Dhana ya ukuaji wa uchumi

Dully47

New Member
Aug 25, 2022
1
0
Utangulizi.

Kwa maisha ya kawaida tunapozungumzia Uchumi ni shighuli zote za binadamu zinazolenga kutekeleza mahitaji ya binadamu ya Kila siku. Dictionary ya Economist's imefafanua Uchumi kama " Utafiti wa uzalishaji,usambazaji, na matumizi ya utajiri katika jamii ya wanadamu.

Hivyo basi kwa jamii za Sasa na hata zilizopita maendeleo ya kiuchumi yanazingatiwa kwa kuangalia Watu Binafsi na nchi kwa ujumla kwa kuzingatia kiwango chake Cha uzalishaji.

DHANA YA UKUAJI WA UCHUMI.
Katika kipengere hiki UKUAJI WA UCHUMI ni ongezeko linalotokea katika Pato la Taifa au Pato la kitaifa kwa Kila mtu wa nchi Fulani kwa kipindi Cha muda Fulani. Kwa maana hiyo ikiwa pesa ambayo Kila mtu anayo inakua inasemekana kuwa Kuna ukuaji Mkubwa wa Uchumi.

Sambamba na hili na ndio maan China ni nchi tajiri zaidi duniani lakini sio kwa sababu Kila mtu ni tajiri hapana, Bali ni kutokana na uwingi wa pesa walizokuwa Nazo, kwa hivyo wakati wakati wa kuamua ukuaji wa nchi Kuna mambo kadhaa ya kuzingatia kwa sababu ikiwa tunajizuia tu kwa mizani michache, matokeo yanaweza sio ya kweli
 
Back
Top Bottom