Diaspora Hawatoi connection?

Bufa

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
10,656
21,083
Naandika huu uzi baada ya kusoma na kusikia mara kadhaa kwamba diaspora wabongo hawatoi connection za kwenda nje compared to diaspora wa nchi kama Kenya, Nigeria nk. Mimi kama diaspora napinga hii notion vikali.

Hapa JF Kuna nyuzi zaidi ya 100 zinazojadili jinsi ya kwenda nje, a quick search mtu unapata majibu yote na bado watu tunachangia nyuzi kila leo. Mnataka connection gani zaidi?

EBM anatoa free knowledge on YouTube na bloggers wengine jinsi ya kwenda nje, hiyo sio connection? Tuwape bundle za kuingia youtube au?

Mimi binafsi nimeshirikiana na watu kadhaa toka kwenye forum hii hii toka walipoanza harakati zao za kwenda nje na sasa wapo mbele needless to say walifanya sehemu zao na mambo yao yakafanikiwa. Sasa urafiki umekua undugu. Tatizo ndugu zangu wamatumbi mnapotaka connection mnataka hao diaspora wawape hadi hela na passport wawatafutie. You have to play your part as well.

Kimsingi kwenda nje is as easy as ABC. Kupata connection ni vizuri but isn't everything. Mimi nilienda bila connection yeyote ile, maelezo yote yapo kwenye websites za nchi husika ila ni lazima uwe tayari kufanya sehemu yako pia, kuna watu wanadhani diaspora wana a magic code ya kwenda nje this couldn't be further from the truth. Ni lazima uwe tayari kufanya sehemu yako.

Wabongo wenzangu punguzeni kulalamika kiboya, JF Kuna more than 100 threads, YouTube ipo, website za nchi husika zipo, tunajitoa as much as we can but we can only do so much. Maisha yako ni jukumu lako, kusaidiana kupo ila sio wajibu.

Nipo around mazee.

wabongo kwenye kusaidiana bado sana mfano mtu ana kila kitu passport,nauli na hela ya kujikimu akiwa mfano marekani kupata mchongo wa kwenda mbele inakua mziki wakati kuna mwaliko tena mtu anaweza kukulipa kidogo kufidia muda wako,kuna internship tunaweza kuonganishiana ata kwa malipo siyo mbaya au kusaidiana link ya vyuo vya bei nafuu kabisa ila kwa mbongo hapo kipengele kukupa mwongozo tuna ogopana sana.

Mkuu kwa mfano mimi nakualika wewe kama nani yangu au kwenye function gani?

Nadhani wengi mnadhani mualiko wowote tu unatosha kupewa visa ila hamjui ni lazima muwe na ukaribu na huyo mtu na wewe as a visitor uonyeshe upo well established nyumbani na utarudi ili upewe visa kigezo ambacho vijana wengi hawana maana ndo wanatafuta maisha. Kama haupo vizuri bongo kwa maana ya a stable job au business, assets, ndoa, watoto, na hela visa ya kutembea kwa mualiko ni mtihani.

Niseme tu diapora wanatumia internet hii hii kutafuta hizo internships na kazi mnazotaka wawajulishe sio kwamba wanaenda kwenye hizo organizations in person. Wewe muhitaji ni bora kuwekeza nguvu nyingi kuzitafuta hizo nafasi, ukikpata ndo mshauriane na mtu wako wa karibu aliyeko huko. Hao diaspora wana majukumu mengine hawawezi kuacha majukumu yao na kushinda online siku nzima kukutafutia internships na kazi. Tujiongeze hapa tuache uzembe na lawama za reja reja.

Hakuna mtu anaogopa kuwapa muongozo ila you're asking way too much hata kwa mambo yaliyo ndani ya uwezo wenu. Mimi sina muda wa kumtafutia mtu chuo, passport au internship huo muda sina kabisa Ila akipata nitamsaidia all the way through ndo maana nilisema lazima ucheze part yako as well hakuna mtu ataacha majukumu yake kukusaidia wewe kila kitu.

Connection inayotakiwa ni wewe akija umpe hifadhi naumsaidie kutafuta kazi na apate viza ya mda mrefu aachane na mambo ya kurenuew viza kila wakati

Sasa nyie mnamwambia tu nauli mpaka Marekani ni million Tatu basi, sasa kujua bei ya nauli ni connection? Acheni uhuni bhana mna Roho mbaya tu

Hifadhi, kazi, viza ya muda mrefu ni hadi ufike nchi husika. You will cross that bridge when you get to it. Step 1 ni kupata visa ya kwenda, kama huna uhakika wa visa ya kwenda kwanini uanzie kuumiza kichwa kwa mambo ya mbele?

Ukifika swala la visa ya muda mrefu ni kupewa the right information tu actions zote ni juu yako. Diaspora hawatoi visa au work permit wao, hakuna sababu ya kunyimwa information.

Kuhusu hifadhi sijawahi kusikia mtu kafika kakosa hifadhi, watu wanafika kila siku wanapewa hifadhi na watu baki kabisa na maisha yanaendelea.

Hizi lawama zenu hazina msingi wowote ni lazima ujisaidie kwanza ili usaidiwe. Hii mentality ya kwamba diaspora watakufanyia kila kitu ni ujinga.

Mkuu kuna watu ni walalamishi ajabu! wakiona unafanya mipango ya kutoka ndio hao hao wanaanza kukukatisha tamaa.
Ukitoka wanageuka kuanza kukuomba connection. Mfano mzuri ni mimi, ni juzi tu niliandika nyuzi humu kuhusiana na safari yangu ya Marekani.
Lakini ukilinganisha negative comments na positive, negative ni nyingi zaidi. Kama hiyo haitoshi mbali na yote nimepambana kivyangu (kipesa) hadi kufika.
Sikuwahi kumuomba mwanajukwaa yeyote humu hata senti 5, ikiwa naongopa ajitokeze yeyote niliemuomba na sikuwa na kitu kabisa.
Kikubwa sana ambacho nashukuru ni kuwa watu walinisaidia sana hasa ushauri wewe ukiwa mmoja wao.
Lakini baada ya kuwa nimefika huku umegeuka msaada mkubwa kupita maelezo kwangu, umekuwa zaidi ya ndugu, ninapokwama unanisaidia sana hadi nimewahi kuweka thread humu.
Ajabu mbali na yote niliyoandika kuna watu wananifata DM wananiuliza ulifikaje huko,ukiwaambia wasome nilichoandika tangu naanza harakati hadi nafika hawarudi tena.
Ushauri, ndugu zangu kama wewe ni kijana una ndogo za kufika nje, fanya commitment mwenyewe, utasaidiwa ikiwa unaonyesha juhudi na nia ya unachokipigania mbali na hapo ni ngumu sana.
Jikusanye taratibu tu ila kwa akili sana na mipango madhubuti, fanya mambo yako mwenyewe bila msaada wa agents bila hivyo utatapeliwa na kuishia kukata tamaa.
Ukifika nje amin utasaidiwa tu, mimi ni shahidi wa haya, Bufa amenisaidia sana, Mungu ambariki sana.

Labda nitoe sources zangu haswa kwa agricultural stream
  1. Kuna CAEP
  2. Kuna waTz wanajiita Universal Career Development Pivot
  3. Kuna Bixter.Training
  4. WISE foundation
Hao ni kama madalali, makampuni, recruiters, nk ama vyovyote unavyoweza kuwaita.... Wanaotafuta kampuni zinazokuwa na nafasi kwa ajili ya kwenda kupata training/internship. Kikawaida utaenda kwa ajili ya hizo internship kupitia J-1 Visa. Nina marafiki walioenda kupitia kampuni zote hapo, binafsi nipo kwny process ila mambo ni kupambana. Kama kuna fursa tushirikishane.

Watanzania lazima tujifunze kuambiana ukweli, kuukubali ukweli hata kama ni mchungu vipi, na kuufanyia kazi ukweli kupata matokeo mazuri.

Sad fact: Nchi za watu hazimtaki kila mtu kutoka huku swekeni kwetu you know! Kwasababu hazimtaki kila mtu lazima ujipangie mpango wa muda mrefu wa kukubaliwa. Kama mpango ni shule/kazi/matembezi lazima ujitahidi kuwa eligible, kama hauko eligible leo jiandae hata kwa miaka mitatu mbele uweze kutimiza vigezo na masharti, baada ya kuvitimiza unaweza kuomba viza mwenyewe kabisa bila hata kuasaidiwa na mtu.

Mnawapraise wakenya na wanaijeria bila kujua kuwa wao kama jamii huwa wanapanga mipango ya muda mrefu kuhamia nchi zilizoendelea, mathalani wanaambizana course za kusoma, experience za kutafuta hata kupata ufaulu mzuri ili kuqualify kwenye scholarships na pia kujiandaa financially.

Sisi sasa hahaha! Ufaulu kizungumkuti, course tulizosoma majanga, vibubu havina mia, experience ya kazi vichekesho, nani atakutaka nchini kwake?
 
Naandika huu uzi baada ya kusoma na kusikia mara kadhaa kwamba diaspora wabongo hawatoi connection za kwenda nje compared to diaspora wa nchi kama Kenya, Nigeria nk. Mimi kama diaspora napinga hii notion vikali.
Yawezekana uko sahihi mkuu labda sisi ndio tuna exaggerate mambo, labda connection ni nauli tu kuna diaspora tumesoma nae nilimuulizia whatsap kila kitu ananiambia nicheki website ya nchi husika sikuona hata maana ya kumtafta.
 
Connection inayotakiwa ni wewe akija umpe hifadhi naumsaidie kutafuta kazi na apate viza ya mda mrefu aachane na mambo ya kurenuew viza kila wakati

Sasa nyie mnamwambia tu nauli mpaka Marekani ni million Tatu basi, sasa kujua bei ya nauli ni connection? Acheni uhuni bhana mna Roho mbaya tu

Sisi tumesaidiwa, tunasaidia na watu wanaendelea kusaidiwa. Nani aliyefika hakupewa msaada unless alikua na mambo ya hovyo. Kuna mambo watu mnajiongelea tu au mnataka tukisaidiana tuwe tunapost?
 
Connection inayotakiwa ni wewe akija umpe hifadhi naumsaidie kutafuta kazi na apate viza ya mda mrefu aachane na mambo ya kurenuew viza kila wakati

Sasa nyie mnamwambia tu nauli mpaka Marekani ni million Tatu basi, sasa kujua bei ya nauli ni connection? Acheni uhuni bhana mna Roho mbaya tu
Japo sikubaliani na wewe kutaka kuwa mwanamke kwa hili nakubaliana na wewe
Hawa wadau wangekuwa wanatoa maelezo ya kina, hizi habari za visa passport kila mtu anaye taka kwenda mbele anazijua
 
Naandika huu uzi baada ya kusoma na kusikia mara kadhaa kwamba diaspora wabongo hawatoi connection za kwenda nje compared to diaspora wa nchi kama Kenya, Nigeria nk. Mimi kama diaspora napinga hii notion vikali.

Hapa JF Kuna nyuzi zaidi ya 100 zinazojadili jinsi ya kwenda nje, a quick search mtu unapata majibu yote na bado watu tunachangia nyuzi kila leo. Mnataka connection gani zaidi?

EBM anatoa free knowledge on YouTube na bloggers wengine jinsi ya kwenda nje, hiyo sio connection? Tuwape bundle za kuingia youtube au?

Mimi binafsi nimeshirikiana na watu kadhaa toka kwenye forum hii hii toka walipoanza harakati zao za kwenda nje na sasa wapo mbele needless to say walifanya sehemu zao na mambo yao yakafanikiwa. Sasa urafiki umekua undugu. Tatizo ndugu zangu wamatumbi mnapotaka connection mnataka hao diaspora wawape hadi hela na passport wawatafutie. You have to play your part as well.

Kimsingi kwenda nje is as easy as ABC. Kupata connection ni vizuri but isn't everything. Mimi nilienda bila connection yeyote ile, maelezo yote yapo kwenye websites za nchi husika ila ni lazima uwe tayari kufanya sehemu yako pia, kuna watu wanadhani diaspora wana a magic code ya kwenda nje this couldn't be further from the truth. Ni lazima uwe tayari kufanya sehemu yako.

Wabongo wenzangu punguzeni kulalamika kiboya, JF Kuna more than 100 threads, YouTube ipo, website za nchi husika zipo, tunajitoa as much as we can but we can only do so much. Maisha yako ni jukumu lako, kusaidiana kupo ila sio wajibu.

Nipo around mazee.

Umefanya utafiti wa kutosha? Ina maana hata nabii Lema?
 
Mkuu, tatizo watu wakisikia connection wanadhani kutafutiwa ajira, kupewa pesa ya nauli, na mahala pa kufikia.

Wabongo wengi wanapenda kitonga.

Ajira utapata ukifika nchi husika.

Pesa ni yako, diaspora nao wana majukumu yao.

Mahala pa kufikia huwezi kosa anza harakati za visa utapata tu, tumehost watu baki kabisa.
 
Connection inayotakiwa ni wewe akija umpe hifadhi naumsaidie kutafuta kazi na apate viza ya mda mrefu aachane na mambo ya kurenuew viza kila wakati

Sasa nyie mnamwambia tu nauli mpaka Marekani ni million Tatu basi, sasa kujua bei ya nauli ni connection? Acheni uhuni bhana mna Roho mbaya tu

Ajira, hifadhi na karatasi ni hadi ufike nchi husika. Unawaza ajira hata visa huna, hiyo akili au matope?

Narudia, tumesaidiwa, tunasaidia na watu wanaendelea kusaidiwa.

Anza step 1 step 10 utafika tu. You will cross that bridge when you get to it.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom