Dhana ya uzalendo ni kama mfumo wa mapenzi ya mzazi na mwanawe: mtazamo wa kimetafizikia (act and potency)

philosophy

Senior Member
Nov 11, 2012
104
42
Suala la upendo wa mtoto kwa mzaziwe ni la kimaumbile (nature) kwani mtoto ni damu ya mzazi, hivyo upo mvutano halisi na wa kiasili ambao kwao dhana ya upendo imejengwa kama uwezekano ila haijawa (potency) na ili upendo ukamilike uwe dhahiri (to be actualize) yapaswa mzazi kufanya mazoezi ya kujenga upendo huo kwa mwanaye. Mazoezi hayo si mengine bali ni matendo mema ya mazazi kwa mwanawe ili upendo ujengeke miongoni mwao. Kinyume chake (matendo maovu) humfanya mtoto apoteze uhalisia wa upendo (there is no actualization of act from potency to act but remains in potenciality). Jambo hilo linajenga chuki kwa mwana dhidi ya mzazi wake na pengine mwana huyo huona mzazi si mzaziwe.

Dhana hii ni sawa na Uzalendo wa raia kwa nchi yao. Uzalendo kimaumbile (naturally) upo kwa kila raia kama uwezekano wa kuwa (potency) ila ili uonekane kwa vitendo au kwa vyoyote vile (to be act) unahitaji matendo mema ya wale wenye dhamana ya kuiongoza nchi dhidi ya raia. Lakini, kama raia watafanyiwa unyama na uovu dhidi yao kisa wanayo mawazo kinzani na pengine mazuri lakini hayaoani na ya wenye mamlaka, hakika uwezekano wa uzalendo kuwa halisi kwao hautakuwepo (the process of potency to act, to be actualized will automatic cease). Raia hao hawataona haja tena ya kuipenda nchi yao, na uzalendo kwao hautakuwepo.

Na MIMI
 
Back
Top Bottom