Romy Jones ndani ya bifu zito na Lamata!

Nifah

JF-Expert Member
Feb 12, 2014
31,531
65,303
DJ maarufu nchini, Romeo George ‘Romy Jones’ ameingia katika bifu zito na bosi wake katika tasnia ya filamu mwanamama Leah Mwendamseke ’Lamata’ kwa kile kinachodhaniwa kuwa vita ya kimaslahi.

Wawili hao wamefanya kazi kwa mafanikio katika tamthilia maarufu nchini ya Jua Kali, kabla ya kuibuka kwa majukumu mapya yaliyomzidia Romy Jones kutimiza wajibu wake wa kushiriki katika tamthilia hiyo.

CHANZO NI WASAFI FESTIVAL!
Ikumbukwe kuwa, licha ya Romy Jones kuwa ndugu wa damu wa Diamond Platinumz, ndiye DJ wake rasmi katika kila tamasha la muziki atakaloshiriki.

Hiyo imepelekea Romy Jones kuwa busy kutokana na utitiri wa shows nyingi ndani ya tamasha hilo ambalo Diamond kama muasisi na mmiliki amewekeza nguvu zake nyingi huko kwa kushiriki binafsi katika kila mkoa ambao kuna ratiba ya kufanyika kwa Wasafi Festival.

Romy Jones baada ya kutingwa na matamasha, akakosa kushiriki kwa ukamilifu na pengine kutokushiriki kabisa kwa sehemu kubwa katika tamthilia hiyo.

Kitendo hiki kilimuumiza sana Lamata ambaye ndiye aliyempa nafasi ya kuigiza kwa mara ya kwanza kupitia tamthilia hiyo kubwa na ilikuwa bahati tu kwa mujibu wake mwenyewe Romy Jones kutokana na mahojiano kadhaa aliyowahi kuyafanya juu ya ushiriki wake katika tamthilia hiyo na nyingine za Kiswahili.

Balaa baina yao lilizuka pale Romy Jones alipokwama kwenye mambo yake, huku akitaka kupewa malipo kutoka kwa uongozi wa Jua Kali ambako hakuwa ameonekana katika shooting kadha wa kadha.

Lamata kama bosi wa tamthilia hiyo hivi sasa amepumzika kwa kiasi kikubwa majukumu kutokana na ujauzito wake kufikia ukingoni karibuni na kujifungua, aliingilia kuweka sawa baada ya mzozo mkubwa kuibuka kati ya mhasibu wake na Romy Jones juu ya malipo.

Alimpigia simu RJ na kuzozana nae kwa kumpa ukweli wa mambo jinsi gani anavyokwamisha shooting, na kutoa maagizo RJ atumiwe laki moja katika simu kwa ajili ya mafuta ya gari kwa RJ kisha amfuate Lamata alipo wakajadili kwa kina, na ikiwa ni pamoja na kulipwa stahiki zake zote.

RJ hakukubaliana na hilo, punde laki moja ilipoingia kupitia simu yake na mhasibu kupiga simu kuthibitisha, RJ akagombana na mhasibu kisha akaurudisha muamala.
Yeye RJ alitaka kuongea wayaweke sawa na sivyo Lamata alivyotaka ‘kumalizana’ nae.

Hadi ninavyoandika hapa, kuna uwezekano mkubwa wa Billy Jr. kutokuonekana tena katika tamthilia ya Jua Kali baada ya kuchokwa na kila mmoja hadi wasanii wenzie kwa ‘uzinguaji’ wake.

RJ mwenyewe anahaha huku na huko kuomba kikao na Lamata bila mafanikio…

Ndimi,

Nifah

IMG_4392.jpeg
IMG_4393.jpeg
 
DJ maarufu nchini, Romeo George ‘Romy Jones’ ameingia katika bifu zito na bosi wake katika tasnia ya filamu mwanamama Leah Mwendamseke ’Lamata’ kwa kile kinachodhaniwa kuwa vita ya kimaslahi.

Wawili hao wamefanya kazi kwa mafanikio ktk tamthilia maarufu nchini ya Jua Kali, kabla ya kuibuka kwa majukumu mapya yaliyomzidia Romy Jones kutimiza wajibu wake wa kushiriki ktk tamthilia hiyo.

CHANZO NI WASAFI FESTIVAL!
Ikumbukwe kuwa, licha ya Romy Jones kuwa ndugu wa damu wa Diamond Platinumz, ndiye DJ wake rasmi katika kila tamasha la muziki atakaloshiriki.

Hiyo imepelekea Romy Jones kuwa busy kutokana na utitiri wa shows nyingi ndani ya tamasha hilo ambalo Diamond kama muasisi na mmiliki amewekeza nguvu zake nyingi huko kwa kushiriki binafsi katika kila mkoa ambao kuna ratiba ya kufanyika kwa Wasafi Festival.

Romy Jones baada ya kutingwa na matamasha, akakosa kushiriki kwa ukamilifu na pengine kutokushiriki kabisa kwa sehemu kubwa ktk tamthilia hiyo.

Kitendo hiki kilimuumiza sana Lamata ambaye ndiye aliyempa nafasi ya kuigiza kwa mara ya kwanza kupitia tamthilia hiyo kubwa na ilikuwa bahati tu kwa mujibu wake mwenyewe Romy Jones kutokana na mahojiano kadhaa aliyowahi kuyafanya juu ya ushiriki wake ktk tamthilia hiyo a nyingine za Kiswahili.

Balaa baina yao lilizuka pale Romy Jones alipokwama kwenye mambo yake, huku akitaka kupewa malipo kutoka kwa uongozi wa Jua Kali ambao hakuwa ameonekana katika shooting kadha wa kadha.

Lamata kama bosi wa tamthilia hiyo hivi sasa amepumzika kwa kiasi kikubwa majukumu kutokana na ujauzito wake kufikia ukingoni karibuni na kujifungua, aliingilia kuweka sawa baada ya mzozo mkubwa kuibuka kati ya mhasibu na Romy Jones juu ya malipo.

Alimpigia simu RJ na kuzozana nae kwa kumpa ukweli wa mambo jinsi gani anavyokwamisha shooting, na kutoa maagizo RJ atumiwe laki moja katika simu kwa ajili ya mafuta ya gari kwa RJ kisha amfuate Lamata alipo wakajadili kwa kina, na ikiwa ni pamoja na kulipwa stahiki zake zote.

RJ hakukubaliana na hilo, punde laki moja ilipoingia kupitia simu yake na mhasibu kupiga simu kuthibitisha, RJ akagombana na mhasibu kisha akaurudisha muamala.
Yeye RJ alitaka kuongea wayaweke sawa na sivyo Lamata alivyotaka ‘kumalizana’ nae.

Hadi ninavyoandika hapa, kuna uwezekano mkubwa wa Billy Jr. kutokuonekana tena katika tamthilia ya Jua Kali baada ya kuchokwa na kila mmoja hadi wasanii wenzie kwa ‘uzinguaji’ wake.

RJ mwenyewe anahaha huku na huko kuomba kikao na Lamata bila mafanikio…

Ndimi,

Nifah

View attachment 2844179View attachment 2844182
Kwa lolote lile nasimama upande wa RJ.

RJ ni mtu poa sana.
 
Hivi wale ni ndugu wa damu au cousins tu, by the way kwenye hilo Romy kazingua big time hata Lamata ni mtu poa ndio maana wanamchukulia poa huwezi kujiamulia tu mambo kienyeji kwenye kazi za watu, sasa huko kwenye jua kali wataambia nini wapenzi watazamaji maana kwa sasa wamefanya iwe kama vile Bill Jr kasafiri
 
Yes, ni ndugu wa damu maana walinyonya ziwa moja, na mama zao ni ndugu pia.

Bill anaweza asirudi tena huko safarini mkaletewa muhusika mpya 🤣🤣🤣
Ila mimi huwa namkubali, naangaliaga scene zake pekee mara nyingi.
 
Back
Top Bottom