Diamond aokolewa na polisi Ujerumani

Diamond aokolewa na polisi Ujerumani

msafwa93

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2011
Posts
4,840
Reaction score
6,148
Usiku wa Jumamosi Agosti 30, 2014, majira ya saa 10 alfajiri, mwanamuziki nyota wa Bongo Flavor, Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart, Ujerumani, baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show.

Sehemu ya ukumbi ulioharibiwa vibaya na washabiki mjini Stuttgart, Ujerumani.

Mashabiki hao waliokuwa wamelipa tiketi euro 25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku, lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa 10 alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anayejiita Britts Event.

Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake, Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya mashabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki, ma-Djs walishambuliwa na wapo hospitalini kwa sasa.

Mmoja wa Djs hao alipoteza lap top yake, mwanadada DJ Flor alipatwa mstuko wa moyo na kukimbizwa hospitali, washabiki hao walimpa kipigo DJ Drazee naye yupo hoi hospitali. Polisi nchini Ujerumani wanamesema tukio hili la aibu halijawahi kutokea, kuwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa Ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa Ujerumani wanaheshimu sana muda wao.

Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema wanachunguza thamani ya hasara iliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promota huyo raia wa Nigeria ambaye pia anachunguzwa kwa kujihusisha na mtandao fulani wa biashara.

KWA JINSI ANAVOPENDA SIFA NAHISI ALITAMANI HATA MTU AFE ILI AZUNGUMZIWE KWENYE MEDIA ZA UJERUMANI..

NA PIA HUO UKUMBI ULIOPO KWENYE picha NDIO ALIOTAKA KUFANYIA SHOW DIAMOND,NI LEVEL ZA UKUMBI WA "HAPPY BIRTHDAY TO YOU"..
 
Attachments

  • IMG-20140901-WA034.jpg
    IMG-20140901-WA034.jpg
    20.4 KB · Views: 1,040
Meneja wa Diamond alimwaminije promota Mnaijeria? Wanaijeria wanaogopwa dunia nzima
kwa kutokuwa waadilifu kwenye business.

Pia ni vizuri sisi kutoka africa tuwe tunaelewa kwamba ulaya wanathamini sana muda; sio kama sisi huku africa -any time is the right time.

Pole zao sana na wajifunze kwenye hiki kisa.
 
Kosa si la diamond Bali n huyo promota mnaijeria na inavyyonekna walikuwa bado hawajapatana malipo coz mnaijeria alitaka leta janja ya nyani
 
Hahaaaaa et ukumbi wa level za happy birthday to you
 
sasa hiyo attachment ya picha si ya ukumbi halisi aliotaka kupiga hiyo show??
kuna haja gani ya kutuwekea hiyo picha ,..?
 
KWA JINSI ANAVOPENDA SIFA NAHISI ALITAMANI HATA MTU AFE ILI AZUNGUMZIWE KWENYE MEDIA ZA UJERUMANI..

NA PIA HUO UKUMBI ULIOPO KWENYE picha NDIO ALIOTAKA KUFANYIA SHOW DIAMOND,NI LEVEL ZA UKUMBI WA "HAPPY BIRTHDAY TO YOU"..
We jamaa na hizo chuki zako kwa Diamond utakuja kupata vidonda vya tumbo!!! Hii habari mbona watu washaijadili sana tu... ipo kila kona!!! Suala la ukumbi, kwani Diamond ndie mwandaaji wa show?? Hivi umeshawahi kuingia Diamond Jubilee? Hii ule ukumbi una sifa ya kuitwa ukumbi wa muziki? Je, kuna wanamuziki wangapi wa nje wamewahi kupiga show mle?? Kwahiyo kama wewe ungekuwa ndo Diamond, cha kwako umeshapewa kama ulivyotaka bado ungekataa kupiga show kwenye hall wakati mwandaaji wa show sio wewe??

Pole wangu... nakumbuka wakati Diamond ameenda BET ulisema ndo mwisho wake lakini ndo kwanza mchizi anaendelea kupiga show... ya nini kujipa pressure na stress??
 
•. •Taswira media•. •
» Taarifa News»

Diamond aokolewa na polisi Ujerumani
about 1 hour ago
Usiku wa Jumamosi Agosti 30, 2014, majira ya saa 10 alfajiri, mwanamuziki nyota wa Bongo Flavor, Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart, Ujerumani, baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show.

Sehemu ya ukumbi ulioharibiwa vibaya na washabiki mjini Stuttgart, Ujerumani.

Mashabiki hao waliokuwa wamelipa tiketi euro 25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku, lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa 10 alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anayejiita Britts Event.

Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake, Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya mashabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki, ma-Djs walishambuliwa na wapo hospitalini kwa sasa.
»Ts media wakai nasa hii»
Mmoja wa Djs hao alipoteza lap top yake, mwanadada DJ Flor alipatwa mstuko wa moyo na kukimbizwa hospitali, washabiki hao walimpa kipigo DJ Drazee naye yupo hoi hospitali. Polisi nchini Ujerumani wanamesema tukio hili la aibu halijawahi kutokea, kuwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa Ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa Ujerumani wanaheshimu sana muda wao.

•Taswira media haikuishia hapo ».

Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema wanachunguza thamani ya hasara iliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promota huyo raia wa Nigeria ambaye pia anachunguzwa kwa kujihusisha na mtandao fulani wa biashara. By. Dr. Ts media
 
Kosa kubwa limefanywa na Diamond mwenyewe kutaka mapromota uchwara na matapeli wa Kinigeria kwa gharama ndogo. Kwa wenzetu muda kwao una thamani. Ukimwambia shoo itaanza saa nne usiku zingatia muda wa kufika ukumbini na kuanza shoo kwa muda mliokubaliana sasa kama alifikiri u super star wa bongo wa kujijia alfajiri badala ya saa nne usiku ungefanya kazi kwa wajali muda alijidanganya. Au walichelewa kwenye majumba ya ngono ya ujerumani? Kama walikuwepo mapromota wajerumani kwa nini alijihangaisha na matapeli ya kinijeria? Hapo ajifunze vinginevyo akienda kuurudia upuuzi kwingine hatatoka ukumbini akiwa mzima.
 
Kwa kifupi mi naona kajiharibia show zingine zote za ulaya na sehem nyingine. Unajua kwa kuwa haoa bongo watu wanamkweza ndio maana anatujia alfajiri. Nakumbuka kuna show alifanya Geita kwa kweli alitudharau vya kutosha kama mashabiki. Ukumbi mbaya, mvua ikatunyeshea na bado alichelewa kuja. Bad enough akaimba nyimbo mbili tatu akatambaa....
Kweli kuchukua promota Nigeria ni kupoteza dira kutokana na sifa za utapeli walizonazo raia wa nchi hiyo....
 
Back
Top Bottom