Dhana za ushindi wa kishindo ccm zimekwisha.

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
2,000
Tumeshuhudia leo jk akikili ya kwamba uchaguzi huu umetoa funzo kubwa kwa ccm na inabidi wakakae chini na kujipanga kwa kuwa hii ni ishara mbaya kwa ccm.yaani toka 82% mwaka 2005 mpaka 61% 2010.na sasa ule usemi wa ushindi wa kishindo hauko tena.wadau nini maana ya asilimia hizi kushuka.Hongera dr slaa kwa kuwanyima usingizi.
 

Catagena

Member
Oct 23, 2010
91
0
Ndugu yangu, maana ya asilimia hizi kushuka ni ishara ya kushuka kwa umaarufu wa JK kwanza, lakini ndani ya hili ni kushuka kwa umaarufu wa chama cha mapinduzi, sera zake, mfumo wake wa uongozi na viongozi wake kwa ujumla. hii inaonyesha kuwa, wapinzani wakijipanga vizuri, soon or later watachukua hatamu za uongozi wa nchi.

Kikubwa ni wao kukaa chini, kujipanga kuanzia sasa na sio kusubiri dying moments. They have a great potential na wana watu wanaokubalika sana..Kwa sababu wanaoongoza CCM na wanaongoza vyama vingine ni watanzania, waliosoma pamoja, pengine hawa wa vyama vingine ni competent zaidi kuliko wa ccm, tatizo ni kwamba wako nje ya system.

I am still optimistic.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom