Diaspora tumesahaulika Awamu hii ya 5

Diaspora tumesahaulika Awamu hii ya 5

Diaspora ni jipu la kutumbua pia maana wengi wenu hamjitambui mnataka nini!! leo hii mnalia lia kukosa uteuzi serikalini? kwa lipi mlichofanyia Tanzania? mmeshindwa hata kuwapa vijana wetu michongo ya scholarships huko ughaibuni mnataka tuwaamini kwenye ngazi ya uwaziri?

Kwani huko nje mliwapeleka nyinyi? Mliwasaidia michongo ya viza na tickets?
 
Diaspora inatakiwa kugawanywa mara mbili. Moja ni the REAL diaspora na nyingine FAKE diaspora.

The real diaspora ni ya wale waTZ walioondoka nchini, wakasoma course ambazo kwa udogo wa uchumi wetu hatukuweza kutumia taaluma zao kiufasaha, hivyo ikabidi waendelee kukaa huko ili waweze kuendelea ku-practice professions zao. Hawa wamekuwa wataalamu wazuri tu waliobobea kwenye fani ambazo kwa sasa tunazihitaji. Tutawahitaji warudi tuwapige tuition kwanza ili kuwasawazisha na hali halisi ya huku ili wasitupangie mambo mazuri yasiyotekelezeka.

Hii Fake diaspora ni ya wale wasaliti ambao walikimbia na kuitelekeza Tanzania tukiwa tunawahitaji kwa sababu tu waliona sisi tuko nyuma na wao hawawezi tena kuishi maisha haya. Hapa pia kuna wazamiaji haramu waliokwenda kubeba ma-box na kuosha wazee. Pia kuna wale watoto wa vigogo ambao walipewa scholaships zetu wakamaliza masomo lakini wakaamua kwa hiari yao kuzamia ughaibuni.

Kwa sasa tuna Raisi mzalendo, aliyesomea hapa TZ shahada zake zote. Ana imani na wataalamu tulionao humu humu nchini na anaelewa kuwa awamu zilizopita ziliwadharau na kuwanyima fursa za kuchangia taifa either kwa ubaguzi wa kifisadi, nepotism na itikadi za vyama. Tulio humu tunaweza. Tulieni muone ama njooni nyumbani tushiriki pamoja. Usisubiri kuitwa kwani ninyi sio special sana kupita tuliomo humu nchini. Kama ni wazalendo kweli, njooni tushindanie fursa za hapa nchini equally na fairly kwa sheria na masharti sawa. Usitegemee mshahara wa mamilioni kwa sababu tu wewe ni diaspora. Ukipata nafasi "Chapa Kazi". Ukikosa sota na sisi utafute fursa nyingine. Hamkufukuzwa hivyo hamkatazwi kurudi.
 
viongozi wa Awamu hii ya 5 tumewakosea nini sisi Watanzania tunaoishi nje ya nchi (Diaspora)? Tofauti na awamu zilizopita ambapo wana-diaspora walipata Teuzi kwenye baraza la mawaziri (Nyalandu, Membe n.k), na taasisi nyeti serikalini (TTCL & TPDC) mpaka leo zaidi ya siku 100 za awamu ya 5 hakuna mwana-diaspora, kwa nini? sisi tuna uzoefu na exposure ya kutosha kushinda baadhi ya hao #FUKUZAFUKUZATEAM#. Mheshimiwa tupia jicho kwenye dhahabu zilizopo nje ya Tanzania.
Tena nyie hamna maana. Mnataka kutengeneza safari tu. Mkitaka mje huku. Hakuna kuwadekeza. Hatutaki kuwapa watu wanaofikiria kuishi marekani tu. Magufuli hatawadekeza. Kwanza hamlipi kodi huku nyumbani. Mnachuma mnabaki huko huko. Enzi za kuwadekeza nyie zimeisha. Kikwete aliiharibu nchi kwa kutengeneza watembeaji wengi duniani.
 
swali langu ni hili
wamarekani wenye biashara nje ya marekani hawalipi kodi Marekani?

Yes Boss

Kila Mmarekani na Permanent Resident popote walipo duniani kwa majibu wa sheria za Marekani wanatakiwa ku-file taxes zao na kulipa their fair share. Else denounce ur citizenship or ur Residency na uwarudishie kadi au passport ubalozini.
 
Bora hii serikali ya awamu ya 5 iwatupe kule diaspora maana kipindi kilichopita wanawake wa diaspora walikua wanatoa papuchi kwa mtindo wa "buy one get one free" ili wapewe tu post za uDC na nyinginezo huku bongo..yaani wabeba mabox walianza ona kuwa CCM ni deal ...Ngosha tupa kule diaspora, awamu ilopita imevunja sana ndoa za diaspora wadada na wamama walishaona CCM ndo kila kitu basi ni kushinda tu kwenye mikutano ya matawi..hapa kazi tu.
 
Diaspora njooni na vitu vya kuisaidia jamii ya Ki-Tanzania hususani kwenye ELIMU.
 
viongozi wa Awamu hii ya 5 tumewakosea nini sisi Watanzania tunaoishi nje ya nchi (Diaspora)? Tofauti na awamu zilizopita ambapo wana-diaspora walipata Teuzi kwenye baraza la mawaziri (Nyalandu, Membe n.k), na taasisi nyeti serikalini (TTCL & TPDC) mpaka leo zaidi ya siku 100 za awamu ya 5 hakuna mwana-diaspora, kwa nini? sisi tuna uzoefu na exposure ya kutosha kushinda baadhi ya hao #FUKUZAFUKUZATEAM#. Mheshimiwa tupia jicho kwenye dhahabu zilizopo nje ya Tanzania.
Usijali mkuu tumeshasikia kilio chako tutakifanyia kazi kwani inaonesha huu mdororo wa uchumi hata huko ng'ambo maji ya shingo.
 
Biashara gani?

Na kundi gani hasa unalolizungumzia?

Mmarekani anayeishi Tanzania kwa miezi 12 bila kurudi Marekani au Mmarekani anayeishi Marekani lakini mwenye biashara zake nje ya nchi huku makazi yake yakiwa Marekani?
Maswali yako nimeyapenda sana mkuu.
 
Wana diaspora haya nafasi hiyo TIC ipo wazi tumeni CV muitwe kwenye interview (msitegemee direct appointment ) Ili mpambanishwe na mnaowaita WALA VUMBI
 
Ndi ndi ndi! Dayaspora wakati wenu huu sasa kutuma CV ili mpambanishwe na wala Vumbi kwenye ajira ya Boss TIC na nyinginezo.
 
Back
Top Bottom