Diamond Platnumz atahamia Yanga?

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,422
21,115
Msanii Diamond Platnumz aliweka wazi kuwa alianza kushabikia mpira na kuishabikia timu ya Simba mara baada ya kupata hamasa kutoka kwa swahiba wake Haji Manara.

Kama hiyo haitoshi ,Diamond alilaani sana kipindi ambacho mabosi wa Simba walipoanza kumtolea maneno machafu Haji Manara na alipoonesha yupo upande wa Haji viongozi wa Simba walimfungia vioo na kumblock kabisa Diamond huko kwenye kurasa zao za Instagram.

Sasa je, Diamond ataendelea kuishabikia Simba au atamfuata swahiba wake Haji kuja timu ya Wananchi Dar Es Salaam Young Africans??

Bila shaka Diamond akihamia Yanga, yule chawa Dulla Makabila bila shaka na yeye atarudi Yanga maana alihama Yanga kwenda Simba kumfuata Diamond Platnumz.
 
FB_IMG_16288628998089902.jpg
 
Suala la Simba na Yanga lipo wazi sana na hesabu zinatabirika. Kama Diamond ni Simba damu atabaki kuwa mnyama tu japo Manara kaenda Yanga. Na iwapo Diamond ni Yanga damu ataenda Yanga. Simba na Yanga ni zaidi ya dini mkuu kwani dini watu huwa wanabadilisha. Simba na Yanga kidogo inaendana na makabila kwani watu huwa hawabadilishi makabila yao lije jua au mvua inyeshe. Ukiona mtu anakuambiwa mimi ni Simba lakini kwa kuwa wameniudhi naenda Yanga jua kabisa huyo ni Yanga toka zamani. Na hata mtu akikwambia mimi Yanga lakini timu haichukui makombe nahamia Simba jua huyo Simba toka zamani.
 
Msanii Diamond Platnumz aliweka wazi kuwa alianza kushabikia mpira na kuishabikia timu ya Simba mara baada ya kupata hamasa kutoka kwa swahiba wake Haji Manara.

Kama hiyo haitoshi ,Diamond alilaani sana kipindi ambacho mabosi wa Simba walipoanza kumtolea maneno machafu Haji Manara na alipoonesha yupo upande wa Haji viongozi wa Simba walimfungia vioo na kumblock kabisa Diamond huko kwenye kurasa zao za Instagram.

Sasa je, Diamond ataendelea kuishabikia Simba au atamfuata swahiba wake Haji kuja timu ya Wananchi Dar Es Salaam Young Africans??

Bila shaka Diamond akihamia Yanga, yule chawa Dulla Makabila bila shaka na yeye atarudi Yanga maana alihama Yanga kwenda Simba kumfuata Diamond Platnumz.
Yametimia.
 
Back
Top Bottom