Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,577
- 729,451
Hamlali? Ama hulali? Ni swali la kawaida sana ambalo limeshaulizwa na members wanapokuta kuna new post hasa wanapotoka usingizini.
Unajua tunapoenda asubuhi kupata staftahi ya chochote iwe chai kongolo mtori supu nk kuna watu walidamka alfajiri kuandaa ili afisa ukija upate mambo.
Najua wazi kabla hujaingia kibaruani utataka kujua kuna nini jipya JF! Haya mapya yanaandaliwa jamani tena buuree kabisa. Hayajiandiki yenyewe!!!
Mapumziko ya mchana na baada ya kazi muda wa jioni lazima utataka kuchungulia na kuona kipi kipya ama nini kinaendelea nchini na duniani kupitia JF.
Humu kuna members ni Kama wapishi wa wengine walioko makazini na mishe nyingine....ambao wanapokuwa free huja humu na kuperuzi yale ualiyokwisha andaliwa kwa ajili yao.
Tuwapende tuwapongeze na tuwashukuru wapishi wetu hawa kwenye vijiwe vyote kuanzia MMU mpaka JLW kwa kazi kubwa wanayofanya bila kuchoka.
Kumbuka tuna mabarmaid humuhumu kwakuwa kuna post za kuburudisha, tuna walimu humu kwa zile post za kufundisha na kuelimisha, tuna wazee wa busara kwenye post za kuongoza kuonya na kuelekeza.
Tuna wezi matapeli walozi hata wanga lakini wote hawa wanastahili kula chakula kitamu cha JF kisichokifu, labda tu kama hakupendi ama una mzio