa transformer kisha unapitishwa kwenye RECTIFIERS(Diodes) zilizoungwa na capacitor kwaajili ya kubadili kutoka AC kwenda DC kisha kutumika ndani ya kifaa husika kama ni radio au chochote.
Umeme wa DC unahifadhika, AC hauhifadhiki.
Nadhani hiyo pia itasaidia kuelezea hiyo tofauti ya AC na DC.