Diamond na Alikiba ndani ya Tangazo la NSSF

Nani kamfunika Mwenzake katika Tangazo hili?

  • Diamond

    Votes: 13 50.0%
  • Ali Kiba

    Votes: 13 50.0%

  • Total voters
    26
  • Poll closed .

Page 94

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
5,204
15,198
Salaam Wakuu.

Wasanii maarufu na wenye mashabiki Lukuki hapa nchini, ambao wamekuwa katika upinzani mzito wamekutanishwa kwenye Tangazo la shirika la mafao la NSSF.
Wasanii hao Nasibu Abdul maarufu "Diamond" na Alli Kiba,wametengeneza mistari yao, Tangazo litaanza kutumika siku si nyingi.

Nyimbo hiyo itatumika katika kulitanganaza na kulinadi Shirika hilo kwa siku zijazo ili lipate wigo mpana na kuzidi kushamiri hapa nchini.

Pamoja na hayo, Ngoma hii ya pamoja inaweza kuwa kipimo sahihi cha nani mkali zaidi ya Mwenzake na kunyamazisha upande Mwingine. Tangazo hilo pia linaweza kumaliza Ubishani wa muda usio na kikomo.

Hebu pata Kionjo na rudi hapa kutufahamisha nani kamfunika mwenzake.
Baada ya hapo utapiga kura moja tu,ili tujue nani ni nani.

NOTE; Huo wimbo uliimbwa na Kigoma All Stars miaka iliyopita.
 
Attachments

  • AUD-20170125-WA0015.mp3
    762 KB · Views: 114
Hebu tuambie Mkuu, nani kamfunika? Au Ali K wako kagaragazwa? Maana ungetoa maoni badala ya kumjibu jamaa, alafu hajamtaja jina. Au umehisi tu....?
Nimedownload attachment ngoja niicheki,hata hivyo sina shaka Ali kafunika kama kawaida.
Diamond kumfunika Ali kwenye kuimba ni ndoto ya mchana.
 
Hii sio jipya,hili tangazo lilitolewa na kigoma all starz,miaka mingi tu iiliyopita,mpaka video yake ipo,wapo wanamzik kibao kina banana,linex,mwasiti,ommy dimpoz,etc etc
 
Flani flani za nini? Mwanaume kuongea lugha za mafumbo ni unaa.
Funguka kiume,mafumbo tuachie wanawake.
Hiyo ya kutumia flan na lugha za mafumbo kuwa unaa ni wapi ilipitishwa rasmi? I mean na kurugenzi ipi hasa?

Kuhusu kufunguka kiume kwani hapa Natongoza?

Hebu jibu hilo la kwanza kisha tuendelee.

Coz huwa nakuheshimu sana na nimeshangaa sana kuniambia hivyo...ilihali wewe si Ali Kiba wala Diamond.
 
Ahaa. Kumbe Mkuu, mi sikua nalijua hili. By the way, Ahsante sana.
Hii sio jipya,hili tangazo lilitolewa na kigoma all starz,miaka mingi tu iiliyopita,mpaka video yake ipo,wapo wanamzik kibao kina banana,linex,mwasiti,ommy dimpoz,etc etc
 
Hiyo ya kutumia flan na lugha za mafumbo kuwa unaa ni wapi ilipitishwa rasmi? I mean na kurugenzi ipi hasa?

Kuhusu kufunguka kiume kwani hapa Natongoza?

Hebu jibu hilo la kwanza kisha tuendelee.

Coz huwa nakuheshimu sana na nimeshangaa sana kuniambia hivyo...ilihali wewe si Ali Kiba wala Diamond.

Azarel tuliza mori bhana,hata mimi huwa nakuheshimu na najua tunaheshimiana ila sio kwamba tusikosoane.

Tunakosoana na mwisho wa siku maisha yanaendelea.

Hata hivyo naona umeshapanic na sikujua kwamba unafiki huwa unapitishwa na kurugenzi.

Kuongelea masuala ya Kiba na Diamond kumbe ni hadi wahusika wenyewe ndio wayaongelee?
Kwa maana hiyo wewe ni mmoja kati yao?
Duh!

Relax...
Cheers
 
Back
Top Bottom