Diamond kaza uzi Rayyvann anakuja kwa kasi

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,956
22,405
Baba la baba diamond platnumz chibu dangote simba kaza mdogo wangu huyu kijana rayyvann anakuja kwa kasi sana

Ingawa ni kitu kizuri kuona kijana anazidi kufanikiwa tena isitoshe yupo katika lebel yako ila nakusihi mdogo wangu huyu dogo atakuvua nguo huko mbeleni usipokuwa makini utaonekana si chochote mbele yake ,kaza kamba sana toa mawe ya kueleweka zaidi

Kijana kafanya vizuri sana katika ngoma yake ya Sugu nina imani na wewe pia utakuwa hujaniangusha katika ngoma yako na Richard mavoko

Kwa leo yangu ndo hayo tu ni mimi shabiki wako nambari moko peninsula xavier dos santos from mpumalanga
 
Mawazo ya kimasikini, mtu ana uwezo wa kuimba usimsaidie kwa sababu atakupita, upuuzi mtupu na ndio maana platnumz hana hayo mawazo kama yenu na ndio maana anafanikiwa, kwa sababu ya kuwanyanyua wenzake.
 
wapi niliposema asisaidiwe?
Uwe unasoma na kuelewa usikurupuke

Nilichokisema ni kuwa diamond aongeze juhudi zaidi asibweteke na mafanikio yake kwa kuwa atawakosa mashabiki wake kwa kuwa kijana Raymond ameonesha ushindani wa hali ya juu
 
Na ndio maana kamchukua ili afanye muziki mzuri kwa kuwa keshamuona kipaji chake,sasa kama atafikia kumpita boss wake ndio itakuwa kipimo cha jinsi gani HAKUM'BANIA alimuacha huru.
 
Kuna kakabila kamoja hivi.. Mmoja wao akiwa na hela hataki kuwasaidia ndugu zake njia ya kupata kama yeye kwa uoga kwamba watamfikia na watafanana naye..basi yeye hujisikia raha sana kuombwa hela na kuitwa na ndugu kutoa misaada tu..

Hatari inaijiaga familia hiyo mara yule mwenye uwezo anapotwaliwa!
 
Baba la baba diamond platnumz chibu dangote simba kaza mdogo wangu huyu kijana rayyvann anakuja kwa kasi sana

Ingawa ni kitu kizuri kuona kijana anazidi kufanikiwa tena isitoshe yupo katika lebel yako ila nakusihi mdogo wangu huyu dogo atakuvua nguo huko mbeleni usipokuwa makini utaonekana si chochote mbele yake ,kaza kamba sana toa mawe ya kueleweka zaidi

Kijana kafanya vizuri sana katika ngoma yake ya Sugu nina imani na wewe pia utakuwa hujaniangusha katika ngoma yako na Richard mavoko

Kwa leo yangu ndo hayo tu ni mimi shabiki wako nambari moko peninsula xavier dos santos from mpumalanga
Uikumbuke Na ile Remix Ya all The Way Up !
 
Ile sugu kama amefanya just kwa kujifurahisha na vitu ka hizo hapo sawa ila kama ni official track aisee hapana hauwezi kuisukuma ngoma kama ile sema kwa sababu sisi wabongo tumekariri watu wa kuwasapot utashangaa ikiombwa redioni!!! Ila ni ngoma ya kusikiliza geto tu kusogeza muda
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom