Wagumu toka sehemu mbalimbali na safari zao kuelekea Marekani ya Kaskazini
Ungana nasi kwa kutazama video hii kufuatilia mguu kwa mguu toka wakiwasili jijini Sao Paolo Brazil wakijifanya raia wa Angola ktk utalii Brazil kisha wanaanza safari kwenda Canada.
Safari hii ya Wakongomani toka Congo wanaoingia Brazil bila viza kisha wanakutana na wahamiaji wengine toka nchi za China, Morocco, Mali, Senegal, Somalia, Nepal, Nigeria and Bangladeshi kwa miezi mitano wanakatiza mito misitu na barabara ktk nchi kumi za bara la Marekani ya Kusini kabla ya kuingia Marekani nia ni kufika nchini Canada.
Safari hii ya kilometa 20,000 wanakutana wa wahamiaji wengine toka nchi za Caribbean na Latino America ambao pia lengo lao ni kufika Marekani na Canada. Wakongomani lengo ni kufika jimbo la Quebec Canada linalotumia lugha ya Kifaransa kama Congo.
Safari hii inajumuisha kutembea kwa miguu, kupanda basi, taxi, punda, boti , ngalawa na kushirikisha wenyeji wa nchi hizo za Latin America ktk kuonesha njia za vichochoro vijijini zisizo ktk ramani za GPS maana wahamiaji wanatumia simu janja smart phone kutafuta welekeo kupuguza malipo kwa wavushaji watu kwa magendo pale inapowezekana.
Njiani katika njia za panya zilizobatizwa "Njia ya Kuzimu" kukwepa askari wa uhamiaji, kunaonekana utelezi utokanao na mvua zisizokoma za misitu minene ya tropiki, matope yafikayo ugokoni, makaburi yasiyo na jina wala alama za imani zao kwani hao wahamiaji waliopoteza maisha na sasa wamelala udongoni hata kaburini utambulisho wao haujulikani.
Nchi nyingi kama Colombia, Ecuador na Panama wameongeza vikwazo ktk vituo vya mipaka rasmi kutokana na mbinyo toka serikali ya Marekani. Hivyo wahamiaji na watu wote wanaojihusisha na biashara ya kusafirisha watu hutumia njia za vichochoroni kukwepa askari hao.
Pamoja na hayo bado kuna ongozeko kubwa la wahamiaji wanaoelekea Marekani ya Kaskazini wakiwa na imani ya kutafuta fursa na maisha bora zaidi. Wenyeji wa vijiji vya ndani ndani Colombia na Ecuador wanashangazwa na ari bila kusahau hamasa ya kusonga mbele ya hawa wageni toka nchi za mbali.
Watu watajiuliza unawezaje kukatiza nchi zaidi ya 10 salama bila kudhuriwa na wenyeji au magenge ya kutorosha watu mipakani.
Sababu ni kuwa hii ni biashara kubwa inayoingiza kipato na makundi ya waliokuwa wanasafirisha madawa ya kulevya sasa wamejiingiza ktk biashara hii ya kusafirisha watu. Hivyo wakubwa wa magenge haya hawataki kusikia mtu kakabwa au kina mama kubaka n.k na kuwataka wote wanaojihusisha na biashara hii ya kuvusha watu kimagendo mipakani kuwalipa 'kodi' ma drug lords na pia kuhakikisha wageni hao wanamaliza safari salama ili njia zao ziendelee kuaminiwa na maelfu ya wageni hawa waendao Marekani ya Kaskazini. Yeyote atakaye mdhuru mgeni huadhibiwa kwa adhabu kali na wababe hawa wa biashara hii ya kusafirisha wageni.
Endelea kusoma:
Source: France 24
Ungana nasi kwa kutazama video hii kufuatilia mguu kwa mguu toka wakiwasili jijini Sao Paolo Brazil wakijifanya raia wa Angola ktk utalii Brazil kisha wanaanza safari kwenda Canada. Safari hii ya 'Wakongomani' toka Congo na nchi za Maziwa Makuu pia Afrika ya Mashariki wanaoingia Brazil bila...
www.jamiiforums.com