Diamond Platnumz na WCB kiujumla mnatukosea

kombaME

JF-Expert Member
Aug 24, 2015
1,777
2,000
Nyie watu mnatukosea sana, mmeamua kabisa kuyachosha masikio yetu, hadhi ya Diamond na Wasafi kwasasa ni kubwa sana, kwasasa mpo kwenye wakati wa kutengeneza uniqueness yenye hadhi ya juu, kwanini mnatufanyia hivi??

Hapa katikati mmeanza kutoa nyimbo ambazo hazieleweki, mnapayuka payuka tu mwanzo hadi mwisho halafu mnapeleka youtube then mnatuambia twende tukasikilize, kweli? Masikio yetu yamewakosea nin nyie watu? WCB siku hizi hamtungi kabisa nyimbo, hakuna ubunifu wowote wa kiuwanamuziki kwenye nyimbo zenu, mmeshajiamini sana kiasi cha kuona mnaweza kufanya chochote mnachotaka, Sio Sawa.

Mziki wenu mnatoa leo baada ya wiki umeisha kabisa nguvu yake na wala hausikiliziki tena, hauwezi kukugusa kwa namna yoyote na katika mazingira yoyote, sasa mziki gani huo? Mnatukosea sana nyie watu

Hebu jifunzeni kwa makundi yaliyokuwa serious na muziki, nyimbo zina miaka hadi 20 lakini ikipigwa inakupa ahueni na kuupooza moyo, muziki ni dawa, nyinyi mnatupa sumu, sikilizeni nyimbo za R Kelly, Westlife, Boys2men n.k... ni kitambo mno lakini hadi leo zinaishi mioyoni mwetu.

Tafadhalini, umizen vichwa, kaeni chini mtunge nyimbo na sio kutafuta kaneno kamoja unakataja taja hako tu nyimbo nzima, mnatukosea.
 

Boeing 757

JF-Expert Member
May 18, 2020
270
500
Dah hongera kwa kuwa na ustahimilivu wa kusikiliza ngoma zao. Hawa jamaa kiukweli nyimbo zao sizielewagi maana hazizungumzii dhamira ya mapenzi kama hisia za upendo na kujali, bali zina central theme ya kuhamasisha ngono mwanzo mwisho. Nyingine zimeenda mbali kuhamasisha na kutukuza kushiriki ngono kinyume na maumbile. Nyimbo zao na baadhi ya bongofleva zina mchukulia mwanamke kama sex object ambaye she always needs to be fuc**d Muda wowote

Sawa hata kama wanaimba kile jamii inataka lakini wamezidisha sana kiasi kwamba mmomonyoko wa maadili unanitafuna jamii haswa ya vijana na mabinti.

Mnisamehe kwa haya nlioyasema ila ndio ukweli wa mambo, na uhalisia uliopo.
 

cocastic

JF-Expert Member
Nov 30, 2019
6,700
2,000
subir team domokaya waje, maan hawapendi kusikia hiki kitu, uwiiiiiiiiiiiih
 

Asksr

Senior Member
Jun 12, 2019
169
500
Ngoma ni kali. nenda kwenye instagram ya mondi ukaone maandalizi ya video utakuja kufuta kauli yako hapa.

"But not every thing is for everybody"
So siwezi nikakupinga
 

Darmian

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
8,447
2,000
Dah hongera kwa kuwa na ustahimilivu wa kusikiliza ngoma zao. Hawa jamaa kiukweli nyimbo zao sizielewagi maana hazizungumzii dhamira ya mapenzi kama hisia za upendo na kujali, bali zina central theme ya kuhamasisha ngono mwanzo mwisho.nyingine zimeenda mbali kuhamasisha na kutukuza kushiriki ngono kinyume na maumbile.nyimbo zao na baadhi ya bongofleva zina mchukulia mwanamke kama sex object ambaye she always needs to be fuc**d Muda wowote .
Sawa hata kama wanaimba kile jamii inataka lakini wamezidisha sana kiasi kwamba mmomonyoko wa maadili unanitafuna jamii haswa ya vijana na mabinti.
Mnisamehe kwa haya nlioyasema ila ndio ukweli wa mambo, na uhalisia uliopo.
Muziki wa hawa jamaa unakera masikioni..na wasanii wengine uchwara nao wanawaiga

Cha msingi ni kutokuwasikiliza kama huwaelewi
 

Asksr

Senior Member
Jun 12, 2019
169
500
not every thing for everybody
Mkuu. Hawafanyi kazi kukufurahisha wewe bali hadhira yao.
Kama nyimbo zinapotea baada ya wiki,kwa nini wao ndo wanaongoza kwa streams katika digital platforms hapa bongo???
Hii ni sawa na mashabiki wa tim fulani hivi. Utasikia eti nyimbo zake haziishi utamu halafu wamezitelekeza mitandaoni huko sijui wanasikiliziaga offline?????
Sio kila kitu kipo kwa ajili yako mkuu. we komaa tu na kina r Kelly hao otherwise utajitesa bure.
 

supe 88

Member
Feb 26, 2020
22
75
tumpe mda na yeye atapita ila historia yake itakuwa hivi DAIMOND NDIO MSANII ALIEWEZA KUTOA NYIMBO ZINAZOPOTEZA RADHA NDANI YA WIKI kwahy mtoa mada hakuna namna tumuache
 

venance7

JF-Expert Member
May 15, 2019
325
1,000
Sijui jamaa wameeidhika au vipi Ila kiukweli sikuhizi wanatoa nyimbo mbovu sana, hapa nauweka u-wcb pembeni, kwa hadhi ya Diamond hastahili kutoa nyimbo za aina hii
 

Kigoma Independent

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
1,819
2,000
Kwanza kabisa WCB sio kundi, Bali ni record label, Halafu kuhusu kukukosea ni wewe na sio wote na kwangu nyimbo zao Zina dumu Sana au una changanywa na hayo makundi ya kizungu kwasababu ya lugha ya kigeni wakati wazungu wenyewe wanazichoka, so calm down dawa ikuingie AMABOKO/AMABHOKO = Mikono iko number moja trending youtube na nia audio tu ,so subiri video in 24 houre 1m viewers ndo utajua watu hawachoshwi masikio yao
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom