Diamond ni mchawi, achaneni naye!

Sumbi Sanchez

Member
Apr 16, 2017
45
172
Diamond ana sauti mbaya. Vocal bwana anazo King Kiba na ana kipaji zaidi cha kutengeneza muziki mzuri kuliko Diamond. Nyimbo za Diamond ni mbaya na hazipendezi masikioni.

Baada ya yeye kutoa ngoma mbovu hapo juzi aliyoiita 'Baba Lao' ambayo haina chochote cha maana kimuziki zaidi ya kelele zisizotoa msisimko wowote Ali Kiba alifuata na ngoma kali mno inayokwenda kwa jina la 'Mshumaa'. Barnabas, Ommy Dimpoz, Aslay na wataalamu wengine wa masauti na muziki kwa ujumla wameusifu na kuupromote sana wimbo wa King Kiba kuwa ni moto wa kuotea mbali.

Lakini mbaka sasa wimbo mbaya wa Diamond umekwenda zaidi YouTube. Upo namba moja kwenye trending na tayari una views zaidi ya 2M wakati hata ngoma kali zaidi 'Uno' ya Harmonize iliyotoka siku zaidi ya nne kabla ya wimbo wa Diamond haujafika idadi hiyo ya views. Oh sorry nilisahau. Hizi views huwa ananunua. Halafu wala sio kigezo cha kupimia mafanikio ya wimbo.

Lakini waliotazama Wasafi Festival waliona namna Diamond alivyoweza kuwapagawisha washabiki waliofurika viwanja vya Posta Kijitonyama kwa kutumia wimbo wake mbaya.

Kiuhalisia hakuna msanii yeyote aliyeamsha shangwe kumzidi yeye ingawa kulikuwa na Wizkid ambaye ana umaarufu mkubwa zaidi.

Sasa Diamond anawezaje kupendwa na washabiki wengi kiasi hiki wakati uwezo wake wa kimuziki ni mdogo mno? Hata yeye mwenyewe aliwahi kusema kuwa wapo wasanii wengi mno, na wengine hata hawajatoka na hawajulikani na wana uwezo wa kuimba kuliko yeye.

Hapa Diamond alifanya vyema sana kukiri kuwa kipaji chake cha muziki ni cha kawaida mno ukilinganisha na watu waliojaliwa sauti na ujuzi wa muziki.

Unapojaribu kufikiri kuhusu hao wenye vipaji zaidi ya Diamond lisikujie jina la Ali Kiba peke yake kwenye kichwa chako kwa sababu unazozijua mwenyewe.

Ali Kiba ana sauti kuliko Diamond. Lakini hana uwezo wa sauti kumzidi Ibra Nation, Beka Ibrozama, Ben Pol n.k.

Hata huko majuu Justin Bieber ni star na anapendwa zaidi kuliko watu wenye uwezo wa sauti na muziki kwa ujumla kumzidi yeye. Kisauti Justin Timberlake, Adam Levine na wakali wengine wako juu zaidi yake lakini sokoni amewaacha mbali mno.

Kwa hiyo ni wazi kuwa sauti pekee haitoshi. Ni lazima uwe mbunifu kwenye muziki na maisha yako nje ya muziki ili uwe na soko zaidi. Zaidi ya hapo unatakiwa kuwa na mbinu mbadala za kuutangaza muziki wako.

Vinginevyo utaishia kusifiwa tu wakati wabunifu wanaendelea kukuacha mbali kwa mafanikio na umaarufu.

Sasa majaribio ya kuwashawishi watu kuwa eti Diamond hajui kuimba na kuna wakali zaidi yake kwenye swala la muziki kwa lengo la kumshusha hayana maana.

Hao wenye vocal na mashairi mazuri watu wanawafahamu lakini macho yote yapo Kwa Diamond na wengine wenye uwezo wa kawaida kimuziki. Wamiliki wa makampuni ya Pepsi, Parimatch, Niceone na wengine wanaomtumia kama balozi wao na kumpatia mpunga wa maana wanajua kuwa nyimbo zake ni mbaya.

Hata Vodacom, Coca-Cola na wengine waliowahi kumpa dili nono miaka ya nyuma nao wanafahamu kuwa Ibra Nation, Barnabas, Ben Pol, Beka Ibrozama, Christian Bella, Ali Kiba, Ommy Dimpoz, Mario, Aslay na wengine wana sauti nzuri zaidi ya Diamond na wana nyimbo nzuri zaidi ya zile zake.

Lakini dili wanampa Diamond kwa sababu ndiye ambaye muziki wake na habari za maisha yake binafsi ni dili kuliko kiumbe chochote Afrika Mashariki na Kati.

Hata wasiompenda Diamond cha ajabu huwa wanampromote mitandaoni. Mara ooh ameiga wimbo wa mtu, mara ngoma yake hii ni mbaya wakati nyimbo mbaya na zinazoibiwa zipo nyingi lakini za kwake huwa zinaongoza kujadiliwa.

Hii yote kwa sababu Diamond ni mchawi. Na uchawi wake ni ubunifu alio nao. Kumchukia Diamond na kutegemea anaweza kushushwa na binadamu ni kujipa maumivu ya kipumbavu.

Mimi nilikataa upumbavu huu miaka mingi mno. Nawasihi na nyinyi pia, achaneni na Diamond. Huyu jamaa ni mchawi.
 
Mziki uliwashinda wasaanii wakongwe kuufanya biashara inayowanufaisha bila kutegemea external forces. Walitengeneza pesa kwa wakati wao ila zilikuwa zinaishia kwa mameneja na ma promoter kwa sababu ya utegemezi wa show tu za kuandaliwa. Na ndiyo maana kelele za unyonyaji zilikuwa nyingi kwa ma managers!

Diamond ndie msanii pekee ambaye ameweza kuizalisha hio force internally bila kutegemea support za hao waliokuwa wanyonyaji mwisho ikabidi waungane nae tu na kukaa kwenye terms zake.

Ameweza kuwa bypass ma meneja na kukamata connections mwenyewe hali iliowafanya jamaa wataharuki maana walitarajia kumzima kama walivyozoea kuwazima wengine ila Mondi akawa kawatangulia kwa mbinu. Katokea mlango wa SociaL Media kujibrand na kwenda mainstream, jamaa walijua atawasujudia kama walivyozoea ila cha ajabu akaunda management na kuwapa kazi ma manager wale wale ambao walikuwa wanawanyonya wasanii wengine ili kujinufaisha zaidi na mziki wake umekuwa ni biashara inayowalipa mno toka kuanza kwa Bongo Flava.

Kiukweli i have no reason to hate on Diamond, zaidi I'm inspired kuwa dogo ameanza kishamba ila ame-grow kuwa mjanja mpaka kuwashangaza moguls wa biashara kubwa hapa nchini. He broke the mold!
 
Nyimbo za Ali Kiba unaweza kuzikiliza ukiwa umekaa na wakwe zako. Hazina matusi anatumia lugha za staha.

Kwasauti Kiba ni Mfalme wa muziki Tanzania.

Ukitaka kumsaidia mtu afanikiwe mpe mfano wa Alikiba na Diamond.

Alikiba ana sauti nzuri anatunga vizuri ila tatizo lake kubwa na linalofanya asifike alipo Diamond ni tabia ya kujiona mfalme, kujiona yeye anapaswa kukimbiliwa, kujiskia na kuvimba.

Diamond sio muandishi mzuri ila anajua kucheza na akili za watu,anaheshimu mashabiki wake, anawalilia na kuwafanya wajione wanamsaidia, ni mnyenyekevu na anatangaza kazi zake kama vile ni msanii chipukizi. Diamond hana kiburi. Watanzania wengi wanapenda kunyenyekewa na ukilijua hilo utawapata sana.
 
images (8).jpeg

Dogo anajituma na anajua industry ya Africa ina taka nini, ya EA inataka nini na ya Bongo ina taka nini.

Diamond ni Mbongo asie kuwa na tabia za Wabongo walio wengi za KUFANYA KAZI KWA MAZOEA.
 
Ukitaka kumsaidia mtu afanikiwe mpe mfano wa Alikiba na Diamond.

Alikiba ana sauti nzuri anatunga vizuri ila tatizo lake kubwa na linalofanya asifike alipo Diamond ni tabia ya kujiona mfalme, kujiona yeye anapaswa kukimbiliwa,kujiskia na kuvimba.

Diamond sio muandishi mzuri ila anajua kucheza na akili za watu,anaheshimu mashabiki wake,anawalilia na kuwafanya wajione wanamsaidia,ni mnyenyekevu na anatangaza kazi zake kama vile ni msanii chipukizi. Diamond hana kiburi.

Watanzania wengi wanapenda kunyenyekewa na ukilijua hilo utawapata sana.​

Napenda kaz za Kiba ila I hate his attitude demeanor and also he got this big ego!

Diamond is still humble person despite his accomplishments.
 
Mziki ni zaidi ya kuwa na sauti nzuri, trend ya mziki wa sasa ni kudance ndiyo maana utasikia nyimbo za Kinaija zinapendwa wakati hakuna chochote walichoimba.

Diamond analijua hilo yuko katika kutengeneza pesa siyo kutafuta sifa naye anakubali kuwa anafanya mziki wa ujanja ujanja.

Utaskia watu wanamlaumu oh kalipia instagram adverts waupromote upate viewers wengi. Uwa nashangaaa kwani tatizo ni nini? Anafanya biashara na biashara matangazo
 
Napenda kaz xa kiba ila i hate his attitude demeanor and also he got this big ego!
Domo is still humble person despite his accomplishments
Kiba anayo nyumba, gari na pesa bank anazo.

Ni kukosea kufikiri kwamba labda bado kuna kitu anatakiwa kutafuta, kama karidhika hivyo ni vyema pia.

Mond yeye still ana kiu ya kuweka rekodi yake peke yake Tanzania au Africa nzima, aungwe mkono kwa hilo, siyo kukunjiana na kuoneana gere na vijembe.
 
Back
Top Bottom