Diaspora wa kitanzania wengi wao hawana sifa za Diaspora

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,383
4,318
Katika kipindi cha Majadiliano asubuhi ya leo Redio TBC Taifa imeonekana watanzania waliowengi hawana sifa za Diaspora kama nchi za India,Thailand,Zimbabwe n.k

Majadiliano hayo kuolekea Kongamano la 4 la wana Diaspora litakalofanyika hivi karibuni chini ya Paskali Mayala mgeni ktk kipindi hicho Dr Willard Shayo alizieleza sifa za mwana diaspora.
  1. Mtanzania aliyeondoka nchini kihalali.
  2. Mtanzania aliyejisajili ktk ubalozi nje ya nchi ili kufahamika kazi yake na makazi yake.
  3. Mwenye vyeti halali vya kuishi huko anakoishi.
  4. Mwenye kazi halali na kipato kinachojulikana.
  5. Mwenye kujua kuwa yuko nje ya nchi na anajua alikotoka na ana wajibu ktk jamii alikotoka na kuweza kuwa na mawasiliano na jamii alikotoka.
  6. Mwenye utayari wa kupokea maelekezo ya nchi alikotoka ili kufanya uwekezaji,biashara au kutuma pesa,kufanya makongamano ya diplomasia ya kiuchumu n.k
Sasa iinaonekana watanzania wengi wanaojiita diaspora hizi sifa ni shida kuwa nazo.

Lakini Paskali Mayala amejitahidi kueleza kuwa wana diaspora wa kitanzania kweli hizo sifa wengi wao hawana lakini si kigezo cha kuwakatisha tamaa la msingi ni kuwa sisi Tanzania hivi vigezo ni vigumu kuwa navyo basi hivyo hivyo tutumie vigezo walivyonavyo kwa Sasa ili hawa wana diaspora tulionao waweze kujulikana na kuwekeza Tanzania na kuifanya jumuiya ya watanzania wana diaspora kuwa Kimara zaidi na kuchangia maendeleo ya kiuchumi ktk nchi yetu.
 
Back
Top Bottom