Diallo amlipua Lowassa

Wote wawili Mwal Nyerere alisema kwa Kizanagi MACHANAGI,Wote si wasafi EL anajisifu na Mradi wa maji ya Victoria mpaka siri za Baraza la Mawaziri anazitoa nje,hivi lazima 2015 awe Rais? Diallo naye ana usafi gani wa kumsema EL? Wafanyakazi wa Sahara media wanaishi kwa shida mishahara haieleweki.
 

Siri gani hizo? Baraza la mawaziri linalojielezea Bungeni linatakiwa kuwa na Siri gani mkuu ebu tujuze
 
Nyerere alimkataa Kikwete alafu akapitishwa na Kamati Kuu na Halmashauri Kuu mpaka kufika mkutano mkuu Nyerere akiwepo?

Waliokataliwa na Nyerere, ambao ni Malecela, Kolimba na Lowassa walikatwa mapema kwenye hatua za awali.
Wewe ni msahaulifu tu! Nyerere alimkataa Kikwete na Lowassa mwaka 1995 na ndipo mkapa akapitishwa mwalimu alimuunga mkono Mkapa. Ktk kumpinga kikwete Nyerere alisema hatuwezi kupeleka mtu wa kuvaa jinsi ikulu, na kuhusu lowassa nyerere alihoji utajiri alionao. Hiyo habari ya mtu kafika kwenye kamati kuu ni kitu kingine kwasababu nyerere alipopinga hawa watu alikuwa anatoa maoni sio kupiga marufuku kwahiyo huko chini wajumbe wenye njaa waliendelea kumpigia debe lakini ilipofika kule juu wale wazee walizingatia maoni ya nyerere. Na wale wazee ndio wengi wameathirika baada ya kiwete kushinda 2005 maana aliwachinjia baharini kwa kisasi. Sasa kwasababu ya maslahi watu mnajifanya mmesahau alichoongea nyerere juu ya kikwete. Wengine wanaoona aibu wanajitahidi kukubali lakini bado wanapindisha ukweli wanasema Nyerere alisema kikwete bado mdogo (miaka 45). Hivi nyerere alimwonaje kikwete mdogo ktk umri wa 45 wakati yeye aliongoza nchi chini ya miaka 40?
 
Tuhuma za Kundi la Makuwadi wa EL dhidi yangu
hayana msingi wowote na kama ni kweli Edward
amewapa waziseme kwangu na kuhusisha Mheshimiwa
Rais ni mwendelezo wa EL kumdharau Rais ambaye
alimpa madaraka makubwa na kosa likiwa kukubali
ajiudhuru baada ya kufanya madudu aliyoyafanya.
Huu ni mwendelezo wa kumsumbus Rais ambao ulianza
tangu 2008 baada ya kujiuzulu uwaziri mkuu.
Anayoyasema haya sipendi kuyajibu ila kwa ajili ya
kuweka kumbukumbu sawa, imebidi niyajibu lakini
nikizingatia kuwa sitaweza kuyajibu yale ninayoyajua
chini ya kiapo:

1: Sijamtuma Mzee yeyote kwenda kwa Lowasa kwa
sababu sio waziri mkuu tena na hata kama angekuwa
bado waziri mkuu nisingeweza kumwambia mtu
akaniombee vyeo kwa Lowassa. Hao wazee aliowataja
wapo Mwanza na mnaweza kupata namba zao za simu
na kuwauliza kama nilishawahi kufanya hivyo. Pili,
mwaka 2003/4 haukuwa mwaka wa uchaguzi,
ilikuwaje niende kuomba cheo wakati niliingia baraza
la Mhe. Rais Mkapa 2001? Wakati huo Lowassa
hakuwa waziri mkuu! Tatu, mwaka 2004 sijaonana na
JK na Karamagi hajanishawishi kumuunga mkono JK
mwaka 2005. Mimi ndiye niliyetumwa kumwambia
Lowassa asigombee 2005 kwavile dhambi na tuhuma
dhidi yake zilizotolewa na Mwalimu zilikuwa kwenye
mioyo ya watanzania na asingeweza kupata kura za
ushindi isipokuwa angempunguzia JK kura zake na
wote kukosa. Karamagi tumekutana naye bungeni
baada ya kuchaguliwa ubunge baada ya kifo cha Mhe.
Kinyondo. Mimi nimezaliwa na kukua kwa kuzingatia
nidhamu ya Kisukuma, sijalelewa kihuni kufika
kumsema mtu kama JK. Namsema EL kwa sababu ni
mchafu, na sasa sitayasema yaliyo mazito au machafu
zaidi dhidi yake, hadi nitakapoona kweli kachukua
fomu kugombea Urais! Mimi sijasema Lowassa
alidhulumu CCM kupata hisa Vodacom, nilichosema
CCM ilikuwa iwe mbia wa MTN, kampuni iliyonyimwa
leseni wakijua fika kuwa ilikuwa ikisaidie chama,
badala yake wakafanya njama kuvunja tume ya
mawasiliano kihuni, na hapohapo wakaipatia vodacom
leseni lowasa kwa kutumia watoto wake, alipata
walikipata. Ushahidi kuhusu hili ni kampuni yake
kupewa U-Super Dealer wa Vodacom ambayo
uliwafanya wanufaike kwa kuuza simu nchi nzima.

Kama wanasema Lowassa ni mzima, naomba akakimbie
uwanja wa Taifa azunguke hata mara moja kama
hataishia ICU. Na kama ni mzima, anatumia fedha za
nchi kwenda kutibiwa nini ujerumani kila wakati au
Ujerumani nako siku hizi kuna waganga wa kienyeji?
Pili kwanini alikwenda kuombewa kwa Emmanuel
Ministries huko Nigeria? Kampeni za Urais zinahitaji
afya nzuri, sio mzaha kuweka mgonjwa akatufia
kwenye jukwaa! Kuhusu tuhuma ya rushwa toka kwa
Kimaro, nina hakika Kimaro bado yupo hai, na kama ni
mkweli aseme ukweli. Kimaro ni rafiki yangu na
nilimshawishi akawekeza hoteli ya Nyumbani sasa ni JB
Belmonte, Mwanza. Sijachukua fedha ili nimpatie
kitalu kwavile yeye sio mwindaji na sijasikia kuwa ana
hiyo biashara. Ninachofahamu ana mahoteli na ndiyo
biashara yake. Rais yupo kama alishaniita kunieleza
hilo anaweza akasema, ni mkweli. Tuhuma za mimi
kuhongwa na Kimaro alizianzisha Lowassa baada ya
mimi kutaka kumuondoa Mkurugenzi wanyama pori
wizara ya Maliasili. Mkurugenzi huyo alikuwa na
mahusiano naye na baadae walikuja kuoza watoto
wao. Hilo kila mtanzania analifahamu, na alimtetea
sana abaki wizarani wakati huo. Lowassa yupo kwenye
mtandao wa yote yanayosemwa kuhusu wanyama pori.
Pia tuhuma za kumtapeli aliyekuwa Rais wa Zanzibar,
Mhe Karume ndio nazisikia leo. Karume sijafika
nyumbani kwake Zanzibar na wala hata alipokuwa
Ikulu Zanzibar. Yupo na anaweza kuulizwa, ni mkweli
atasema yaliyo kweli.

Huyo msichana anayesemekana nilimpa mimba,
mhudumu wa Dodoma hotel, ndiyo namsikia leo, na
kama yupo aniletee mtoto huyo kwani ndio nasikia
kwenye watu wa Lowassa baada ya kuweweseka na
machache tu tuliyoyaweka hadharani. Mwisho la
kupewa fedha na mtuhumiwa wa IPTL nalo jipya
simfahamu, labda Lowassa anamfahamu! Tatizo la
huyu Lowassa, ni kupata URAIS, asipoupata sijui kama
atabaki na afya ya kuridhisha. Anatuhumu watu
tusiounga mkono jitihada zake tu, je wanaogombea
watakuwa na hali gani mbele yake? Ushauri wa bure
kwa wapambe wa Lowassa: Kuleni fedha yake maana
ni halali yenu, fedha za kukwapua kwa njia zisizo
halali ni haki ya kila mtu kuzitafuna, ila Urais
hatopata.Kidumu Ccm.
 

Huo mradi ulikwa wa siku nyingi sana. Kitu gani kimemwamsha Dialo kipindi hiki? Huu urais unawatesa wengi
 

Vita ya panzi hiyooooooooo
 

mkuu umenena na nmekuelewa sana
 

Ebu tuwe serious jamani!!! Diallo amejibu hoja iliyotupwa kwake!! kama sikosei kulikuwa na uzi unaomwumbua Diallo na yy analeta majibu..dawa ya moto ni moto..hivyo sioni sababu ya kumlaumu bali hoja ziendelee. nyie washabiki wa EL je anaweza kukimbia uwanja wa taifa???mbona mnashindwa hoja na kuendeleza uswahili!! boss wenu hawezi kupata ukubwa kwa kuhit the bush njoeni na hoja za mashiko ili ss tulio neutral tuhamie upande wenu. lakini kwa matusi mnayoleta hapa nashawishika kuamini Diallo kuna kitu ameandika kina ukweli.
 
Dialo ni muaji na jambazi mkubwa ndio maana alikataliwa na wananchi wa Ilemela, haitaji science kugundua amepoteza mvuto siasa za mwanza , mbona hajibu issue ua mauaji ya mtumishi wa CCM Ibrahim Babangida

Nakubaliana na wewe jamaa huyu ni KILLER hata mauaji ya Mh Mabina ana mkonowake katika mauaji hayo.
 

labda kama alishamuibia mama yako mzazi.ninachojuwa watanzania tunamuhitaji lowassa
 
wadau
Nimeona tukumbusha list ya mafisadi wa elimu nchini ili jamii iwafaham walivyo na vyeo ambavyo walishakuwa navyo.
Nilishasikia kuwa Anton Diallo naye ni fisadi wa elimu naombeni udhibitisho kwa hili na listi ya wengine pia.
Tafdhali niombe tusimwandike mtu kwa chuki ambazo hazina msingi wowote
 
Nasikia d ndio kiongoz wa makanjanja wote wasiokuwa na elimu.nasikia anayo mpaka phd lakin kichwani ni patupu
 

Huko 'Ulikosikia' ingekua busara kama ungeomba "Uthibitisho" kulekule kisha uje na habari kamili hapa!
 
Nasikia alikuwa na certificate ya kufunga vidonda sijui aliukwaa vipi udr.
 
Naiyonea huruma sana hii nchi yangu Tanzania.
Hivi hii serikali mpaka mtu anakamata nafasi kubwa kama ya uwazir na hana elimu usalama wa taifa wakati huo wanakuwa wapi?
 

Japo sijasoma ulichoandika, ila najua wewe utakua ni msukule EL.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…