Diamond ajaza nyomi la watu Zambia

MosiOfThunder kama ambavyo wenyewe wa Zambia wanapenda kuliita hili tamasha ni kati ya matamasha makubwa Zambia na linafanyika kila mwaka chini ya wizara ya Utamaduni na kampuni ya Bewaries yaani kama inavyokua Fiesta huku kwetu na wana utaratibu wa kualika wasanii toka nje ya Zambia na safari hii ilikua atumbuize Tekno ila akashindwa kwenda dakika za mwisho ndio kijana wetu Diamonda akapata nafasi ya kwenda kama mbadala wa Tekno.
Tuache uwasilishaji mbovu wa habari ni aibu kama Tekno alivyokuja Fiesta Dar alafu akatangaze aliujaza uwanja wa Leaders wakati kulikua na timu kubwa ya wasanii wetu ambao wamewavuta hao watu hii ni sawa Diamond yeye alienda kama mualikwa naamini hata angeenda Kingwendu watu wa Zambia wangejazana kwenye tamasha lao maalumu ila tunadanganyana kua kijana wetu amejazana uwanja ingawa mwenyewe Diamond aliweka wazi kua anaenda kuungana na wasanii lukuki toka Zambia kwenye hilo tamasha ni sawa uwepo wake ni chachu lakini hata asingeenda asingepunguza idadi ya watu,kwenye ukweli tuwe tunaambiana tu sio vibaya ila pia Diamond ametuwakilisha vyema kwa classic show.
hivi fiesta Dar mkisema anakuja Rihanna na kusema watakuepo wakina Lina tu?
lipi litajaza?
sio mfanya biashara ,ila uwepo wa Main artist katika tamasha unalipa Thamani Tamasha zima kwanzia Attention ya watu, mpaka Pesa ya kiingilio.
kwa maana akija Rihanna wanaweza fanya kiingilio 30000 kutokana na thamani ya msanii isiyokwepeka ,na local artist ikawa 10000 na wasijaze vile vile

local wanaweza piga show hata wasanii 10 club na haijai! club tu...

kwahiyo hapo diamond kafanya chachu kubwa sana. tumpe heshima yake, kwenda kuwa main Artist tu ni kujidhihirisha kuwa hata bila sapoti ya wasanii wengine anaweza akajaza vile vile.
ukizjngatia ameimba na mashabiki mwanzo mwisho ni kwasababu wanafahamu uwepo/ukubwa wake

Diamond anajitambua sana. asipokushika kwenye Tungo zake, basi mavazi atakayovaa ,usipoyapenda utapenda Dance!
ana sifa zote za kuwa mtumbuizaji Bora Africa.
sifa zake tumpe ,kafanya vizuri zaidi Zambia
 
Kama walikuwa wanauwezo wa kujaza uwanja bila diamond walimualika wa nini kupoteza zaidi ya milioni 100 za bure? are you serious?
Wanatanzia tunapenda mafanikio lakini tunachukia waliofanikiwa
Mkuu nyingine hii hapa itafanyika DRC CONGO akijaza tena uwanja huko mtasema Tekno hakwenda
View attachment 503598
watasema Davido hakwenda!
tena huko akipiga lile sebene lake sijui kama wacongo watakaa

waKenya wanamtamani awe wao ,wanaija wanamtamani maana anapelekesha wasanii wao!
Mungu katujalia neema imetoka kwetu kukomboa mziki wetu lakinj bado hatuikubali...
sasa nimejua kwanini waisraeli walimsulubisha masihi.
 
Tatizo lako akili yako inawaza Diamond na Kiba kwa kua wamewafundisha kuvaa suruali za kubana au pengine umri wako pia hawa watoto ndio wamekufanya upende muziki sasa nakushauri kajifunze kuhusu hilo tamasha jaribu ku-google attendence ya mwaka jana wakati wamelikwa Casper na Roberto ilikuaje na mwaka huu ilikuaje utajua hilo tamasha sio la mtu au msaani mmoja ndio maana nimesema hata angeenda Kingwendu asingepunguza wala kuongeza idadi ya watu kwa kua wizara yenyewe wanasimamia kuvuta watu kwenye utamaduni wao duh watoto wa siku hizi hata nguo za ndani mtakua mnavaa kuwafuata hao wanaongoza timu zenu Diamond na Kiba maana mtu akitoa maoni tu fast mnawahi uyu atakua timu flani kwa kifupi hao kuku wenu wawili wamenikuta naupenda muziki hata kabla hawajaruhusiwa na mama zao kuimba.
Rudi kwenye comment yangu ya mwanzo nionyeshe nilipomtaja uyu kaka yenu Kiba maana ishu ya Diamond sijui Kiba ameingiaje,itakua ni KICHAA 1st class siku Baraka the Prince ajisifie alijaza uwanja wa Nangwanda Sijaona wa Mtwara kwenye tamasha la Fiesta wakati waliotumbuiza walikua wengi wapo walioenda kumuona Blue na wengineo,narudia tena Diamond kwenye tamasha la MosiOfThunder hakua kwenye ratiba amepata zali baada ya yule mtoto Tekno kuthibitisha hatokwenda na hata angeenda Tekno tungekataa kama angetuambia kajaza ule uwanja wa golf maana kwenda au kutokwenda kwa Tekno hakujabali idadi ya wahudhuriaji duh walimu wana kazi kweli uko mashuleni FYI hiyo show nimeiona yote.
Acha uongo!!hiyo ratiba ya Diamond kwenda kupiga show huko Zambia alikuwa nayo tangia mwezi wa kwanza!!

Nakuona tu unavyojifanya unajua wakati huna unachokijua!!muongo mkubwa
 
Back
Top Bottom