Bongo kutamu mzee baada ya Bi mkubwa kuchukua kitengo magogoni😂🤣🤣🤣🤣 kidogo kuna ahueni.Nilikua na mpango wa kwenda Chicago kule southside Parkway gardens 6400 blocks (WIIIC City)kwenye zile project now days wanaziita O block nikaanzie aharakati huko ila mwenyeji wangu ambae ni raia wa marekani kanitisha kwa kuniambia ukweli kuhusu gang,s violence eneo analoishi ambalo mimi nitafikia kwake kukaa nikaghairi kwa mda mipango yote mkuu.
27 March 2023
Balozi Tom Amolo azungumzia nafasi za zilizopo za kuingia Germany kufanya kazi mbalimbali pia fursa za elimu ktk nchi hiyo ya ulaya. Balozi amefanya mahojiano ktk video hii kwa lugha sanifu ya kiswahili
Source : Nation
N.B
SERIKALI INA RASILIMALI ZA KUTOSHA KURASIMISHA RAIA KWENDA KUCHUKUA FURSA KIHALALI NJE YA NCHI
Ni mfano mzuri wa serikali kushiriki ktk kuwatafutia raia wake fursa, kuweka makubaliano ya visa, kazi za muda mfupi na mrefu masuala ya wananchi kupata pasipoti, masomo ya lugha za kigeni kuongeza uwezekano wa kupata kazi za aina zote n.k
Nchi kama nchi ya the Philippines 🇵🇭 kwa mfano inatoa uzito unaofaa kwa mafunzo ya somo la ziada kuhusu lugha na tamaduni za nje kupitia vyuo kibao vya kama Ras Simba zinavyoratibiwa kwa karibu ubora wake na serikali ili raia wake wapate ufahamu, connections, network na wepesi wakihitimu vyuo vya VETA, UBAHARIA, UUGUZI n.k moja kwa moja wanakwenda nchi za Ulaya, Canada, Mashariki ya Kati na Australia kufanya kazi .
Hili suala la huku Tanzania mtu mmoja mmoja ktk diaspora kubebeshwa zigo la lawama wakati ilitakiwa serikali ya Tanzania iwe mstari wa mbele kuweka mazingira mazuri mikataba mizuri baina ya nchi na vyuo vyote kuwekewa
mtaala wa somo la lugha za kigeni na tamaduni za nje ili wahitimu wa Welding, makenika useremala udereva VETA, MUCHAS, UDSM, SAUT n.k wawe tayari kutimkia ngambo wakiwa wanajiamini kunyakua fursa.
Connection wanazotoa wakenya, wanigeria, waghana etc ni hizi hizi mnazosaidiwa hapa ila wabongo wavivu wa kufikiri na matendo pia, wanapenda kulia lia na kulalamika tu. Sasa mnataka wabongo wawalishe kwa vijiko mle na kumeza mtataka kusaidiwa na kunya sasa. Wakenya akili zao sio kama hizi za wabongo wao wako sharp kujiongeza. Kuna thread humu zaidi 100 kuhusu haya haya ya connection na diaspora, sasa kama zote hizo hazijakusaidia wewe hupaswi kwenda mamtoni kaa huko huko upambane na tozo... bila akili huku mamtoni hauishi pia utabaki kulalamika hukuhifadhiwa kwiiikwiikwiii
Green card sio connection ujinga mtupu ilr ni bahati nasibu
Wakenya connection wanapeana ni kuambiana hapa kuna kazi moja mbili tatu kuipata fanya moja mbili tatu au kuna chio kinatoa scholarship huku.ugenini au kusoma bure fanya moja mbili tatu
Green lottery unaita connection shame on you
Naijua vizuri sana kupata Green si rahisi sababu ni bahati nasibu na ukipata bado unahitaji connection kuwa hata uwe na pesa za tiketi bado utahitaji host wa kuku host na kukupa connection za ukifika USA kazi utapata wapi ,Social Security namba nknk
Ili ukitua tu USA mtu ajue aelekea wapi
Kupewa Green card pekee si kuwa mtu katoka bado ahitaji connection ambazi Diaspora wetu hawataki ku share
Ndugu usijichoshe sana kujibishana na mtu jibu tayari linajulikana wabongo wazinguaji kwenye kutoa connection za majuu kama siyo uchoyo basi tunaogopana labda.
Labda nitoe sources zangu haswa kwa agricultural stream
Hao ni kama madalali, makampuni, recruiters, nk ama vyovyote unavyoweza kuwaita.... Wanaotafuta kampuni zinazokuwa na nafasi kwa ajili ya kwenda kupata training/internship. Kikawaida utaenda kwa ajili ya hizo internship kupitia J-1 Visa. Nina marafiki walioenda kupitia kampuni zote hapo, binafsi nipo kwny process ila mambo ni kupambana. Kama kuna fursa tushirikishane.
- Kuna CAEP
- Kuna waTz wanajiita Universal Career Development Pivot
- Kuna Bixter.Training
- WISE foundation
Mdau huyo mwana wa kuitwa @ Bufa alikuambia uwe shoga ndio uende marekani🤣🤣🤣🤣😂😂😂??????Yeye anakaa state ipi??????? Nitafute nikupe connection za wana wapo Chicago na Huston city Texas wanaweza kukupa maelezo yaliyonyooka mkuu.Usikate tamaa kama ipo basi ipo tu.
Wana wanaishi kininja sometimes😂😂😂 USA sema ukitusua basi umetusua kweli.Lakini serikali ya USA inazingua sana kuhusu kutuma hela nyumbani,process ndeefu sana.
Em niambie zaidi kuhusu NALA, ushawahi itumia?Hizi story mnatoa wapi? Kuna apps zaidi ya 100 za kutuma hela bongo form NALA ya mbongo kabisa, Sendwave, worldremmit, remitly, WE, moneygram, bank2bank (wire transfer). Hamna usumbufu wowote, I wonder hizi story mnazitoaga wapi ndo maana nasema mnasikiliza sana story za vijiweni na hamna uthubutu.
Niko kiwanja tangu 2016 ila nna mpango wa kuhamia kwa Putin.Achana na box la Russia mkuu, njoo kiwanja.
Em niambie zaidi kuhusu NALA, ushawahi itumia?
Process za kujisajili na kutuma hela, rates zao, usalama na kufika kwa wakati..
Ipo vipi
Naenda kwa Putin kucheki warembo wa kirusi.Umemchoka Biden mkuu? Usitukimbie tupambane na huyu mzee mwakani tunambwaga.
Kumbuka Nchi za nje zipo nyinigi ila kiwanja ni kimoja tu duniani 😀
Huko ndiko nina mwenyeji mkuu.Kwani sehemu ya kufikia ni Chicago tu? Ndo maana tunasema wabongo mnawaza step 9 wakati hata step 1 hujapita, wewe pambana na visa sehemu za kufikia sio Chicago tu, USA kubwa sana. Huwezi badili plan yako kisa gang violence in Chicago unless kama hukuwa motivated to begin with.