Diamond sasa kuimba taarabu

Diamond sasa kuimba taarabu

Gumzo

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2012
Posts
211
Reaction score
9
BAADA ya kutamba kwa muda mrefu katika muziki wa kizazi kipya nchini, msanii nyota wa muziki huo, Naseeb Abdul ‘Diamond' amesema anafikiria kujitosa katika muziki wa taarab.


Diamond alisema Jijini Dar es Salaam wiki hii kuwa,amefikia uamuzi huo kutokana na kuvutiwa na muziki huo wa taarab. Mshindi huyo wa tuzo mbalimbali za muziki za Kilimanjaro amesema, anajua uamuzi wake huo utawashangaza mashabiki wengi, lakini ni jambo la kawaida kwa msanii.

Diamond alisema hadi sasa anaamini hana mpinzani katika muziki wa kizazi kipya na hakuna msanii anayeweza kufikia kiwango chake hapa nchini.

Diamond alisema ameamua kupiga miondoko tofauti ya muziki kutokana na kipaji alichonacho katika fani hiyo, ambayo imempatia umaarufu mkubwa, Kutokana na kipaji chake hicho,Diamond alisema hakuna kitu anachoshindwa kukifanya katika fani ya muziki.

"Nashukuru mungu kwa kipaji, nahisi naweza kufanya aina yoyote ya muziki, nitajaribu kwa kuwa nia yangu ni kufanya zaidi aya kile nilichofanya sasa" alisema

Alisema bado hajaanza rasmi kupiga muziki wa taarab,na kuwa sasa anafanya tathmini ya soko la muziki huo ili kuona kama unaweza kumletea mafanikio kama ilivyo kwa muziki wa bongo fleva.

Alisema anaweza kufanya kila aina ya muziki kwa sababu anakipaji cha kuimba nyimbo aina zote, hivyo endapo atafikia muafaka anaweza kufanya muziki wa taarabu.
 
mwenzie chid Benz alianza hivyohivyo kaishia kutoboa pua!!!!! Maumivu ya kichwa huanza polepole
 
Mamaaaaaaaaaaa.....anaenda Kufa huko na wala hawatampenda tena. Mwanza,Dodoma n.k hakuna taarabu

KWA TAARIFA DIAMOND MGONJWA AMELAZWA HOSPITAL kwa kubanwa na Kifua

268238_253107908140167_1764971929_n.jpg
 
Tatizo hawa wana mziku wanatatizo moja wanakuwa na watu wenyepesa na wanwafanyia kitu mbaya yani..(Mamula)Mfano ni Mr.Nice mareh allahbuu...wanawatigolies..mwishowe unasikia kaisha utamu!!arrgh!
 
Mamaaaaaaaaaaa.....anaenda Kufa huko na wala hawatampenda tena. Mwanza,Dodoma n.k hakuna taarabu

KWA TAARIFA DIAMOND MGONJWA AMELAZWA HOSPITAL kwa kubanwa na Kifua

268238_253107908140167_1764971929_n.jpg

these hoaxes nowadays leave someone spoofed. Mlianza na Eid Murphy, kisha Meles zinawi na sasa alimas platnum?!
 
Tatizo hawa wana mziku wanatatizo moja wanakuwa na watu wenyepesa na wanwafanyia kitu mbaya yani..(Mamula)Mfano ni Mr.Nice mareh allahbuu...wanawatigolies..mwishowe unasikia kaisha utamu!!arrgh!

Mkuu hii kitu mmmh! Kwahiyo inamaana jamaa wanapumuliwa visogoni? Tafadhali bwana.
 
Back
Top Bottom