Dhana ya USALITI ndani ya CHADEMA na Hatma ya Demokrasia ndani ya vyama vya Siasa

mkuu wangeweka wazi kua ni " STRUGGLE FOR POWER" badala ya kutafuta a very soft and deceiving terminology ya " USALITI" watu wae wawazi wanapoamua kuwa viongozi katika jamii yenye watu wenye uelewa
tatizo kubwa la waTz hawajawekezwa vichwani mwao (na hii ndo sababu ya kuichukia ccm) na chadema kama ilivyo ccm wanatumia mwanya huo huo wa watu kuwa weupe vichwani kuwalaghai. lakini baya zaidi ni kutumika mtu kama tobo lisu, mtu ambaye anaweza kuishi maisha mazuri hata bila ya chadema, tofauti na watu kama akina mnyika, lema nyasari et al ambao chadema ndo kila kitu. ni aibu kwa kweli.
 
Je ni kweli kwamba kuna Usaliti??

Tafsiri halisi ya usaliti inaendana na uhalisia wa tuhuma dhidi ya wahusika??

Je ni kweli kwamba CCM inapoteza muda wake kuwa na mapandikizi katika Chadema. SI KWELI NA SI SAWA!!!

Dhana ya Usaliti katika Chadema ni muendelezo wa kampeni za kuhalalisha ubinafsi na kutakatisha mbinu chafu za kuwahadaa watanzania kuwaunga mkono chadema kwa kutegemea public sympathy.

Chadema ni mabingwa wakubwa wa kupotosha na kutegemea sympathy kuliko kuibua hoja halali zenye ushawishi na weledi.

Viongozi wa sasa pamoja na wafuasi wengi, wanajenga misingi ya chama katika hisia zaidi kuliko uhalisia...Kosa kubwa.

Hii si mara ya kwanza kwa Chadema kutegemea huruma ya wananchi ili kukubalika, ni utaratibu mbaya ambao utaliangamiza taifa siku moja kama hauta achwa haraka, si ajabu kutengeneza matukio ili kuipaka matope serikali na wao kuonekana wema. (mtindo wa chui kuvaa ngozi ya kondoo).

Kila taasisi lazima iwe na utaratibu wa kidemokrasia na kujenga misingi ya wazi , Chadema inakosa sifa hii muhimu.

Kudai kwamba CCM ina mapandikizi ndani ya Chadema ni hoja mfu, na kama hivyo ni sahihi si ajabu kusikia mapandikizi ya Chadema ndani ya CCM.

Hivyo basi, kelele za kuhusisha " usaliti" ndani ya chama cha demokrasia na maendeleo na CCM ni kukosa hoja za msingi za kuwaambia wananchi bali ni propaganda tu za wadau ndani ya chama kulinda nafasi zao, na kupunguza kasi za wengine katika kukuza demokrasia ya kweli.

Karata hii imegoma na chadema watafute mbinu nyingine ya kupata public sympathy badala ya hii ya usaliti ambayo ipo kwa ajili ya maslahi ya wachache ndani ya chama.

Heri ya waka mpya 2014 wenye siasa bora!!
Ebu angalia kidogo maana ya "Msaliti" kwa lugha ya wenzetu,yanatokana na maneno Betray na Traitor
betray |biˈtrā|1 expose (one's country, a group, or a person) to danger by treacherouslygiving information to an enemy: a double agent who betrayed some 400 British and French agents to the Germans.• treacherously reveal (secrets or information): many of those employed by diplomats betrayed secrets and sold classified documents.• be disloyal to: his friends were shocked when he betrayed them.2 unintentionally reveal; be evidence of: she drew a deep breath that betrayed her indignation.
traitor |ˈtrātər|nouna person who betrays a friend, country, principle, etc.: they see me as a traitor, a sellout to the enemy.PHRASESturn traitor betray a group or person: to think of a man like you turning traitor to his class.ORIGIN Middle English: from Old French traitour, from Latin traditor, from tradere ‘hand over.'

Jee chadomo wanao ushahidi wa zito kununuliwa na ccm ama hyo stry ni funika kombe kumstiri mwenye kiti
Ukitazama waliothbutu kumuondosha mbowe wote wamepigwa na chini kwa majina mbali mbali reefer to chacha wangwe R.I.P na sasa zzk utauona jinsi gani m/kiti na katubu mkuu walivo waoga kuachia madaraka ama wana madudu wanayaficha ndio maana wanaogopa
 
Labda niulize hivi hapa duniani hakuna wasaliti? Wasaliti wanarangi gani? utamjuaje mtu Fulani ni msaliti? Ni seme tu kwamba ZZK kwa muda mrefu sana amekuwa akituhumiwa kwa mambo mbalimbali, mengine alikiri. Kwa mfano mawasiliano yake na mkurugenzi wa usalama wa taifa (ccm). Ushaidi upo vilevile kwamba aliisaidia ccm kupata baadhi ya majimbo kwa kuhakikisha wagombea wa CDM kutolewa. Siyo hivyo tu alisema mbele ya kamera kwamba atamsaidia Kafulila kushinda ubunge kabla ya Mnyika. Huyu ZZK tumwite nani basi??? kwangu mimi ninayefikiri kwa kutumia kichwa badala ya tumbo nitamwita ZZK ni MSALITI. Bahati yake tu ni kwamba usaliti ameufanyia uraiani na siyo jeshini. Maana jeshini wanaadhabu moja tu ya msaliti.
mkuu hujasoma comment yangu vizuri.
niambie huo usaliti wa Zitto kwa nini umeonekana baada ya kumchallange mbowe tu? kwa nini kashfa za aina hiyo pia zilimuandama chacha wangwe kwa sababu hiyohiyo?
kuhusu kuongea na jack nzoka wa TISS, zitto alishalitolea maelezo hilo suala, angalia mahojiano yake na Asha dee/di humu JF, kuna uzi ulikuwa kwa ajili ya kumhoji Zitto.
kuhusu kafulila, hilo liko wazi ni kuwa alifukuzwa kwa sababu alionekana kumsapoti zito, nani asiyelijua hilo? hata wewe ungefanya hivyo hivyo.
hebu nakushauri jipe muda utafakari hizi tuhuma za zitto utaelewa ni nini kiko nyuma yake.
otherwise vijana tutatumika sana tu mpaka hapo tutakapojitambua.
 
mkuu wikolo,
kwanza nakiri ni kweli mie ni mwanamageuzi, pia sina tatizo na dr slaa hata kidogo.
nadhani CDM tujielekeze ktk kuangalia mantiki ya hoja zinazozotolewa bila kujali zimetolewa na nani.
ikumbukwe tuhuma nilizokugusia hapo juu kuhusu kamanda mbowe zimetolewa na wanaCDM wenzetu tu na sio ccm - rejea waraka wa marehemu chacha wangwe na sasa wa akina dr kitila.....hii sio bahati mbaya hata kidogo.
CDM tuna viongozi wenye uwezo wengi tu, nadhani ni busara kwa mwenyekt kujipima na kuwaachia wengine waongoze chama pindi uchaguzi mkuu ndani ya chama utakapofika mwakani.

Mkuu wangu, nafikiri hapa tunatofautiana tu kwa namna ambayo tunalitazama hili jambo. Tuhuma kutolewa na wana CDM haimaanishi kwamba ni lazima ziwe za kweli! Kama hivyo ndivyo kwamba kwa sababu Mbowe ametuhumiwa na wana CDM basi shutuma ni sahihi, ni kwa nini basi unapinga hizo shutuma zingine zinazoelekezwa na wana CDM hao hao kwa ZZK? Katika posti zako nyingi hapa unapinga sana suala la ZZK kwamba halina ushahidi wakati huo huo sijaona wewe ukiweka ushahidi wako hapo juu ya tuhuma za Mbowe! Nilikuuliza kwenye ile posti nyingine kwamba ni kwa nini wana CCM nao wanataka Mbowe aondoke kwenye nafasi eti ili CDM iimarike na iwe na demokrasia zaidi? Au hao wana CCM nao ni wana mageuzi kama wewe?
 
Yaani tumchague ZZK kuwa mwenyekiti wa chama chetu wakati kila siku anashinda anacheza bao na rais wa chama cha mizigo?

Tumchague ZZK wakati ni mkwepaji wa ushiriki wa operation tofauti tofauti za chama km operation sangara n.k.?

Tumchague ZZT wakati kwenye matukio mbalimbali muhimu bungeni amekuwa haudhurii kukwepa kumuuzi Baba wa rafikiye(JK)?

Mie nafikiri hata bila ushahidi ule wa uasi ulioonyesha na Chadema,ushahidi wa kimatukio ambao Zitto amekuwa akiuonyesha ndani na nje ya bunge unafaa kabisa kumuondoa kwenye kinyanyiro chochote cha uongozi ndani ya chama!

Hebu jifikirieni mtu mnaemwaminia kwenye Chama Chenu cha Mizigo mnamuona kila siku anawasiliana na Dr.Slaa na mara nyingine akishirikishwa kwenye shughuli nyingine za chama chetu,unafikiri mpaka sasa huyo mtu angekuwa bado ana meno 32?Mngekuwa mmeshamng'oa yote kama sio kumpeleka kule mlikompeleka Mwangosi!
 
Mkuu wangu, nafikiri hapa tunatofautiana tu kwa namna ambayo tunalitazama hili jambo. Tuhuma kutolewa na wana CDM haimaanishi kwamba ni lazima ziwe za kweli! Kama hivyo ndivyo kwamba kwa sababu Mbowe ametuhumiwa na wana CDM basi shutuma ni sahihi, ni kwa nini basi unapinga hizo shutuma zingine zinazoelekezwa na wana CDM hao hao kwa ZZK? Katika posti zako nyingi hapa unapinga sana suala la ZZK kwamba halina ushahidi wakati huo huo sijaona wewe ukiweka ushahidi wako hapo juu ya tuhuma za Mbowe! Nilikuuliza kwenye ile posti nyingine kwamba ni kwa nini wana CCM nao wanataka Mbowe aondoke kwenye nafasi eti ili CDM iimarike na iwe na demokrasia zaidi? Au hao wana CCM nao ni wana mageuzi kama wewe?

kamanda, ktk tuhuma na hata propaganda mbali mbali za akina nape na wenzie dhidi ya chama daima uongozi wetu umekuwa ukijitokeza haraka kutolea ufafanuzi ili kama ni uongo usije kuaminiwa na wananchi kwa ujumla na hatimaye kupoteza matumaini - hii ni sahihi kabisa.
tukirudi ktk tuhuma za mbowe mara zote (chacha wangwe na sasa zito) uongozi wetu umeshughulika na watoa tuhuma tuhuku hku UKIPOTEZEA kujibu tuhuma zenyewe, kuna nn hapa?!
Kuhusu zito, ni wajibu wa kamati kuu kuturidhisha sie wanachama tusiokuwa wafuasi namna ya ushiriki wa zito ktk tuhuma zinazomkabili - hapa simaanishi wafuasi waliolishwa chuki dhidi yake kwa sababu kimsingi wenyewe wanacheza mziki wasiouelewa hata mirindimo yake, namaanisha uongozi hususani kamati kuu kwa mujibu wa katiba ya chama.
 
Tunasubiri Ijumaa ili tujue kama kweli CDM kuna power struggle au vipi. Wakifukuzwa wanaoitwa wasaliti na chama kisipomeguka basi tutajua mengine yote porojo. Hadi sasa kinachoshangaza ni kwa chama kinachoelezwa kuwa cha "kikabila", "kiukoo" na "kidini" kuendelea kung'ang'aniwa na wanachama watuhumiwa pamoja na mashabiki wao ambao hawaishi kuanzisha mijadala lukuki na kukesha JF wakijadili "uozo" wa chama hicho.

Nilitarajia watakiacha kijifie. Lakini utashangaa wakati mwingine washambulizi wake wakidai kuwa CDM bado ni tumaini pekee la wapenda demokrasia hivyo hawawezi kukiachia kwa "wahafidhina"! Chama cha ukoo? ukabila? ukanda? udini? Who would need such a party? And why waste time and energy discussing it kama sio kuna mchezo wa covert operations kukisambaratisha kwa kisingizio cha demokrasia? Let's be serious! CDM lazima ichukue maamuzi ya uhakika kumaliza ujinga huu unaoendelea bila hitimisho.
 
Je ni kweli kwamba kuna Usaliti??

Tafsiri halisi ya usaliti inaendana na uhalisia wa tuhuma dhidi ya wahusika??

Je ni kweli kwamba CCM inapoteza muda wake kuwa na mapandikizi katika Chadema. SI KWELI NA SI SAWA!!!

Dhana ya Usaliti katika Chadema ni muendelezo wa kampeni za kuhalalisha ubinafsi na kutakatisha mbinu chafu za kuwahadaa watanzania kuwaunga mkono chadema kwa kutegemea public sympathy.

Chadema ni mabingwa wakubwa wa kupotosha na kutegemea sympathy kuliko kuibua hoja halali zenye ushawishi na weledi.

Viongozi wa sasa pamoja na wafuasi wengi, wanajenga misingi ya chama katika hisia zaidi kuliko uhalisia...Kosa kubwa.

Hii si mara ya kwanza kwa Chadema kutegemea huruma ya wananchi ili kukubalika, ni utaratibu mbaya ambao utaliangamiza taifa siku moja kama hauta achwa haraka, si ajabu kutengeneza matukio ili kuipaka matope serikali na wao kuonekana wema. (mtindo wa chui kuvaa ngozi ya kondoo).

Kila taasisi lazima iwe na utaratibu wa kidemokrasia na kujenga misingi ya wazi , Chadema inakosa sifa hii muhimu.

Kudai kwamba CCM ina mapandikizi ndani ya Chadema ni hoja mfu, na kama hivyo ni sahihi si ajabu kusikia mapandikizi ya Chadema ndani ya CCM.

Hivyo basi, kelele za kuhusisha " usaliti" ndani ya chama cha demokrasia na maendeleo na CCM ni kukosa hoja za msingi za kuwaambia wananchi bali ni propaganda tu za wadau ndani ya chama kulinda nafasi zao, na kupunguza kasi za wengine katika kukuza demokrasia ya kweli.

Karata hii imegoma na chadema watafute mbinu nyingine ya kupata public sympathy badala ya hii ya usaliti ambayo ipo kwa ajili ya maslahi ya wachache ndani ya chama.

Heri ya waka mpya 2014 wenye siasa bora!!

Hii ni dhana inayoshabikiwa na viongozi dhaifu wanaoogopa mabadiliko,hua na tabia ya kuanzisha vikundi vya wapambe ambao baadae ugeuka kuwa wanaharakati kwani wao hufuata kauli za viongozi na wala sio sera nzuri za chama,Hili ndilo lilizaa hii dhana ya akina lema kujiona wao ni wanasiasa kumbe ni wanaharakati,Mbowe kudanganywa na hao wanaharakati na wachumia tumbo,akawa kipofu meli kubwa ya chadema inazama kisa ZITTO wanademokrasia wa karne ya 21,tumaini la vijana na wakulima.Kwa dhana ya usaliti akuna atakayebaki chadema,wachumia tumbo wanazidi kumpofusha mwenyekiti naye aoni mbele(chaguzi ndani ya chama na serikali za mitaa),kumbe wanasahau baada ya zitto ni slaa
 
Leo ZITTO KABWE anaonekana msaliti, ingekuwaje kama Zitto angekuwa na kadi hai ya CCM kama DR.SLAA na hataki kuirudisha? Wanachadema tungekuwaje hasa wale wanaomwita msaliti?

Watu kama kina Shibuda walishawahi kutamka hadharani uzushi kuhusu chama chetu na mpaka leo ameachwa kama akiba, je hakuvunja katiba au kwa kuwa hana madhara kwa uongozi wa juu? (muungwana Mnyika tu)

Leo tunamnyooshea kidole Zitto; je, viongozi wetu wa juu ni wasafi?

Wanachadema tufikirie kwanza kabla ya kukaririshwa wimbo wa "Zitto msaliti". Wapo vijana Makao Makuu ni waganga njaa tu hawana vision na watanzania maskini zaidi ya posho kidogo wanayopewa na wazee ambayo imetokana na kodi ya wananchi, vijana tubadilike tusitumike.

Pia katika mikutano kadhaa ya chama iliyofanyika kwa nini hoja ni wasaliti tu na isiwe gharama za umeme, kodi juu, ukiukwaji wa haki za binadamu na kutokuwajibika kwa serikali ya CCM au ni kuishiwa hoja?

Mimi ni mwanaCHADEMA hai na CDM inahitaji uongozi kuelekea uchaguzi mkuu 2015.
 
Mnafiki mwenyewe,kwanza tutake radhi popo wewe

Unafikiri kila kitu siasa zisizo na mbele wala nyuma,kama ni wanafiki wewe umekosa nini? si unakula kwako,unalala kwako,unaendelea na kibarua chako? sasa sie wanachadema kuwa wanafiki imekunyima nini wewe angali wewe si mwanachama?
 
ninachosema ni tuwe wakweli mkuu,inawezekana una nia ya dhati ya Tanzania kupata mabadiliko lakini baadhi ya wanacdm ni wanafiki(waganga njaa)
 
Mkuu hata mimi ninayokadi ya CCM tawi la Abijani UDSM but Niko Chadema so kuwa na kadi sio issue kadi lazima ilipiwe kuwa nayo bila kuilipia ni sawa na kutokuwa nayo tu. ...!!!!
 
Mkuu hata mimi ninayokadi ya CCM tawi la Abijani UDSM but Niko Chadema so kuwa na kadi sio issue kadi lazima ilipiwe kuwa nayo bila kuilipia ni sawa na kutokuwa nayo tu. ...!!!!

namaanisha mashtaka ya zitto yangekuwaje kama angekuwa na kadi tuseme mfu ya ccm? kwa nini wanataka afukuzwe kipindi hiki ili hali mwanaccm robo tatu kama shibuda akiachwa? mkuu binafsi nasikitishwa sana na mivutano hii inayodhoofisha chama
 
Kadi sio hoja wengi tunazo kama kumbukumbu kwani lichama lenyewe linaelekea kufa tutaziweka makumbusho.,Hebu kuwa makini kidogo kufuatilia track za huyo unayemtetea kuanzia pale alipoikwaa kamati ya madini.
 
Back
Top Bottom