Mbogela
JF-Expert Member
- Jan 28, 2008
- 1,384
- 257
Kwa kifupi ningependa nitoe wosia kwa vyama vya SIASA hasa vyama vya Upinzani na hasa CHADEMA.
Imetokea kasumba ambayo imekuwa inakuwa kwa kasi ya ajabu ndani ya vyama vya upinzani. Ndani ya vyama vya upinzani umetokea upepo wa kutokuaminiana, kumetokea wimbi kubwa la kutuhumiana USALITI miongoni mwa wanachama. Mtu akionekana kuwa amekuwa na mawazo tofauti na wenzake hata anapokuwa tofauti na kundi dogo tu ndani ya Chama au na kiongozi mmoja tu ataitwa msaliti na kundi la upande wa pili. Wakati mwingine hata utofauti wa Hoja humfanya mwanachama mmoja aitwe msaliti.
Mtiririko wa matukio ya kuitana wasaliti ndani ya CHADEMA nilianza kuyasikia uchaguzi wa BAVICHA, baadaye tukayasikia akituhumiwa mheshimiwa Shibuda, yakaenda kwa Mh. Zitto Kabwe, yakamaliza na kuwachinjia baharini akina Mtela Mwampamba na Juliana Shonza na kundi lake,
Historia inanikumbusha ni suala la tuhuma za Usaliti zilizoisambaratisha NCCR- Mageuzi, chama kilichokuwa maarufu miaka yetu ya 90. Kundi la Mrema liliwatuhumu kundi la Mabere Marando kuwa ni wasaliti na Kundi la Mabere Marando lilimtuhumu Augustino Mrema na kundi lake kuwa wanatumiwa na CCM na Serikali. Kutokana na tuhuma hizo, viongozi na wanachama wa kila kundi wakawa busy na kupanga mashambulizi dhidi ya kundi lingine kila kukicha. Hatima yake ni kurushiana viti na majaribio ya kutaka kuuana katika Hotel ya Mkonge huko Tanga na huo ukawa ndio mwanzo wa kifo cha NCCR-MAGEUZI.
Ninaona tatizo hili linainyemelea CHADEMA, tatizo hili linahitaji kutibiwa, CHADEMA inahitaji kujenga demokrasia ya kukosoana bila kuchukiana na kuhisiana vibaya. Wanachama wa CHADEMA wamekuwa waoga kutoa mawazo yatakayokinzana na wanachama wenzao na hasa viongozi fulani fulani kwa kuogopa kuitwa wasaliti.
Na kutokana na udhaifu huu ni rahisi sana adui kupenya. Kwa mfano katika mkanda wa video unaonyesha Lwakatare akipanga njama za kuteka, kushambulia na kudhuru mtu. Sababu inayotajwa kuandaliwa kwa mkakati huo ni Zitto Kabwe. Kuwa Mh. Lwakatare alikuwa anapanga njama za kigaidi dhidi ya mwandishi wa habari kwa kile kilichosemwa ukaribu wake na Zitto. Sasa unajiuliza shida iko wapi kuwa karibu na Zitto Kabwe, majibu katika video hiyo hiyo yanasema anadhofisha juhudi za chama, kwa kifupi ni msaliti.
Sijui kama video hiyo ya kweli au si ya kweli, na wala sihitaji kujua hilo, Lakini, Sababu ya hisia za USALITI ndio chanzo cha uwepo wa video hiyo. Sasa kama video hiyo ni ya kweli, basi utaona kuwa idara nzima ya ulinzi na usalama chini ya Lwakatare ilivyopoteza dira, Badala ya kushughulikia ulinzi na usalama wa chama kutoka kwa maadui wa kweli imejikita kwenye hofu hofu ya kusalitiwa. Kama hiyo video sio ya kweli utaona kuwa maadui wametumia kuwepo kwa hali ya kutokuaminiana ndani ya CHADEMA na hivyo imewezekana kutengeneza video hiyo kwasababu ya mwanya uliotengenezwa na CHADEMA yenyewe, mwanya wa hisia za usaliti.
Sasa hivi ndani ya CHADEMA ili uonekane wewe ni mwanaharakati wa kisiasa wa kweli, na mpenzi wa CHADEMA wa kweli ni lazima uongelee watu wanaohujumu jitihada za chama, lazima uzungumzie watu unaodhani hawako upande wenu. Sasa wanachama wa CHADEMA hawazungumzii tena Itikadi ya chama, Hawazungumzi tena hoja za mipango mikakati ya chama inayohusiana na maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi, watu wako busy na nani anatuangusha wapi na kwa vipi na wasababu zipi.
Sasa badala ya kuwa kwenye mapambano dhidi ya mpinzani wa CHADEMA anayefahamika CCM mapambano yamebadirishwa na kuwa ni mapambano kati ya kundi moja la CHADEMA dhidi ya kundi lingine la CHADEMA, hii ni HATARI sio tu kwa CHADEMA yenyewe bali hata kwa ustawi wa Demokrasia ya nchi yetu na Afrika kwa ujumla.
Niwasihi viongozi wa ngazi ya juu wa CHADEMA warudishe ajenda muhimu kwenye meza za mazungumzo za wanachama wao, kufanya juhudi za makusudi za kuondoa hisia za hujuma na usaliti na kuwafanya wanachama wajione wao ni kitu kimoja, wenye nia na lengo moja wanaoenda njia moja.